Monday, March 31, 2014
Petty Mloka kanisani Matombo
Petty Mloka (kushoto) akifuatilia kwa makini ibada ya Misa takatifu ya kumuombea baba yake Balozi Daniel Mloka miaka 20 tangu aiage dunia hii. Kumbukumbu ilifanyika tarehe 22/03/2014 kijijini Matombo, Morogoro kushoto ni mtoto wake Nia .
Ibada ya kumbukumbu ya Miaka 20 ya kifo cha Balozi Daniel Mloka
Cesar Mloka na watoto wake Jews na Jordan wakiwa ndani ya Kanisa Katoloki Parokia ya Matombo wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya kumbukumbu ya Baba yake Marehemu Balozi Daniel Narcis Mtonga Mloka iliyofanyika tarehe 22/03/2014 kijijini Matombo,Morogoro.
Kaburi la mjomba Dr. Gregory Paul Constance Mluge
Dr. Mluge alikuwa mwema na mpole. Profesa wa Tiba. Dr Mluge aliiacha Dunia hii akiwa anapendwa.TUTAKUPENDA daima (Tafsiri yangu) . Ni mmoja wa wasomi waliotukuka wazaliwa wa Matombo mkoani Morogoro. Alizaliwa tarehe 12 Machi 1937 na kufariki tarehe 9 Juni 2012. Amezikwa kwenye makaburi ya Kanisa lake Parokia ya Matombo alikobatizwa na kupata, komunio na Kipaimra. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. AMINA
Darini kwa waimbaji kanisani Matombo
Nilibahatika kusali njia ya msalaba Ijumaa ya tarehe 21/04/2014 kanisani Matombo. Nilipogeuka nyuma na kutazama juu nikaona sehemu ya darini walipokuwa wakikaa waimbaji na kuimba Noel ! Noel !ajaye Mtu MUNGU! au Mkristu Miye niko salama shetani wee usinijie......Hakika siku zinapita kwa kasi na mabadiliko ni mengi. Wakati huo kinanda kilikuwa kikiporomoshwa na Babu marehemu Mwl. Paul Lugonzo au Marehemu Mwl. Isdori Baggo.Mungu awalaze mahali pema peponi AMINA. Siku hizi waimbaji wanaimba wakiwa mbele kanisani na huku kinanda kikiwa chini!
Sehemu ya 'Kupolisi' kanisani Matombo
Nilipokuwa mdogo nilimsikia Babu yangu Mzee Mwl. Ephrem Kobelo a.k.a Mzee Vibaya akinieleza kuwa sehemu hiyo iliyotengwa kanisani ni kwa ajili ya 'kupolisi'. Mara nyingi nilimuona Padri akishamaliza kusoma Injili hupanda ndani ya chombo hicho na kuanza kuhubiri. Siku hizi mapdri hawakitumii tena. Akiwa ndani ya chombo hicho waumini waliweza kumuona barabara naye kuwaona waumini. Na ikumbukwe kuwa wakati huo kulikuwa hakuna vipaaza sauti. Pengine sasa hatuhitaji tena chombo hiki kwani tuna vipaaza sauti. Tutawaeleza wajukuu wetu kuwa hiyo ni sehemu ya kupolisi. Huenda Paroko wa Matombo wa sasa Fr. Kobelo atakitumia chombo hiki wakati wa sherehe ya Pasaka mwaka 2014!
Hivi tunataka kuwamaliza hawa?
Kwa uroho wetu wa kupata utajiri wa harakaharaka kuna watu tunaowaita majangili wana mkakati wa kumaliza tembo hawa kwa lengo la kupata meno yao na kuyauza. Tulinde raslimali za taifa wakiwemo tembo. Wakiisha hawatapatikana tena.
Sehemu ya kufanya kitubio kanisani Matombo
Ndani ya Kanisa Katoliki Parokia ya Matombo kuna chombo mahususi kilichotengenezwa kwa kutoa kitubio kwa waumini. Kitubio ni kitu cha siri kati yako na Padri. Padri anamwakilisha mwenyezi Mungu. Wakati huu wa Kwaresima wangapi tumeshafanya kitubio? Je tumeshakuwa na nia makusudi ya kuwaomba tuliowakosea watusamehe? Tafakari.
Twiga akiwa mbugani Mikumi-Morogoro
Mnyama twiga mrefu mwenye ngozi ya kuvutia na mwendo wa madaha anapataikana nchini Tanzania, hasa katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Morogoro, Tanzania
Pundamilia michirizi haifanani
Ukipata bahati ya kuwaona pundamilia wengi unaweza kudhani kuwa michirizi ya ngozi yao hufanana. La hasha, wataalamu wanasema kuwa michirizi ya punda milia ni tofauti kwa kila mmoja.
Mafunzo kazini
Wizara na Taasisi zake hapa nchini hutenga bajeti ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wake kwa lengo la kuleta tija katika utendaji kazi. Pichani wanafunzi na walimu wao kutoka Taasisi ya Taifa ya Tija (NIP) mara baada ya kuhitimu mafunzo mwezi Machi 2014 kituo cha Tushikamane mjini Morogoro. Bi Halima Yusufu wa Idara ya Utafiti na Maendeleo kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanga (wa tatu kutoka kulia waliosimam a mstari wa mbele) ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo kazini aliyegharamiwa na mradi wa EAAPP. HONGERA.
