Saturday, July 9, 2011

Abiria wanaposubiri chombo bandarini Malindi-Unguja


Hata sehemu ya kupumzika abiria kabla ya kupanda 'chombo' nayo si ya kiwango. Tofauti kabisa na ile iliyopo Dar.

Choo cha Bandarini-Malindi Unguja


Pamoja na mambo mazuri niliyovutiwa nayo nikiwa Unguja hivi karibuni. Choo kile cha bandarini Malindi hakikunipendeza hata kidogo. Pamoja na watalii wengi wanaoingia Zanzibar iweje hapo bandarini kuwepo na huduma ya choo ambacho si cha kiwango?

Karafuu za Zanzibar


Karafuu ni zao maarufu visiwani Zanzibar has kisiwa cha Pemba. Japokuwa ni maua madogo ya kutoa harufu ya kuvutia ambayo hutumiwa kama viungo na hata manukato. Miti ya karafuu ni mirefu na wakati mwingine wakati wa kuvuna ajali hutokea kwa mvunaji kuanguka kutoka kwenye mkarafuu.Pichani ni mikarafuu ya Kizimbani, Unguja.

Utafiti wa Soya

Moja ya tafiti zinzofanyika katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo, Uyole - Mbeya ni kupata aina za mbegu bora za soya. Soya ni chanzo kizuri cha protini ambayo ni muhimu kwa afya ya binadamu.

Mdogo wangu anaipenda Simba


Damas mdogo wangu wa Morogoro ni shabiki mkubwa wa Simba Sports Club ya Dar Es Salaam a.k.a. Wekundu wa Msimbazi. Pale nyumbani Moro chumbani kwake amening'iniza bendera ya SSC. Hata T-shirt zake ni za Simba. Hebu mcheki basi!

Ametoka kwa baba mdogo

Hapa wapi jamani?

'Kocha' yuko Forodhani


Utanitambua? Niko Forodhani-Unguja napunga upepo ati!

Utafiti wa zao la muhogo unaendelea Zanzibar.


Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Kizimbani-Zanzibar ndiyo yenye jukumu la kufanya utafiti kisiwani humo. Nilipotembelea Taasisi hiyo hivi karibuni. Majaribio ya mbegu za muhogo zinaendelea kufanyiwa utafiti ili kuweza kupata mbegu bora inayostahimili magonjwa ya muhogo.

Hilo ndilo Doriyani


Kwa mara ya kwanza kutembelea kisiwacha Unguja mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu, pale Kizimbani niliweza kuliona tunda la Doriyani. Tunda hili lina harufu kali. Limefanana kidogo na fenesi lakini si kubwa sana.

Malongoza mtaalamu wa pilau

Tulipohitimisha 40 ndugu zetu pale Morogoro-Kola, aliyetuandalia chakula alikuwa Bw. Malongoza. Licha ya kuchelewa kufika lakini chakula kililiwa saa 7 mchana nasi wa Dar tuliweza kurudi masikani. Ukikaa na Malongoza utajifunza mengi katika upishi wa chakula cha watu wengi.

Kinu na mchi

Bado tunahitaji kinu na mchi katika maandalizi ya chakula. Hali hii si kwa vijijini hata kwa mjini pia. Pichani mwanamama akitayarisha viungo vya pilau kwa kuvitwanga ndani ya kinu.

Mjomba na Mpwa

Kushoto ni mjomba Charles Mbena na kulia ni mpwa wake Silyvesta Jakka walipokutana nyuymbani Morogoro hivi karibuni.

Tuesday, July 5, 2011

Ndugu wanafahamiana


Unapotembelewa na wajomba

Jumamosi ya tarehe 2/7/2011 tulitembelewa na wajomba kutoka DSM-Ilala wakisindikizwa na dogo Anthony Kunambi.

Wapambe hawakosi



Dada Batsheba, Meab,kaka Inno,Frank, shangazi Mbwala na Bw wote walikuwepo.Umewaona?

Kwa furaha Ana aliimba wimbo




Baada ya kuvikwa pete ya uchumba, dada Ana kwa furaha aliwaimbia wageni akishirikiana na rafiki yake. Baadaye akina mama, shangazi, dada na wadogo walijimwaga. Mzee Crispin Mangengesa Mdimi (Baba mzazi) na Dkt. Gregory Paul Mluge (Mjomba) wote walifurahi baada ya tukio hilo.

