Tuesday, June 9, 2009

Kisemvule wajikita kwenye kilimo cha mbogamboga


Wananchi wa Kisemvule vijana, wajane, na wazee wamejiunga katika vikundi na kuanza kuzalisha mboga za aina mbalimbali kwa ajili ya kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao. Mradi huo unafadhiliwa na TASAF.


Mradi umeanza rasmi mwaka huu na tayari mazao yameshaanza kupandwa na wakati wowote kuanzia sasa yako tayari kuvunwa hasa pilipili hoho. Blog hii ilitembelea kwenye eneo lililolimwa na kujionea mazao mazuri ya bamia, nyanya maji (tomato) na pilipili hoho na nyanya chungu.

Kutokana na mazungumzo na mmoja wa wana kikundi, Bw Maulid Pembe, TASAF imetoa madawa, mbolea na vifaa muhimu vya kilimo cha mbogamboga kama vile mashine ya kumwagilia maji na mabomba. Mategemeo ni kuvuna mboga kwa wingi tatizo ni soko. Kwa mfano aliuliza blog hii kama wanaweza kupata soko la pilipili hoho. Pichani Bw Maulid Pembe akikagua mche wa nyanya chungu uliostawi vizuri.

1 comment:

Unknown said...

hongera kaka kwa jitihada za kuliendeleza taifa kwa kujituma,
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa mwisho UDSM(Jafari Selemani),napenda na ninawazo la kufanya kilimo cha mboga,matunda na ufugaji.Ila sijui nianzie wapi ili nipate anza kilimo baada ya kumaliza tu sitaki kwenda kuajiliwa.nahitaji msaada wako ili tuwe sote ktk uwajibikaji.