Friday, August 19, 2011
Banzi wa Moro
Chini kulia miaka 37 iliyopita nikiwa Njombe Secondary School - FORM ONE. Nyuma yangu ni Library ya shule!Juu kushoto mwaka huu nalishwa keki na Mamaa- nyumbani Kisemvule, Mkuranga, Pwani.Taja tofauti 5 za picha hizo.SHUKRANI KWA MUNGU
Tuesday, August 16, 2011
Lugaluga wanalima na kuuza
Kama tunataka wakulima wetu wasinyonywe na wakione kilimo kinalipa wazalishe na kuuza wenyewe huku wakimiliki zana za usalishaji na ikiwezekana na miundo mbinu. Lugaluga wameshaanza kufanya hivyo. Kinachowakwimisha ni miundo mbinu ya umwagiliaji na barabara safi za mashambani. Hilo linatakiwa kufanyiwa kazi.
Lugaluga walikuwepo 8/8
LugaLuga Agricultural Marketing and Cooperative Society kulikuwepo kwenye maonyesho ya wakulima ya mwaka 2011 kwenye uwanja wa maonyesho-Morogoro. Walioneysha zana wanazotumia (matrekta madogo na makubwa) ambayo wanamiliki wanachama kupitia Ushirika wao. Bidhaa wanazozalisha- Mpunga, alizeti na mahindi. Hao ndiyo Lugaluga waliojizatiti kuondoa umaskini kupatia Ushirika.
Wakorea wanataka kuibadilisha Pangawe
Katika muda wa miaka mitano ijayo, Wakorea wanataka kukibadilisha kijiji cha Pangawe kilichopo wilaya ya Morogoro vijijini kuoenakana cha kisasa zaidi kikiwa na miundombinu ya umwagiliaji, barabara za mashambani, shule bora ya msingi, maji safi huduma ya afya, umeme na huduma nyingine. Tusubiri tuone. Kazi hiyo inafanywa na KOICA-Korea Interanational Cooperation Agency.
Tunatarajia kupata aina mpya ya kunde
Banda la utafiti wa Kilimo mwaka 2011
Banda jipya la Utafiti - Morogoro
Wizara ya Kilimo na Chakula imeanza kujenga banda jipya la Utafiti na Maendeleo katika viwanja vya Nane Nane - Morogoro na kuanza kutumika katika maonyesho ya mwaka huu.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti kanda ya Mashariki - Dr. Chaboba Mkangwa, banda hilo likikamilika litakuwa likitowa huduma za mikutano na shughuli nyingine muhimu za Wizara katika viwanja hivyo.
Hivi sasa Kibungo Juu
Tunalisha na kuhifadhi ardhi
Majani yajulikanyo kwa jina la mabingobingo yanatumiwa na wakulima wa Kibungo Juu wilayani Morogoro vijijini kwa kulishia mifugo hasa mbuzi na nguruwe pamoja na kuhifadhi ardhi. Pichani mkulima akimuonyesha Banzi wa Moro majani hayo katika banda la Maonyesho ya Idara ya Hifadhi na Matumizi Bora ya Ardhi.
Kijana na Kilimo cha Nyanya- Kibungo
Kijana huyu aliyekuwa kwenye banda la maonyesho la Idara ya Hifadhi na Matumizi Bora ya Ardhi alinieleza jinsi alivyojifunza kilimo bora cha nyanya juu ya milima ya Kibungo na kusema kuwa kwa mara ya kwanza magari ya mizigo yalipanda mlimani kubeba mazao ya mbogamboga ambayo yamemsaidia sana kuongeza kipato chake.Pichani akiwa kwenye bustani ya maonyesho ya nyanya.
Utunzaji wa Ardhi ni pamoja na ufugaji bora
Wakulima kutoka Kibungo Juu
'LUP' yafanya kweli 8/8 Moro
Idara ya Hifadhi na Matumizi Bora ya Ardhi ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imefanya kweli katika maonyesho ya Wakulima (Nane Nane) 2010 kanda ya Mashariki mkoani Morogoro wameleta wakulima halisi kutoka Tarafa ya Kibungo wilaya ya Morogoro vijijini. Wakulima hawa wanashiriki katika mpango wa kuhifadhi vyanzo vya maji pamoja na utunzaji na matumizi bora ya ardhi.
Tuesday, August 2, 2011
Na mashine ya kupura mpunga je?
Moja kazi ngumu katika kilimo cha mpunga ni kupura (kutoa punje kwenye mmea). Kwa wakulima wadodo hutumnia njia nyingi iliyo maarufu ni kuupiga kwa kutumia fimbo au kufikicha majani.Unapopiga mpunga uliotandazwa chini mara nyingi ubora wake huathirika sana hasa mchele kuwa na mchanga na harufu ya udongo. Kwa kutumia mashine hii ya Wakorea (pichani) kazi huwa nyepesi na ubora wa mchele huongezeka hivyo kumvutia mlaji.
Teknolojia ya umwagiliaji
JK afungua maonyesho ya Wakulima 2011
Monday, August 1, 2011
Kariakoo usiku
The Banzis
Wajumbe wa Africana wakisikiliza kwa makini
Mwenyekiti wa Africana awataka wanakikundi kulipa ada za uanachama
Tarehe 17/7/2011 kikundi cha Africana kilichopo jijini Dar kilifanya kikao chaker cha mwezi nyumbani kwa Bw. Gaitan Banzi huko Kimara Temboni. Moja ya maazimio makuu yaliyotolewa kwenye kikao hicho ni kuwataka wanakikundi kukamilisha malipo ya ada ya kila mwezi kuanzania mwaka jana hadi Desemba 2011. Pichani Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Innocent John Banzi akitoa msisitizo wa jambo hilo.
Subscribe to:
Posts (Atom)