Kilichofuata ni hafla ya 'engagement'



Nikueleze?Baada ya kupata mkwanja wa kutoka ..... Kuna nini tena! Ilikuwa ni hafla fupi ya 'engagement'Wahusika walijitokeza hadharani. Kulia ni dada Anna na kushoto ni shem wetu Mlaki. Aliyeshika microphone ni Banzi wa Moro.Hapa sasa ni mshereheshaji.Wakati wa kutoa mahali nilikabidhiwa jukumu na familia kuendesha mchakato wa kutoa na kupokea posa.Waandishi wa habari wa vyombo vyote hapa nchini walishuhudia tukio hili.

Tunapokea mahali



Baba alipokea chake, mama alipata mkaja wake, babu alipata kichana ndevu, shoka na panga pia ni baadhi ya vitu vya posa. Dada Vicky Mdimi alipokea fedha kwa niaba ya familia na kaka mtu Kamsopi Mdimi alipokea shoka na panga na baadaye kukabidhiwa wahusika. Akina Ngowi walilijizatiti kweliwkeli. Kilichofuata .........

Karibuni!



Siku ya Jumapili tarehe 3/7/2011. Familia ilipokea posa ya dada yetu Ana Mdimi anayeolewa na Bw. Pichani shangazi anagalagala chini kwa mila na taratibu za kimanda mpaka afichuliwe na wakwe ndipo wakaribishwe!

Paroko Tomy alisimamia maandamano



Maandamano ya kuabudu Ekaristi Takatifu Parokia ya Vikindu.Father Tomy mbele ya Watoto wa Utatu,waimbaji waliimba kwa shangwe.Watoto walishiriki kikamilifu katika maandamano.

Maandamano Parokiani-Vikindu Jimbo kuu la Dar Es Salaam



Sakaramenti hiyo twaiabudu kifudifudi na sheria za zamani zikomeshwe na hiyooo. Yafichaikayo machoni imani huyaona. Wimbo huu ni maarufu sana siku ya Sikukuu ya Ekaristi Takatifu nilianza kuiimba nikiwa katika Parokia ya Mt.Paulo Matombo,Morogoro.

EKARISTI TAKATIFU

Tarehe 26/6/2011 Wakatoliki waliazimisha sikukuu ya Ekaristi Takatifu. Pichani chombo kinachong'aa ni 'MONSTRANCE' kule kwetu Matombo tunaiita 'Monstrandi'

Friday, July 1, 2011

Taasisi ya Utafiti Kizimbani -Zanzibar




Hapa ndipo Makao makuu.Utafiti wa Mpunga - NERICA unaendelea.Na mahojiano yalifanyika pia ofisini kwa Mkurugenzi wa Taasisi - Dr. Salehe Haji

Mwanakwerekwe


Na hapa ndipo Mwanakwerekwe. Ni mahali maarufu Zanzibar.

Na hizi amejenga mtoto wa Karume


Mhe. Amani Abeid Karume alifuata nyayo za baba yake na kujenga flats hizi.

Makutano ya Legezamwendo na Bubu


Hapa barabara mbili zinakutana. Moja ni Legezamwendo na nyingine ni Bububu. Ukienda Kizimbani sharti upite hapa.

Bahari imetulia


Bahari ikitulia unaweza hata kufanya kazi na Laptop!

Bahari ikichafuka!



Bahari ikchafuka. Abiria chomboni ni kama uonavyo.

Flats alizojenga Sheikh Abeid Amani Karume

Majengo haya ni kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume. Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la mapinduzi Zanzibar hapa ni Michenzani-Unguja.

Wanafurahia boat

Kama hakuna mawambi ni raha kusafiri na boat.

Hiyo ndiyo bahari ya Hindi

Bahari ya hindi imetulia tuli!

Ndani ya boat

Nje ya boat juu kwa mbele.

Nje ya Boat Je?

Azam Marine


Unaposafiri kwenda Unguja kwa kutumia boat. Boat yenye uhakika na raha na Azam Marine na hii ndiyo ofisi yao - Dar