Friday, June 29, 2012
Wengine hawana nafasi
Alipoona hana nafasi alitafuta nafasi yake ili angalau aweze kushuhudia kinachoendelea (mtoto juu ya gogo la mkorosho)
Zambia fedha nyingi kunyakua ubingwa Afrika
Waziri wa Michezo wa Zambia, Chisimba Kambwili amesema Serikali ya Zambia ilitumia kiasi cha Kwacha 1.2 bilioni (Dola 235,865) kwa ajili ya kuiandaa timu ya taifa ya soka ya Zambia "Chipolopolo" iliyotwaa ubingwa wa Afrika 2012.
Kambwili alisema baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa Afrika wachezaji walipewa posho mbalimbali ambazo zilifikia Kwacha 11.5 bilioni (Dola 2,260,380).
Waziri huyo alisema hayo katika Bunge la Zambia wakati alipokuwa akijibu swali aliloulizwa ni kiasi gani cha fedha kilitumika kwa ajili ya kuiandaa Chipolopolo iliyotwaa ubingwa wa Afrika 2012 na kiasi gani wachezaji hao walipewa baada ya kushinda ubingwa huo wa Afrika.
Hata hivyo waziri huyo aliiponda Serikali ya zamani ya Zambia iliyokuwa ikiongozwa na chama cha siasa cha MMD.Alisema Serikali iliyopita ilikuwa ikigombana mara kwa mara na Shirikisho la Soka la Zambia (FAZ). Waziri Kambwili alisema Serikali iliyopita ya Zambia chini ya Rais Rupiah Banda ilimuajiri kocha wa timu ya taifa Dario Bonetti bila kuomba ushauri kutoka FAZ hali iliyoonyesha na kusababisha soka la Zambia kushuka.
"Kama watu wa Zambia wasingekiweka chama cha PF madarakani na kuunda serikali, basi kombe la Mataifa ya Afrika lisingekuja Zambia. Ninao ushahidi wa ninachokisema, watu wengi Zambia wanajua, dunia inajua kwamba Serikali ya MMD ilimleta kocha Bonetti bila kuishauri FAZ," alisema Kambwili.
"Soka ilikuwa imepoteza mwelekeo, chama cha PF kilipoingia madarakani na mimi kuingia wizara ya michezo hatukukuta bajeti ya kuiandaa timu ya taifa kwa sababu ya uongozi wa Serikali iliyopita ilikuwa haifanyi kazi vizuri na FAZ,viongozi walikuwa wakifanya hivyo ili FAZ, ionekane haiwezi kazi yao," alisema Kambwili.
Alisema chama cha PF chini ya Rais Michael Sata kiliposhinda uchaguzi na kuunda Serikali ya Zambia kiliandaa bajeti ya kuisaidia timu ya taifa na kuiweka timu kambini nchini Afrika Kusini.
"Serikali ya MMD ilikuwa haitaki timu iweke kambi Afrika Kusini na ilikuwa inataka timu iweke kambi Ndola, lakini PF tulipoingia madarakani tuliwapa FAZ fedha na timu ikaweka kambi Afrika Kusini kwa sababu ya kulingana hali ya hewa na nchi za Guinea ya Ikweta na Gabon zilipokuwa zikifanyika fainali za kombe la Mataifa ya Afrika 2012, matokeo yake Zambia ikatwaa ubingwa wa Afrika.
"Hivyo napenda kuwaambia viongozi wa chama cha MMD kwamba hawakufanya chochote katika ubingwa wa Afrika wa Zambia, ila ubingwa huo ulitokana na mipango mizuri ya chama cha PF," Alisema.(Habari na picha kwa hisani ya gazeiti la Mwananchi 29/6/2012). JE KUNA UKWELI WA MAELEZO HAYA? TAFAKARI
Utafiti wa malisho ya mifugo
Watafiti wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo Tanga (LRC-Tanga) wanaendelea kukusanya aina mbalimbali za majani ya malisho na kuyafanyia tathmini kuweza kufahamu lishe iliyomo kwenye majani hayo na matumizi yake kwa mifugo.
