Monday, April 30, 2012
Huko ndiko kuagwa
Ukiona sanduku, ujue safari imeiva. Pichani Bw. George Ng'atigwa, akimuaga dada yake Adela Nga'tigwa wakati alipowakabidhi rasmi ukoo wa Kavia (mume mtarajiwa) katika ukumbi wa Magadu ulipo ndani ya Kambi ya Jeshi la Wananchi-Mzinga siku ya tarehe 28/4/2012.
Bw na Bibi Ng'atigwa
Hawa siyo maharusi bali wazazi wa Bi Adela Ng'atigwa Bw. Na Bibi Ng'atigwa wakiwa pamoja kwenye sherehe ya kumuaga binti yao iliyofanyika katika ukumbi wa Magadu Leaders Club mjini Morogoro tarehe 28/4/2012
Dada Adela Ng'atigwa akiingia ukumbini
Dada Adela Nga'tigwa akiwa na mpambe wake Imaculata Banzi wakiingia ukumbini Magadu Leaders Club Morogoro siku ya Jumamosi tarehe 28/4/2012 tayari kwa sherehe ya sendoff.
Tuesday, April 24, 2012
Jirani wa Chuo cha Nelson Mandela -Arusha
Jirani huyu amejenga karibu kabisa na Chuo cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.Ni nyumba nzuri na ya kisasa huenda atapata wateja!
Uanikaji nguo maghorofani
Ni tabia iliyozoeleka na baadhi yetu kuanika nguo ovyo ovyo. Juma la jana Banzi wa Moro alifanikiwa kunasa jengo hili likiwa na nguo zilizoanikwa barazani. Hili ni jengo la ghorofa, ni kubwa na zuri lililoko kati kati ya jiji la Dar Es Salaam. Hivi kweli hii ni tabia nzuri ya kuanika kila kitu nje? Huu nao ni uchafu.
Uvunaji wa maji ya mvua
Shule ya Msingi Kisemvule iliyoko wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imebahatika kuwa na mradi wa uvunaji maji. Maji haya hutumika kwa shughuli mbalimbali yanafaa pia kwa kunywa ila inashauriwa kuwa ni vizuri kuyachemsha kabla ya kunywa.
Ukitaka kwenda Kigogo
Juzi nilitembelea maeneo ya Kigogo. Barabara ya Kigogo kwa sasa ni nzuri na mabus yanayotumia njia hiyo ni mazuri na makubwa. Pichani ni njiapanda ya Kigogo. Hapa ndipo unapoweza kuunganisha mabus ya kwenda Kigogo, Mburahati na hata Manzese.
Monday, April 23, 2012
New Kisemvule Butchery
Mwekezaji amewahi Kisemvule. Sasa tuna duka la nyama. Zamani ilitubidi kupata kitoweo pale Vikindu au Mbagala. Sasa hivi nyama wakati wowote. Haya ni maendeleo yanayokuja kwa kasi katika kijiji ninachoishi, Kisemvule-Mkuranga.
Friday, April 20, 2012
Doreen Nyanjura
Msichana Doreen Nyanjura wa Uganda hivi karibuni alitawala vyombo vya habari vya Uganda na Afrika Mashariki baada ya kukamatwa na kutiwa ndani kwa sababu ya kuandika kitabu kiitwacho "Is it The Fundamental Change?"
Doreen ana umri wa miaka 22 na ni mwanafunzi wa chuo kikuu. Sifahamu kilichoondikwa ndani ya kitabu hicho kwani sijakisoma. Lakini kutokana na makala ya Padri Privatus Karugendo (Raia Mwema Aprili 18- 24,2012 baadhi ya nukuu ambazo zimenisisimua kwenye kitabu hicho kama alivyonukuu Karugendo ni "Maisha yanaelekea mwishoni, siku tunapokaa kimya kwa mambo ya msingi" na "Dunia inateseka, si kwasababu ya vurugu na maasi ya watu wabaya, bali ni kwa sababu ya ukimya wa watu wema".
Nimesisimka kuona msichana wa miaka 22 kuandika ambacho kinaanza kuleta changamoto! Hongera sana Doreen Nyanjura na pole kwa kutiwa kolokoloni!
Tunawachia nini watoto hawa?
Vituko vya Iddi Amin Dadah
Wednesday, April 18, 2012
Ah, magogo tena!
