Wednesday, February 3, 2010

Tunashtuka tu watu wanapokufa?


Ajali nyingi zinatokea na kupoteza maisha wananchi wengi. Ajali ya gari ni kifo hc ghafla kinashtua na tena kinaacha maswali mengi bila majibu. Jana tena ajali nyingine mbaya imetokea barabara ya Dar - Arusha na kuua watu 24! Hivi tunashtuka tu watu wanapokufa? Baadaye mambo ni kama juzi. Hivi kweli tumeshindwa kudhibiti ajali za barabarani? Kama ndivyo basi kuukomesha UKIMWI ni ndoto! (Pichani - Ajali, Taswira katika Taifa - Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi tar 21 Novemba 2009)

1 comment:

drngarawakessy said...

Kwakeli ni aibu kubwa,wenzetu wanatuambia(prevetnion is better then cure,yani kuzuia ni bora kuliko tiba).Ukweli nikwamba wenda Mw.Mungu ama katuongeza ngozi nyeusi(haswa watanzania)akili nyingi,au tuna kaupungufu wa("elementi")akili.Ajali kuzuilika inawezekana sawa na Maambukizi ya VVU,kinachotakiwa ni kufuata njia sahihi.Lakini njia tunazotumia kuamasisha zikiwa kama "Tumia kondomu timiza haja yako","Kondom kinga madhubuti",filamu ambazo tunaonyesha asubuh,mchana,usiku kw TV mtu akimbusu mpenzi wake,wakilala chumbani.hadi wakifanya mapenzi, tunategemea vijana watapokea ujumbe gani?Wakati akili ya mtoto nikufyonza anyoyasikia na kuona.Unamuonyesha kw TV mtu maarufu akiwa na ereni akiwasiliana na mkwe wakipata kinywaji na k.d.Kw upande wa barabarani wazee wa kazi upewa kitu kidogo basi endesha utakavyo.Ukitaka kujua ya barabarani safiri mikoani na ifadhi 5.000 kama 100000 na endesha kwa fujo,utayaona hayo au panda basi,dereva akienda pole pole basi watu hulalamika nikumpigia makelele,lakini akienda haraka,watu kimya,haya ajali ikitokea yeye mwenye makosa.Usalama barabarani nikitu kidogo tu.Kwa Sub Sahara Africa ni magonjwa 2 tu makuu tatizo:Ni Maambukizo ya VVU/UKIMWI na malaria,tunashindwa kupambana nayo na watu wanakufa mno,wakati wenzetu ata nafasi aitoshi kuyaandika.