Handeni-Mkata mwisho wa lami
Sehemu kubwa ya matengenezo ya barabara kutoka Handeni kwenda Mkata ikiunganisha barabara kuu ya Chalinze Segera imeshakamilika kwa kiwango cha lami lakini bado haijaanza kutumika.
Inaitwa 'Segere'!
Ndivyo alivyonieleza mama wa Kimasai (aliyeficha uso ili asipigwe picha) niliyemkuta Handeni mjini akiendesha biashara yake, nilipomhoji kifaa kinachoning'inia kwenye nguzo chenye urembo mzuri! Sasa sijui ni segere matata au vipi lakini wengine huita 'utunda', 'chachandu'....
Haya ni mateso
Mkazi wa Kariakoo, jijini Dar Es Salaam, Pyarali A.Pyarali (35) anasumbuliwa na maradhi ya kuvimba miguu. Mwananchi huyu alitembelea ofisi za Mwananchi Communications Ltd Tabata Relini jijini Dar Es Salaam kuwasilisha kilio chake kwa wasamaria wema kumsaidia ili aweze kupatiwa matibabu kutokana na maradhi yanayomsumbua. Binafsi hana fedha za kumudu gharama za matibabu.(Picha na maelezo kwa hisani ya gazeti la Mwananchi 29/6/2012). Wito tuisifiche maradhi punde tuyapatapo.Maradhi hayachagui rangi, dini wala kabila. TUJITOKEZE KUMSAIDIA.
Askofu Mtanzania kuongoza Idara ya Uinjilishaji Vatican
PAPA Benedict XVI amempandisha cheo na kumteua Askofu wa Jimbo la Kigoma wa Kanisa Katoliki, Protase Rugambwa kuongoza Idara ya Uinjilishaji akiwa pia Rais wa Baraza la Kipapa la Umisionari. Kwa uteuzi huo wa Juni 26, mwaka huu ambao ulitangazwa na Shirika la Habari la Kipapa, Fides Agenzia, Askofu Rugambwa sasa atakuwa na hadhi ya Askofu Mkuu. (Chanzo cha habari- Gazeti la Mwanachi 29/6/2012)
Tanesco yatangaza neema
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) limetangaza kuwa wateja wote walioomba kupata huduma ya kuunganishiwa umeme kwa muda mrefu wanapaswa kuwa wameunganishiwa umeme ifikapo Juni 30 2012 kwani kwa sasa shirika hilo lina vifaa vya kutosha hayo yamesemwa na Msemaji wa Shirika hilo Bi Badra Masoud. "Hakuna mfaynyakazi wa Tanesco anayepaswa kumzungusha mteja hivyo mteja yeyote atakayezungushwa awasiliane na makao makuu ili waweze kushughulikiwa. Tutatoa namaba maalum ili wateja ambao watakuwa wanasumbuliwa na wafanyakazi wetu waweze kutupigia moja kwamoja na sisis tutashughulika nao," alisema.(Chanzo cha habari-Gazeti la Mwananchi 29/6/2012)
Mchango wa 'Development Partners' kwa utafiti
Shughuli za utafiti wa kilimo zinahitaji usafiri wa kuaminika kwahiyo mchango wa wabia wa maendeleo (DPs)wa kutoa vyombo vya usafiri (pichani) utarahisisha kutekeleza shughuli za utafiti kwa wakulima
Mama ametimiza miaka 70
Familia ya Mloka wakati wa tafrija ndogo ya kumpongeza mama yao Paulina Mloka kutimiza miaka 70 mwezi huu. Ndani ya picha yupo Freddy Mloka,Doreen Mloka,Petty Mloka na Ceasar Mloka (Watoto wa Mama P.Mloka)
Nguzo ya familia miaka 70
Mwezi wa sita 2012 shangazi yangu Paulina Ephrem Kibena (Mama Mloka) ametimiza miaka 70 akiwa na nguvu na afya tele. Bila kutegemea watoto wake Fredy, Doreen, Petty na Ceasar (The Mlokas) walimuandalia tafrija fupi ya kumpongeza. Shangazi Pau ni kiungo mkubwa kwa familia yetu. Wengi tumepitia kwenye malezi yake, ametusomesha na kutuozesha amefanya kuwa karibu na ndugu na jamaa wengine. Msimamo wake umesaidia sana kuijenga familia mahali ambapo ipo. Ninakupongeza sana shangazi yangu kwa kutimiza umri huo wa miaka 70 MUNGU akupe afya na maisha marefu zaidi. AMINA
MC wa Familia
Hivi karibuni dada Petty Mloka ameonyesha umahiri mkubwa wa kuendesha sherehe au 'MC' kiasi kwamba sasa hivi familia yetu haina tatizo la kukodi MSHEREHESHAJI iwe kwenye sikukuu ya Ubatizo, Ekaristi, Kipaimara, Sendoff na hata Reception ya harusi. Hongera sana dada PETTY!Tunafanya mpango wa kukutafutia vyombo!
