Tuesday, November 3, 2009

Vijana wanapaswa kutekeleza kauli mbiu ya KILIMO KWANZA


Ukitembelea katika vijiji vingi hapa nchini hutoshangaa kukuta washiriki wakuu wa kilimo ni wazee. Vijana walio wengi hawajihusishi kabisa na kilimo. Ukiwauliza wanazo sababu nyingi za kutojihusisha na kilimo zilizo nyingi si za msingi. Wakati Taifa linajipanga katika kuitikia kauli mbiu ya KILIMO KWANZA vyema vijana wakaandaliwa ili waifahamu vizuri kauli mbiu hiyo kwa kuwa tayari kwa utekelezaji wake. Kwa hiyo mafunzo mafupi ya uzalishaji wa kilimo yakiandaliwa kwa vijana wetu yatasaidia sana kuboresha uzalishaji wa kilimo. Kilimo kikiachiwa wazee kitakufa.

1 comment:

Bennet said...

Kilimo kwanza kimekaa kisisa zaidi, kama kweli tunataka mapinduzi ya kilimo inatupasa kuachana na jembe la mkono tuanze kutumia angalau maksai, kubota na ikiwezekana trekta, kwa maana hiyo mashamba madogo madogo inabidi tuachane nayo na kuanza kulima kilimo hasa kwenye mashamba makubwa kibepari