Leo mchana mimi na wenzangu tunaoshiriki warsha ya kupelemba na kutathmini (M&E) hapa Nairobi tumepata bahati ya kutembelea moja ya kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Kenya (KARI) kinachoitwa NARI-Kabete. Kituo hiki kiko umbali wa kilometa 10 kutoka mjini Nairobi.
Unapoingia kwenye mazingira ya kituo hicho utapata jawabu kuwa hicho ni kituo cha Utafiti kina maabara mengi na vifaa vya kutosha. Hapa shughuli kubwa zinazofanyika ni utafiti wa udongo, magonjwa, Bioteknolojia na utafiti wa sayansi jamii (socio-economic research).
Tulipokuwa tunatembezwa kwenye moja ya screen house makubwa ya kuvutia ya kiutafiti tulijionea na kuelezwa na watafiti wa Kenya. Tunaambiwa kuwa hii ni screen house kubwa barani afrika. Watafiti wa Kenya wamepiga hatua kubwa kwenye nyanja ya biotekenolojia. Wana facility za kutosha pamoja na watafiti waliobobea. Kuna haja ya kujifunza kutoka kwao.
No comments:
Post a Comment