Wednesday, December 20, 2006

SOKONI KARIAKOO NI TOPE TUPU

Leo mchana nimetokea maeneo ya Kariakoo. Nilipita kabisa karibu na Soko la Kariakoo. Huwezi kuamini, soko hilo tunalojivunia kuwa ni la Kimataifa, hakuna kitu ni tope tupu. Mvua inayoendelea kunyesha hapa Dar es Salaam kwa kweli ni hatari tupu kwa afya zetu. Hebu fikiria mwenyewe karibu mboga na matunda hushushwa sokoni kariakoo na kwenyewe ni kuchafu sasa kweli tutapona?

Miundo mbinu inayolizunguka soko hilo pia ni mibovu, barabara zimechimbika, mitaro imeziba. Lakini waswahili wako pembeni wanajichana chips tu! Umeme nao hakuna, majenereta yanaunguruma, nyumba zinaendelea kujengwa, mikokoteni nayo inakusukuma. Daladala zilizochanika viti basi shida tu. Hili ndilo jiji la DAR ES SALAAM.

Jiji? Rekebisheni mambo hapo kariakoo, ni aibu.

1 comment:

Ndesanjo Macha said...

Soko chafu sana lile. Miaka na miaka jiji la Dar halina mifereji ya kisasa ya kudaka maji wakati masika. Na nchi haina kampeni ya kuelimisha watu madhara ya kutupa takataka kwenye mifereji iliyopo. Nadhani hadi siku tutakuwa na askari wa usafi na kuanza kuadhibu watu kwa kuchafua mazingira kama Singapore na pia kuadhibu wanaokula kodi za soko kama la Kariakoo badala ya kuzitumia kwa ajili ya kuliboresha, basi tutaendelea kuishia na uchafu kama funza.