Utafiti wa viazi vitamu
Watafiti wanaendelea na utafiti wa kupata aina bora ya viazi vitamu yenye lishe nzuri, inayostahimili magonjwa na wadudu waharibifu. Kituo cha Utafiti wa Kilimo - Kibaha kinafanya kazi hiyo kwa kukusanya aina mbalimbali za viazi na kutafiti ili kuweza kupata aina bora ya mbegu za viazi kwa mazingira tofauti na kukidhi mahitaji ya walaji.
Utafiti wa muhogo - Kibaha
Kituo cha Utafiti wa Kilimo- Kibaha kilichopo mkoani Pwani kinaendelea na utafiti wa zao la muhogo. Kwa mujibu wa Afisa Utafiti Kilimo Mkuu Bwana Marton Muhana, aina ya muhogo unaopendwa na wakulima na walaji kwa ukanda wa Pwani ni aina ya 'kiroba' kwa maelezo zaidi tembelea kituo cha Kibaha (Pichani mtafiti Muhana akitoa maelezo kwa timu ya ufuatiliaji na tathmini ya shughuli za utafiti inayoongozwa na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP)
STK 933 kijijini Handeni
Magari aina ya Toyota Landcuiser 'mkonga' yanafaa sana kwa barabara za vijijini ambazo ni za udongo. Magari haya inabidi yananuliwe kwa wingi na kusambazwa kwenye vituo vya utafiti kwa shughuli za utafiti kwenye mashamba ya wakulima (Pichani STK 933 YA Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika-Idara ya Utafiti na Maendeleo ikiwa kijijini Handeni hivi karibuni katika shughuli za kufuatilia na kutathmini shughuli za utafiti Kanda ya Mashariki mwaka 2011/12)Wtafiti
Thursday, June 28, 2012
'Masaki ya Handeni'
Hivi ndivyo tulivyoona wigo katika kijiji kimojawapo cha Handeni. Ni ubunifu wa hali ya juu. Karibu kila nyumba kijijini hapo kumezungushwa wa wigo wa majani haya kwetu tunaita 'kigomvi' kijiji hiki kina usafi wa hali ya juu. Sote tulishangazwa na tulichokiona utafikiri Masaki!
Dr. Everina Lukonge
Afisa Kiungo wa Kanda ya Mashariki
Lawrence Alphonce Kadeng'uka a.k.a Kade kwa sasa ni Afisa Kiungo wa Utafiti, Ugani na Mkulima Kanda ya Mashariki. Makao Makuu yake yako Kituo cha Utafiti Ilonga, Kilosa-Morogoro. Kade huratibu masuala yote yanayohusiana na usambazaji wa teknolojia za kilimo kanda ya Mashariki anaongea na watafiti, wagani pamoja na Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa wakulima wanapata Teknolojia bora kutoka kwa watafiti, wagani wanasambaza teknolojia hizo kwa kutumia njia sahihi katika mazingira husika. Hatimaye wakulima wanazitumia teknolojia hizo katika kuboresha uzalishaji wa mazao na mifugo hivyo kuinua kipato chao na kuboresha uchumi wa nchi.
Utafiti wa ngozi
Ukielezwa thamani ya ngozi na jinsi walanguzi wanavyowaibia wafugaji unaweza kulia.
Watafiti wa kituo cha Utafiti wa Mifugo Tanga wameanza kutafiti jinsi ya kuboresha thamani ya ngozi kuanzia uchinjaji wa wanyama, uchunaji ngozi, utayarishaji ngozi, utunzaji na hata kuitafutia masoko. Mtafiti Masakia kutoka kituo hicho anaeleza kuwa kipande kidogo cha ngozi ya mbuzi kwa kawaida huko vijijini mkoani Tanga huuzwa kwa shilingi 300 lakini kikiandaliwa vizuri kinaweza kuuzwa kwa shilingi 15,000. Hivyo hivyo kwa ngozi ya ng'ombe ambayo wafugaji huuza kipande kwa kiasi cha shilingi 2,000 hadi 3,000 lakini walanguzi hukiuza hadi shilingi 150,000/- kwa ukubwa unaofanana.Utafiti unaoendeshwa katika wilaya ya Handeni utawawezesha wafugaji kuboresha ngozi na kuboresha vipato vyao. Ngozi ni mali!(Pichani Mtafiti Bariki Masakia akitoa maelezo ya utafiti wake wa kuongeza thamani ya ngozi).
Mwanakikundi na fundi (Bw. Saidi) wa bidhaa za ngozi mjini Handeni akionyesha mkanda aliotengeneza kutokana na ngozi ya mbuzi iliyoongezewa thamani.Mwanakikundi ambaye ni fundi akionyesha cherehani yake anayoitumia kwa kushona bidhaa zinazotokana na ngozi.Hapa ndipo Halamashauri ya Handeni inapoweza kutoa mchango wake mkubwa kwa vikundi hivi kwa kuwapatia mashine bora na mtaji wa kupanua shughuli wananchi wanaojihusisha na utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na ngozi hivyo kuwaongezea kipato chao na kipato cha Halmashauri kutokana na makusanyo ya kodi.
Analisha mbung'o
Chakula cha mbung'o ni damu. Hivyo mbung'o wanaofanyiwa utafiti kituoni TTRI-Tanga hulishwa damu ya wanyama (mbuzi au ng'ombe).Kutunza mbung'o wa utafiti ni zoezi gumu na ni gharama. Linahitaji umeme wa uhakika wakati wote, wafanyakazi wanaojituma na uangalifu wa hali ya juu. Kwani kosa dogo tu linaweza kusababisha mbung'o wengi kufa. Mbung'o wanaofugwa hutumika kitaalmu katika kutokomeza mbung'o wengine.Wananchi wengi hawajui kinachoendelea hapo kituoni na wengine hutua habari za uongo kuwa kituo hicho hushughulika na unyonyaji wa damu hiyo si kweli ni vizuri wananchi waweze kutembelea kituo hicho na kujionea wenyewe jinsi watafiti wetu wanavyoshughulika na utokomezaji wa mdudu hatari mbung'o ambao husababisha ugonjwa wa malale kwa binadamu na ndigana kwa wanyama hatimaye vifo.Hawa ndiyo mbung'o wanaofugwa.
TTRI katika kutokomeza Mbung'o
'Tsetse and Trypanasomiasis Research Institute' (TTRI) kilichoko mkoani Tanga ni kituo mahiri kinachojishughulisha na utafiti wa mbung'o na ndorobo. Kituo hiki chenye historia tangu mwaka 1971 kilipoanza kama Mradi wa Utafiti wa Mbung'o kimefanya makubwa katika kutokomeza mbung'o ambao husababisha ugonjwa hatari wa malale kwa binadamu na ndigana kwa wanyama. Mwaka 1997 walifanikiwa kutokomeza wadudu hao visiwani Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ijulikanayo kwa jina la International Atomic Agency (IAEA) kwa kutumia teknolojia ya 'Sterile Insect Technique' (SIT).
(Pichani Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Furaha Mramba akitoa maelezo kwa timu ya ufuatiliaji na Tathmini kwa shuguli za Utafiti chini ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo -ASDP)
Hiki ni moja ya kifaa kinachotumiwa katika utafiti wa ndorobo ni pekee Afrika Mashariki na ya Kati.
Mitego ya mbung'o
Wednesday, June 27, 2012
Sayansi ipo kituo cha Utafiti Mikocheni
Sayansi ipo Mikocheni.Hii ni maabara bora kabisa ya baiteknolojia hapa nchini chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.Kwa sasa watafiti katika kituo hiki wanaendelea na tafiti za kupata mbegu bora za muhogo zinazohimili magonjwa hatari ya muhogo.
Karibuni LRC-Tanga
Ndivyo anavyosema Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo- Dr. Julius Bwire. Hapa tulipta maelezo ya shughuli zilizofanyika kwa mwaka 2011/12 kuanzia utafiti, ukarabati wa majengo, ununuzi wa vifaa, na mafunzo. Hakika LRC kwa kipindi kifupi imebadilika kabisa kuna ubunifu mkubwa wa shughuli za utafiti na miundo mbinu imeanza kukarabatiwa.
Tanga-Mombasa ni kuteleza!
Barabara ya kutoka Tanga kwenda Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania kwa kiasi kikubwa imekamilika hivi ndivyo alivyoikuta Banzi wa Moro akiwa kwenye shughuli za kikazi wilayani Mkinga mkoa wa Tanga. Tanga-Mombasa sasa ni kuteleza tu!
Utafiti wa mbolea kwenye mahindi
Utafiti huu unafanyika wilayani Handeni kwa ushirikiano wa wakulima na watafiti wa kituo cha utafiti cha Mlingano kilichoko mkoani Tanga. Hapa tulipata maelezo kutoka kwa wakulima kuwa mbolea ya DAP imeonyesha matokeo mazuri ukilinganisha na mbolea nyingine. Jaribio halijafikia tamati. Watafiti watatuandikia kuhusu jaribio hili pindi watakapomaliza utafiti wao.
Nyumbani kwa mkulima Handeni
Hivi karibuni tulikuwa tunatathmini shughuli za utafiti kanda ya mashariki hususan mikoa ya Tanga na Pwani.Pichani tupo kijijini Magamba wilayani Handeni mkoa wa Tanga nyumbani kwa mkulima. Nyumba ni bora,anafuga mbuzi na kuku pia hulima muhogo na mahindi kwa chakula na biashara. Tunataka wakulima wetu angalau wafikie hatua hii.Vijana wataacha kukimbilia mijini.
Utafiti shambani kwa mkulima - Muheza
Ndivyo wafanyavyo watafiti wa kituo cha Utafiti Mlingano Tanga (soma bango) wakulima na watafiti wanashiriki kwa pamoja katika utafiti na kutoa tathmini yao kutokana na walichokiona
WASIFU WA DR.GREGORY P.C.MLUGE
Picha ya ukumbusho wa Dr. Gregory P.C.Mluge (katikati)enzi za uhai wake akiwa na mkewe Restituta (wa kwanza kushoto) wakitambulishwa na mpwa wao Inno Banzi wakati wa sherehe za komunio ya kwanza ya watoto wake nyumbani kwao Kisemvule-Pwani
Dr. Gregory Paul Constance Mluge alizaliwa tarehe 12 Machi 1937,wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambako baba yake Mwalimu Paul Lugonzo alikuwa anafundisha. Dr. Gregory Mluge alizaliwa katika familia ya Bw.Paul Lugonzo na Bibi Annastazia Hugo Mlachuma. Alikuwa mtoto wa pili kwenye familia ya watoto saba wakiwemo wanawake watano na wanaume wawili. Kati ya hao Sr. Philomena, Janeth, Rosemary na Frederick wametangulia mbele ya haki. Waliobaki ni Beatrice na Dolores.
