Baadhi ya vitu vya mahali vilitolewa ukumbini siku ya kumuaga Bi. Neema Timothy Kirway. Inawezekana hii ni mila ya utamaduni wa Wairaq. Babu, Bibi, Mama na Baba, wajomba,baba wadogo, mama wadogo,shangazi na wadogo zake Neema walipata mgao wao.Kwa kweli ilipendeza sana. Jamani eeh tuuenzi utamadani wetu.
Monday, November 17, 2014
Neema Kirway-Mahali ukumbini
Baadhi ya vitu vya mahali vilitolewa ukumbini siku ya kumuaga Bi. Neema Timothy Kirway. Inawezekana hii ni mila ya utamaduni wa Wairaq. Babu, Bibi, Mama na Baba, wajomba,baba wadogo, mama wadogo,shangazi na wadogo zake Neema walipata mgao wao.Kwa kweli ilipendeza sana. Jamani eeh tuuenzi utamadani wetu.
Wednesday, November 12, 2014
Tido Muhando-Mwandishi nguli
Huyu ndiye Mwandishi wa habari wa Kimataifa Dunstan Tido Mhando. Mwandishi mahiri na mtangazaji pia. Enzi zake alipokuwa Radio Tanzania alikuwa akitangaza vizuri sana kipindi cha michezo na hasa matangazo ya moja kwa moja ya soka. Alipokuwa BBC alikuwa akitupasha habari kemkem kutoka Bara la Afrika. Amefanya mahojiano na marais mashuhuri wa Bara la Afrika akiwemo Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere, Hayati Laurent Kabila aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Rais Paul Kagame na Rais Yoweri Mseveni. Katika mahojiano yake na Hayati Laurent Kabila ilibainika kuwa alikuwa shabiki mkuwa wa klabu ya Soka Simba ya jijini Dar, Tanzania.
Kilimo cha bia
Kilimo cha bia. Shamba limeandaliwa vizuri. Variety ya mbegu (bia) inaonekana na spacing inaonekana vizuri tu tena zimepandwa kwa mstari. Zitavunwa lini? Hatujui na matarajio ya mavuno kwa hektari ni bia ngapi. Kweli duniani kuna mambo kila mtu anafikiri nini na ni kipi ni kipaumbele chake. Mtu kufikiri kupanda bia ili azivune nyingi basi upeo wa juu kabisa wa kufikiri. Picha hii nimeipata kwenye mtandao wa fb kuna wengi waliotoa maoni yao kuhusu picha hii wengine walibaki kutoa sentensi za kushangaa na wengine walidai pengine ndio zitakuwa kali zaidi!
Monday, November 10, 2014
'Togwa limeingia nzi'
Mdudu nzi kwa asilimia kubwa hapendwi na wanadamu. Mbwiga wa Mbwiguke wa Clouds huwa anasema kuwa 'Togwa limeingia nzi.' Ninavyoelewa mimi togwa ni kinywaji baridi cha asili hasa kwa watu wa Pwani ni tamu kwa sababu huongezwa sukari kwa maana hiyo lisipotunzwa vizuri mdudu nzi hunyemelea na kwa kuwa nzi ni mdudu mchafu, anapoingia kwenye togwa basi hulichafua na kuwa halifai tena kwa kunywa. Utafakari usemi huu.
Huwezi kuwakataza watoto wa familia
Watanzania tumekuwa na tabia mbaya ya kuandika kwenye kadi kuwa watoto hawaruhusiwi kwenye hafla za harusi na sendoffs. Lakini huwezi kuwakataza watoto wa familia. Watajifunzaje kushughulikia matukio haya muhimu wakati tunawakataza? Pichani watoto wa Familia ya Mbetwa wakiwa ukumbini siku ya harusi ya baba yao mdogo Mpoki. Angalia jinsi wanavyoburudika na soda!
Subscribe to:
Posts (Atom)