Dadaz wa Magomeni bado wapo
Kikundi cha sanaa maarufu kama Dadaz bado wanaendelea na shughuli za burudani. Walianza wakiwa wadogo sana sasa wameanza kuwa mamaz. Pichani wanaonekana wakitoa burudani kwenye siku ya kubariki Kanisa la Magomeni jimbo Kuu la Dar Es Salaam. (Picha kwa hisani ya Silyvester Jakka)
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo abariki Kanisa la Magomeni
Tarehe 01 Machi 2014 Kanisa Katoliki Parokia ya Magomeni (Mashahidi wa Uganda) Jimbo Kuu la Dar Es Salaam lilibarikiwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo Askofu wa Jimbo hilo. Kanisa hilo lilibarikiwa baada ya kufanyiwa ukarabati mzito na kupata sura mpya kama inavyoonekana pichani. Nani alijenga sasa KANISA kama siyo MIMI na WEWE. Amina.(Picha zote kwa hisani ya Slyvester Jakka)
Thursday, March 27, 2014
Zoezi la kutambua mchumba
Dada wa Bi Harusi mtarajiwa (Ruthgard Mapunda) akiletwa hadharani kutambuliwa na mchumba wake |
Kabla ya kukamilisha kulipa mahali ni lazima wachumba kutambuana. Usije ukuuziwa mbuzi kwenye gunia. Ndivyo ilivyokuwa katika shrehe ya kulipa mahali wakati Richard na familia yake walipokuja kutoa mahali ya kutaka kumchumbia Bi Ruthgard Prosper Mapunda wa Yombo, Dar Es Salaam
Richard anamtambua mchumba wake Ruthgard Mapunda
Raha ilioje unapoletewa chaguo lako na kujihakikishia na mchumba kuonyesha furaha, hali ya kukubaliwa. Hongera Richard na Ruthgard kwa kuanza mchakato wa ndoa. Picha ndogo juu - Ruthgard Prosper Mapunda alipokuwa mdogo.
Mzee Prosper Mapunda
Mzee Prosper Mapunda akiwa katika pilika za madalizi ya kupokea posa ya binti yake Ruthgard Prosper Mapunda shughuli iliyofanyika nyumbani kwake Yombo tarehe 23/3/2014 Jumapili. Mama Banzi na shem Mama Happy (aliyebeba mtoto) walikuwepo kushuhudia tendo hilo. Banzi wa Moro alikuwa upande wa Mzee Mapunda.
Tuesday, March 25, 2014
Kumbukumbu ya Miaka 20 ya Marehemu Balozi Daniel Narcis Mtonga Mloka
Kaburi alimozikwa Marehemu Balozi Daniel Mloka. Mwaka huu ni miaka 20 tangu afariki na kuzikwa kijijini kwao Matombo, Morogoro. Balozi Mloka atakumbukwa kwa kuchapa kazi, ukweli na ucheshi wake. Alisimamia aliyoyaamini bila kuyumba. Mwandishi aliyeondoka na kalamu yake na kuacha vitabu vingi vya falsafa nzito kama vile 'Baharia bila Meli.'
Kaburi la Mama Mzazi-Maria Patrick Mchiro
Hapa ndipo alipozikwa Marehemu mama yangu Maria Patrick Mchiro a.k.a Binti Jamunda takribani miaka 19 iliyopita. Alizaliwa mwaka 1937 na kufariki mwaka 1995 akiwa na umri wa miaka 58. MUNGU mrehemu Mama yetu. AMINA
Sanamu ya Mt. Paulo kanisani Matombo
Kwa walio bahatika kusali ndani ya kanisa Katoliki Parokia ya Matombo wanaikumbuka sanamu hii ya Mt. Paulo somo wa Kanisa. Enzi zetu siku ya Sikukuu ya Petri na Paul ilikuwa ni maarufu Matombo. Siku hizi waumini hawajali kabisa sikukuu hii. Tukumbuke tulikotoka pengine kuna la kujifunza.
Usafiri- Morogoro-Matombo
Kutokana na kuimarishwa barabara ya Morogoro Matombo. Mabus mengi husafiri kutoka Morogoro kwenda Matombo kila siku ni safari ya saa moja tu. Hivyo bus linaweza kufanya safari ya kwenda na kurudi kwa siku moja. Pichani ni bus la kutoka Morogoro kwenda Matombo-Tawa likishusha abiria kituoni Kiswira.
Monday, March 24, 2014
Matombo sekondari yapata umeme
Hakuna sababu tena ya wanafunzi kushindwa mitihani, hakuna sababu tena ya kukosa kutumia computer.Matombo Sekondari yapata umeme. Hongera sana
Kiwanja cha mpira Matombo Sekondari
Nimewahi kucheza mpira kwenye kiwanja hiki miaka ya sabini huku nikifunga magoli muhimu kwenye goli linaloonekana au wakati mwingine kufungwa na kuokoa michomo nikiwa golini. Kiwanja hiki bado ni kilekile miaka takaribani 40 iliyopita. Tarehe 21/3/2014 nilipita hapa. Kwa mbali naziona nyumba za walimu wa Sekondari Matombo.
Njia ya Msalaba ndani ya Kanisa Katoloki Matombo
Ijumaa ya tarehe 21 Machi 2014 nimebahatika kuhudhuria ibada ya njia ya msalaba kwenye kanisa langu la Matombo, Parokia ya Mt. Petri na Paulo. Tumsifu YESU KRISTU. AMINA.
Matombo Secondary School
Zamani ilijulikana kama Matombo Middle School. Sasa ni Matombo Secondary School. Shule hii ipo kijijini kwangu Kiswira, Matombo, Morogoro.Ilijengwa na wamisionari wakatoliki mwaka 1945. Shule hii imejengwa kwa ubora wa hali ya juu. