Saturday, February 27, 2016
Kama tuko Matombo vile
Furaha ilipelekea mimi na shangazi yangu Paulina (Mama Mloka) kucheza ndani ya Kanisa kama vile tuko ndani ya kanisa la Mt. Paulo nyumbani Matombo. Ni furaha baada ya Bw na Bi Macarios Banzi kufunga ndoa tarehe 6/2/2016. Muone Binti Mwl na msinga wake na mimi mwanae Banzi nikiwa na kitu kinachoitwa 'Mambatsa' 9kishoka kidogo cha kuchezea ngoma).
Wasimamizi wa harusi ya Bw & Bi Macarios Banzi katika ubora wao
Mbwembwe nyingine za upigaji picha huwa zinaniacha hoi kabisa.Picha ya juu huyo mtoto aliyepiga akiangalia kulia ndiyo kivutio cha picha hiyo. Lakini hawa wote ni wasimamizi wa harusi ya harusi ya Macarios na Martina (Mr & Mrs M.Banzi) siku ya tarehe 6/2/2016 kanisani Vikindu. Wasimamizi wa Kuu ni Mr & Mrs Gaitan Banzi
Harusi ya Macarios Banzi-Tunatua kanisani
Ni kawaida watun kuhudhuria reception na si ibada takatifu ya ndoa. Kwa Macarios Banzi ilikuwa ni kinyume. Ndugu,marafiki,jamaa na wageni waalifika walifika Kanisani kwa ibada. Pichani ndugu waliokuwa nyumbani Kisemvule wakishuka katika bus maalum tayari kwa ibada hiyo kanisani Vikindu tarehe 6/2/2016
Thursday, January 21, 2016
Karafuu kijijini Konde-Matombo-Morogoro
Pengine wengi wetu tunafikiri kuwa Karafuu inastawi visiwani Pemba na Unguja tu. Hapana, huko Morogoro vijijini katika kijiji cha Konde tarafa ya Matombo, karafuu hustawi pia. Hii ni karafuu iliyooteshwa kijijini hapo. Wakulima wa Konde wameanza kufaidika na kilimo cha karafuu na kubadili maisha yao kutokana na kilimo cha zao hilo.
Jengo la UWT katika ubora wake
Hili jengo (Mfano wa Meli) ni Kitega Uchumi cha Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Lipo kando ya makutano ya Barabara ya Kawawa na Ally Hassan Mwinyi pale Morocco, Dar Es Salaam. Jengo hili kwa kweli ni zuri na linavutia. Ni ubunifu mkubwa umetumika katika kuchora mchoro wa jengo hili. Ndani ya jengo hili kuna ofisi za mashirika mengi ya binafsi, serikali na ya kimataifa. Hapa ndipo yalipo makao makuu ya Kampuni ya simu ya Airtel-Tanzania. Aidha hapa ndipo yalipo makao makuu ya "Presedential Delivery Bureau" (PDB) ya Big Results Now.
Friday, January 15, 2016
Sijachelewa-Happy New Year
Kweli sijachelewa. Heri na Baraka za mwaka mpya 2016. Nilishindwa kabisa kuwaaga. Ah, mambo mengi bwana. Mwaka 2015 haukuwa mzuri sana kwangu. Misiba, na kukatika kwa mara kwa mara kwa umeme kumezorotesha mawasiliano yangu kupitia Blog hii, Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2015 niliweza kuning'iniza posts 257 tu ukilinganisha na posts 956 mwaka 2014. Sababu nyingine kubwa ni kuibuka kwa njia nyingine ya mawasiliano hasa Facebook. Mwaka 2015 nimeweza kuweka posts nyingi kupitia facebook za group mbalimbali.Wakati mwingine nimetumia muda mwingi kujishughulisha na Whatsapp. Kilichonipa nguvu kwenye facebook na whatsapp ni kupata feedback kutoka kwa wadau ukilinganisha kwenye blog ambapo ni nadra kupata feedback.
Hata hivyo mwaka 2015 mafanikio haykukosekana kwangu binafsi na kwa familia. Nimeweza kukutana na ndugu na jamaa kupitia vikundi mbalimbali hasa 'Africana Group' (Pichani). Nimeweza kushiriki shughuli za Kanisa
Kura nilipiga na kushangilia nyumbani kwangu Kisemvule na kumpata Rais, Mbunge na madiwani.
Nawatakia mwaka mpya wa mafanikio na pia tuimarishe mawasiliano kwani maisha ni kuwasiliana.
Hata hivyo mwaka 2015 mafanikio haykukosekana kwangu binafsi na kwa familia. Nimeweza kukutana na ndugu na jamaa kupitia vikundi mbalimbali hasa 'Africana Group' (Pichani). Nimeweza kushiriki shughuli za Kanisa
Kura nilipiga na kushangilia nyumbani kwangu Kisemvule na kumpata Rais, Mbunge na madiwani.
Nawatakia mwaka mpya wa mafanikio na pia tuimarishe mawasiliano kwani maisha ni kuwasiliana.
Subscribe to:
Posts (Atom)







