Monday, September 7, 2015

Siasa za Tanzania-Niwakumbushe miezi miwili iliyopita







Wanafunzi kwenye kijiji cha utamaduni-Swaziland

Ni muhimu kwa wanafunzi kufahamu utamaduni wao na kuupenda. Pichani wanafunzi wa shule ya sekondari Swaziland wakiwa ndani ya ukumbi wakiangalia ngoma za utamaduni wa Swaziland. Huu ni utaratibu mzuri wa kuwajenga vijana hawa na kukua wakiwa wazalendo na kuupenda utamaduni wao.

Mazingira mazuri ya kujifunza- Mananga


Haya ni mazingira mazuri ya kujifunza  chuoni Mananga-Swaziland. Nilikuwa huko mwezi Agosti 2015 nikipata utaalamu katika masuala ya 'project management'

Monday, August 31, 2015

Kutoka 1980-2015 Wana TOSA wakutana

Schoolmates- TOSAMAGANGA HIGH SCHOOL- Kutoka kushoto Packshard Mkongwa, Nicodemus Mboje na John Banzi. Tulipokutana Double View Hotel, Sinza tarehe 29/08/2015. Ilikuwa siku nzuri sana ajabu. Lengo ni kumpongeza John Mboje kwa kufunga ndoa na binti mrembo -cheupe (picha ya chini). Tuliwapongeza kwa niaba ya TOSA alumni. Asanteni sana. Watoto wameshakuru na kufurahi kwa mzigo!
(pichani)

Wataalamu nje ya nchi

Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wakiwa mafunzoni-Mananga, Swaziland

Bwawa la kuogelea-Chuoni Mananga

Pembezoni  mwa mabweni, ukumbi wa starehe na dinning hall kuna bwawa la kuogelea ambalo husafishwa na kujaza maji safi kila siku. Hapa ni chuoni Mananga- Swaziland

Familia inapowapa "company"

Waafrika tuna mapenzi makubwa. Tulipotembelea Afrika ya Kusini, dereva wetu pamoja na familia yake (mke na mtoto pichani- wengine ni wa Tz Dr. Nkuba na Bw. Mjema) walisafiri nasi na kutuelekeza kila tulichotaka kuelewa wakati wa safari hiyo. Binti huyo mdogo anaitwa Nashera.. kuna wakati aliponiona nakuja akaongea kwa Kiswati .....'mkulu' akiwa na maana mkubwa au mzee anakuja  alifurahi kwamba sasa safari itaanza kuendelea kama kawaida kwani mkulu ameshaingia ndani ya gari. Hata kwa Kiliguru 'mkulu' ina maana ni mkubwa kweli Waafrika wengi ni Wabantu!

Nje ya nyumba ya asili ya Waswati

Tulipotembelea Mantenga Cultural Village nchini Swaziland, nilivutiwa na nyumba hii ya asili. Ni nyumba imara isiyovuja na imejengwa kwa ustadi mkubwa huko ulinzi ukipewa kipaumbele bila kusahau kuwapanga watu kwa jinsi wakati wa kulala humo ndani na huku bibi akilala kati kati.Haki wazee wetu walikuwa na lojik na falsafa zao katika maisha.

Moja ya sehemu za maduka jijini Mbabane

Nchini Swaziland watu wengi hupendelea kununua mahitaji yao kwenye maduka makubwa. Hata wanafunzi hufurika kwenye maduka hayo wakati wa jioni. Unaweza kuliona kwa mbali duka moja linalouza bidhaa za Mr. Price hasa nguo.

King Mswati wa III hutawala na mama yake

Nchi ya Swaziland inaongozwa na Mfalme - King Mswati wa III. Huyu huongoza nchi yake kwa kushirikiana na Mama yake  kwa hiyo kimadaraka kwanza ni King halafu Mama na anayefuata ni Waziri Mkuu ambaye pia huteuliwa na King. Angalia jinsi picha zilivyobandikwa.

Kuelekea Afrika ya Kusini




Kundi letu tulipata bahati ya kutembelea mji wa Afrika ya Kusini ambao hauko mbali sana na Swaziland. Mji huu unaitwa Nelspruit ni makao makuu ya jimbo la Mpumalanga. Nilivutiwa na barabara nzuri. Na kweli kwa mwendo wa masaa takribani mawili sikuweza kuona ajali barabarani!

Mazingira murua ya kujifunza chuoni Mananga



Mara nyingi nilikuwa mimi na facilitator wangu darasani mwangu nikiwa na vifaa muhimu ikiwemo kompyuta mpakato kwa kuwa nilitengenezewa moduli ya peke yangu kwa kile nilichotaka kujifunza. Pichani ni mmoja wa facilitator, Mr. Vincent Loveday

Agosti - Kwa Mswati III

Wiki mbili za mwezi Agosti nilikuwa nchini Swaziland  kwa mafunzo ya muda mfupi kuhusu Project Management kwenye chuo cha Mananga pale Ezwilini. Mafunzo yaliyoniongezea utaalamu kuhusu menejimenti za miradi pamoja na masuala mtambuka kama jinsia na mazingira.

Monday, July 13, 2015

Alinena kwa lugha za kimataifa


Hii ilikuwa Arusha mwaka huu

Tunasubiri ya Dodoma mwaka huu pia

Anacharaza kinanda


   Ningependa kucharaza kinanda kama anavyofanya huyu.

Altare nyumbani kwa Nkwera

Jumuiya ya Mt.Joseph Mfanyakazi ilipoazimisha  siku ya somo wa Jumuiya tarehe 2/5/2015. Wanajumuiya walikusanyika nyumbani kwa Mwl. Angriberth Nkwera na kusali pamoja. Altare ya Mungu inapohamia nyumbani kwake ni jambo la kumshukuru Mungu.

Tunaandaa database ya uwekezaji katika sekta ya kilimo

Kwa kushirikiana na Bill and Melinda Foundation na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika pamoja na wale wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi wakiwa katika mafunzo ya kuandaa database hiyo.

Hii ni familia yangu


Ndiyo. Hii yote ni familia yangu. Ni siku mtoto wetu Frt. Linto alipokuja kutuaga pale nyumbani Kisemvule. Frt. Linto anatoka India, lakini kwa takribani mwaka mmoja alikuwa parokiani kwetu Vikindu  kwa uchungaji. Alipopewa vazi la kuwa Frateri yeye alituomba mimi na mke wangu (Nancy) kuwakilisha wazazi wake ambao wasingeweza kuwepo siku hiyo. Kwa hiyo Linto ni mmoja wa familia yangu. Kwa sasa Ftr. Linto yuko Uganda kwa muda baadaye ataelekea Nairobi kwa masomo ya Teolojia.Pichani pia wanaonekana  waseminari ambao walikuwepo kwa mwaka mmoja parokiani kwetu wakianza mafunzo ya useminari kwa sasa wako Uganda.

Ilibidi kuweka kumbukumbu na watoto hawa




Junior na Herieth wa Buguruni ni watoto marafiki. Nilipowatembelea nyumbani kwao nilifurahishwa jinsi walivyokuwa wakishirikiana. Wanacheza pamoja na kula pamoja. Junior ni Mluguru na Herieth ni Mchagga. Ushirikiano waliounyesha ni dalili nzuri kuwa hata wazazi wao wanashirikiana. Hii ndiyo Tanzania umoja unajengwa toka tukiwa wadogo. Nami niliona ni heri nikapiga picha ya kumbukumbu pamoja nao.