Saturday, October 25, 2014

Mzee 'Kutapatapa' wa Parokia ya Vikindu




Mzee 'Kutapatapa' ni maarufu Parokiani Vikindu. Hufanya kazi kwenye nyumba ya Mapadri wa Shirika la Vincentian  ni mcheshi, mkarimu na mchapa kazi. Leo asubuhi aliwasaidia na kuwaelekeza madada hawa wadogo kutoka shirika la Carmel jinsi ya kubeba ngazi. Kudos! 'Kutapatapa'

Chai ya asubuhi baada ya misa ya mavuno

 
Leo asubuhi misa ya mavuno Jumuiya ya Mt. Vincent -Parokia ya Vikindu, imeadhimishwa. Baada ya misa tulipata chai ya pamoja iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ndg. Faustini Onyango.(hayupo pichani)

JESUS TOWN-Vikindu


Je, unafahamu mahalipo paitwapo Jesus Town? Poa-Jesus Town iko Vikindu ndani ya Parokia. Pichani ni makazi ya Mapadrei na Seminari ya Vincetian Fathers.

Je ni kubana matumizi au ubahiri?

Ana mizigo mingi mwingine ameubeba kichwani

Alipochoka ilibidi aupakate 
Hii ni hatari. Kama safari hii ni ya Ubungo stand, kwa kweli kazi ipo. Je ni kubana matumizi? Usalama wako je?

Cardinal Polycarp Pengo

Huyu ndiye Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam- Kanisa Katoliki- Cardinali Polycarp Pengo

Askofu Edgar Marantha


Askofu Edgar Marantha ndiye aliyebariki Altare ya Kwanza ya Parokia ya Magomeni tarehe 25/09/1965

Mtoto wa UTATU MTAKATIFU akisoma NENO

Mtoto huyu anaanza mapema kuizoea adhira (watu wengi) akikua atakuwa jasiri hataogopa kuongea mbele za watu na pia atajifunza ni kipi cha kuongea, kwa wakati gani na wapi. Wakatoliki tuwapeleke watoto wetu wajiunge na Utume wa Watoto wa Utatu Mtakatifu.

Wachina Kanisani Magomeni

    Kuna Wachina pia Wakatoliki nani anabisha?

Friday, October 24, 2014

Kanisa la Magomeni katika sura Mpya

Kanisa la Magomeni linavyoonekana sasa. Limekarabatiwa na kutoka na sura hii, kweli linapendeza. Mwaka wa kesho Parokia ya Magomeni inatimiza miaka 50 tangu ianzishwe. Kwa kuwa familia yetu imeishi Magomeni kwa muda mrefu, hii ni Parokia yangu. Hapa ndipo nilipobariki ndoa yangu mwaka 1997. TUMSIFU YESU KRISTU. AMINA (Picha kwa hisani ya Silivester Jakka fb)

Maria - a.k.a Mc Bonge sasa ni journalist!

Maria Yuda - a.k.a MC-Bonge (Kulia) mwaka huu amehitimu rasmi mafunzo yake ya uandishi wa habari. Nimekuwa nikimsikia kwenye Tumaini Radio akisoma habari sijui wameshampa ajira huko? Hongera sana Maria- Utafika mbaliiiiii. (Picha kwa hisani ya Slivester Jakka fb)

Walinzi wa Vatican

Hawa ndiyo walinzi wa Vatican. Usicheze  kabisa, kaa mbali nao. Bado wanalinda kwa mikuki. Vao yao je? Wako kiutamduni zaidi kuliko unavyofikiri wewe.(Picha kwa hisani ya Silivester Jakka fb)

Kaburi la Lazaro

Siyo hadithi hili ndilo kaburi la Lazaro ambalo kwamo,Bwana wetu Yesu Kristo alimfufua.

Alhamisi Kuu-Magomeni

Mwaka huu Ibada ya misa ya Alhamisi Kuu  katika Parokia ya Magomeni iliendeshwa na Kardinali Polycarp Pengo (Picha kwa hisani ya Silivester Jakka fb)

Matawi yametoka Vikindu

Kwa mara ya kwanza mwaka huu, parokia nyingi za jimbo kuu la Dar Es Salaam zimenunua matawi yake kutoka parokiani kwetu Vikindu. Mwaka huu Jumapili ya Matawi Parokiani Magomeni iliazimishwa na Muhashamu Baba Askofu Nzigilwa (Picha kwa hisani ya Silivester Jakka fb)

Anafanya kama alivyofanya Yesu Kristo

Mbele ya wenzetu lazima tujitoe na tunyenyekee. Tukio hili hutokea siku ya Alhmisi  Kuu ya kila mwaka. Wakati Wakatoliki tunapokumbuka mateso ya Bwana Wetu Yesu Kristu. (Picha kwa hisani ya Silvester Jakka  fb)

Credo Silima-Mpiga kinanda maarufu wa Parokia ya Magomeni

Credo Silima akikwangua keyboard kanisani Magomeni (Picha kwa hisani ya Silivester Jakka fb)

Kwaya ya Mt. Antoni wa Padua-Magomeni


Hiki ni kikundi mojawapo cha Kwaya katika Kanisa Katoliki Parokia ya Magomeni- Kwaya ya Antoni wa Padua. Ni kwaya ya vijana zaidi. (Picha kwa hisani ya Silivester Jakka fb)

Kwaya kongwe jimboni Dar- Mashahidi wa Uganda

Hii ni moja ya kwaya kongwe kanisa katoliki jimbo Kuu la Dar Es Salaam- Ni mashahidi wa Uganda mwakani itatimiza miaka 50. Hii ndiyo kwaya iliytuimbia siku ya harusi yetu Bw & Bibi IJbanzi - aka Banzi wa Moro family. Banzi Simba na kwaya nayo Simba! AMINA (Picha kwa hisani ya Silivester Jakka fb)

Chagua mchumba



Vijana watanashati wa Kitanzania. Hawa walisimamia moja harusi zilizofungwa jijini Dar (Picha kutoka Silivester Jakka fb)

Sababu ya kuchanga

Wengi wetu tunachangia harusi na sendoffs ili tujumuike na wenzetu katika kinywaji. Iwe bia au soda! (Picha kutoka Silivester Jakka fb)