Thursday, March 20, 2014
Busu la hongera kwa mwana
Mama mkubwa na mdogo wakimpongeza binti yao Mwajuma Pembe wakati wa hafla fupi ya kumfunda iliyofanyika kijijini Kisemvule hivi karibuni.
Zawadi ya mwavuli
Bi. Mwajuma Pembe akiwa na zawadi yake ya mwavuli aliyozawadiwa wakati wa harusi yake iliyofanyika nyumbani kwao Kisemvule, wilayani Mkuranga. HONGERA
Wednesday, March 19, 2014
Ajali barabara ya Morogoro
Ajali inapotokea ni hasara tupu kwa gari na biashara. Angalia jinsi mahindi yalivyasambaratika katika ajali hii.
Alama za barabarani
Alama za barabarani zimesimikwa kando ya barabara ya Tanzania-Zambia. Swali, madereva wanazielewa maana ya alama hizi na kuzitumia?
Betty na Agnes akina mama Watafiti wachumi
Betty Chalamila kushoto na Agness Ndunguru ni watafiti wachumi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wakiwa kwenye kikao cha kazi cha kuandaa taarifa ya Followup Survey ya mradi wa EAAPP kilichofanyika mjini Morogoro mwezi Machi 2014
Ajali barabara ya Morogoro
Barabara ya Morogoro haikosi ajali. Pichani ni ajali ya magari tanker za mafuta iliyotokea Chalinze hivi karibuni. Moja ya sababu za ajali za mara kwa mara inasemekana ni madereva kusinzia.
Monday, March 10, 2014
Mtalii ndani ya kibajaji
Vibajaji ni uasafiri unaopendwa sana na watalii kati ya Mto wa Mbu na Monduli. Pichani mtalii akiwa ndani ya Bajaj.
Shabiki wa Yanga - kutoka mji wa Mto wa Mbu-Manyara
Ushabiki wa mpira wa miguu nchini Tanzania ni wa timu mbili ni Simba na Yanga. Hapa Mto wa Mbu nilimkuta shabiki huyu wa Dar Young Africans. Kwa mtindo huu Mbeya City wana kibarua kikubwa cha kuwa mabingwa wa Tanzania!
Mfereji msafi -Mto wa Mbu
Moja ya vitu vilivyonivutia nikiwa Mto wa Mbu-Manyara ni kuona mifereji misafi sana na iliyotengenezwa kwa uimara wa hali ya juu. Nikawa nalinganisha na ile mifereji iliyopo jijini Dar Es Salaam. Loh kichefuchefu! Angalia pia jinsi sehemu ya waenda kwa migu na baiskeli ilivyotengwa.
Moja ya Mitaa ya Mto wa Mbu-Manyara
Huu ni mmoja wa mtaa wa Mto wa Mbu mkoani Manayara. Sehemu hii ni ya bonde. Mafuriko yanapotokea ni balaa. Lakini sehemu hii ni maarufu kwa kilimo cha Mpunga na mbogamboga. Hivi sasa kimeanza kuwa maarufu kwa watalii.
Wakulima wa Mto wa Mbu mafunzoni
Subscribe to:
Posts (Atom)