DARLIVE yetu
Uchafu karibu na KTM ya zamani
Huu si ustaarabu
Adha ya Traffic jam-Barabara ya Kilwa
Duka la viatu vya Bata
Thursday, April 12, 2012
Tukubali Dar chafu
Siku ya jana mvua kubwa ilinyesha jijini Dar. Nilishuhudia mafuriko katika mto Kizinga. Baadhi ya maeneo ya Tandika nyumba zilibomoka.Uchafu ulijitokeza waziwazi kwenye mitaa ya Tandika, Temeke na Mbagala. Mifereji imeziba maji hayatiririki kwenye mitaro iliyojengwa. Kila aina ya uchafu ulisambaa kirahisi kabisa. Mifuko ya plastiki, chupa, matambara, miwa, matunda, matairi chakavu na vingi vingi. Ni uchafu ambao umekuweko kwenye mitaa yetu kwa siku nyingi bila kushughulikiwa. Nina imani kuwa kuna kampuni za usafi zinazolipwa na jiji au Manispaa husika. Hizi zinafanya kazi gani je zinapata malipo bila kazi? Manispaa kwanini zimeshindwa kusimamia usafi? Mbona Moshi wameweza. Hakika ukifika Moshi utadhani ndiyo makao makuu ya Tanzania kwa jinsi maeneo yalivyo safi. Moshi kila mmoja ni askari wa usafi. Tukubali Dar Chafu!
Tuesday, April 3, 2012
Mawasiliano na Banzi wa Moro
Kuanzia sasa unaweza kuwasiliana na Banzi wa Moro kwa kutumia email addresses zifuatazo:- banzi.john@yahoo.com;jlsbanzi@gmail.com
kuna wasomaji wangu wengi walikuwa wakiuliza mbona siwajibu wakinitumia msg kwa email ya jbanzi@hotmail Ndugu zangu hii ilishibiwa na wajanja siku nyingi kwa hiyo nilikuwa siitumii lakini ilikuwa inaonekana kwenye blog yangu ingawa mimi nilikuwa natumia hiyo ya gmail.Leo nimempata mtaalamu wa IT hapa Mananga Centre na kunirekebishia mamboos.Vitu sasa safi kabisaa.Byebye hotmail.Na pole sana aliyeningilia hata kama hajui Kiswahili habari ndiyo hiyo!
Nauli za mabus Tanzania hizi hapa
Heshimu lugha ya mwenzako
Mambo ya mpakani
Squarters za Maputo
Jinsia inazingatiwa chuoni Mananga
Wimbi la kujiendeleza kitaalamu haliangalii jinsi ya mtu. Hapa chuoni Mananga idadi ya wanachuo ukizingatia jinsi ni asilimia 50 wanawake na asilimia 50 wanaume. Wanawake wana nafasi sawa na wanaume na kwa hakika wanawake wanapewa kipaumbele zaidi. Hata waajiri wameshaliona hilo ndiyo maana hali ni kama nilivyoieleza.
Msafiri Kafiri!
Msafiri kafiri.Ndiyo methali tuliyoizoea nyumbani Tanzania. Nikiwa Maputo Msumbiji hivi karibuni nilithibitisha uhalisia wa methali hiyo. Tukitokea Swaziland (nyumbani kwetu) tulijiandaa kwa vitafunnwa na vinywaji. Tulipofika Maputo tulipata kifungua ndani ya gari letu tulilosafiria. Mimi nilipata kipande cha kuku sehemu ambayo huwa siipendi!Tuko ugenini, safarini-Kweli Msafiri Kafiri.
Madafu- Maputo kama Dar!
Monday, April 2, 2012
Kila mlo - Juice
Inawezekana
Essau Banda (katikati) ni Mhasibu - Benki Kuu Malawi na pia ni Mchungaji(Pastor).Tupo naye Swaziland hapa chuoni Mananga. Juzi tulisafiri naye kwenda Maputo Msumbiji. Kabla ya kuanza safari yetu tuliomba mmoja wetu aombe kwa sala ili Mungu aibariki safari yetu. Banda alijitokeza na kuomba sala fupi na nzuri.Kwenye bus nilikaa karibu naye pembeni yake kulikuwa na kitabu. Nilimuomba kukisoma ndipo nipogundua kuwa Banda ni mchungaji baada ya kusoma ukurasa wa kwanza ulioandikwa Pastor Essau Banda! Ona, Banda hajawahi kujionyesha kuwa ni mchungaji au mlokole. Na pia sikutegemea kuwa na mchungaji akisoma mambo ya dunia hapa Mananga, kumbe yote inawezekana!
Sunday, April 1, 2012
Bus linapovuta trailer la mizigo
Ushuru wa barabara-Maputo
Subscribe to:
Posts (Atom)