Marehemu Dr.Mluge alianza masomo yake ya msingi huko Bagamoyo na baadaye familia ilirudi Matombo, Kiswira ambako marehemu Paul Lugonzo aliendelea kufundisha katika Shule ya MsingiMatombo.
Dr. Mluge alisoma shule za msingi Matombo na Bigwa. Aliendelea na masomo ya sekondari shule ya wavulana Tabora na baadaye shule ya sekondari maarufu hapa nchini ya Pugu. Dr. Mluge alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere , Kampala Uganda kutoka mwaka 1960 hadi 1965 ambako alipata shahada yake ya kwanza ya udaktari.
Alianza kazi ya udaktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam. Baada ya mwaka mmoja alihamishiwa hospitali ya mkoa Tabora. Baada ya muda aliteuliwa kuwa daktari mkuu wa wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora mwaka 1967. Hapo Nzega alikutana na afisa wa wauguzi ambaye alimpenda kwa jina Restituta Emmanuel Assenga wa Rombo Mashati mkoani Kilimanjaro ambaye alimrushia ndoana ya huba naye Restituta akanasa. Ukawa mwanzo wa uchumba na hatimaye kufunga ndoa.
Dr. Mluge alipewa ‘scholarship’ ya kwenda Uingereza kuendelea na masomo ya udaktari bingwa mwaka 1969. Huko Uingereza alisomea diploma ya ‘Tropical Public Health’, katika chuo cha London School of Tropical Medicine na kupata stashahada. Mwaka 1971 huko Uingereza alipokea tena stashahada ya ‘Tropical medicine and Hygiene’. Mwaka 1972 hadi 1973 alisoma na kuhitimu shahada ya uzamili ya ‘Occupational medicine’ kutoka chuo kikuu cha London. Mwaka huo huo pia alisomea na kupokea shahada ya ‘Industrial health’ na mwaka 1973 hadi 1975 alipata shahada ya tatu ya medicine na cheo cha MRCP kutoka chuo kikuu cha London.
Alifanya kazi katika hospitali bingwa mbalimbali nchini Uingereza kuanzia mwaka 1975 hadi 1980. Alipendwa sana na madaktari wenzake na wagonjwa wake wote. Mtoto wake pekee Janeth Mluge Schoemaeiker alizaliwa mwaka 1978. Mwaka 1980 Dr. Mluge aliajiriwa kama Proffessor wa udaktari na afya ya Jamii na mwalimu wa madaktari wadogo katika Chuo Kikuu cha Jeddah nchini Saudi Arabia. Mwaka 1989 alirudi Tanzania kufanya kazi zake mwenyewe, lakini mwaka huo huo aliombwa na serikali ya Saudi Arabia kurudi tena na kuendelea na kazi ya Proffessor huko. Alifanya kazi huko pamoja na mke wake Restituta ambaye alikuwa Mkurugenzi huko Saudi Arabia. Familia ya Dr. Gregory Mluge iliamua kurudi Tanzania mwaka 2006.
Dr. Gregory Mluge alikuwa ni mtu aliyependa sana watu wote, mkarimu sana, aliyewasaidia watu wengi katika nyanja zote za maisha ikiwemo kitabibu, kielimu, kiushauri na mengine mengi ambayo nina imani itahitaji muda mwingi kuyataja yote. Dr. Mluge alikuwa ni mtu mwenye msimamo wa kweli. Alikuwa mkweli, mvumilivu sana, daktari mzuri na mpole sana. Na kwa hayo yote tunasema AHSANTE SANA.
Dr. Mluge alikuwa mpenzi wa kilimo,ujenzi,na magari lakini ‘hobby’ yake kubwa ilikuwa muziki, na katika hilo alikuwa bingwa wa kupiga kinanda.
Marehemu Dr. Mluge ameacha mjane, mtoto mmoja ,wajukuu wawili na dada wawili.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA! NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI….AMINA.
Saturday, June 16, 2012
Paul Wilbart
Mama Mloka
Subscribe to:
Posts (Atom)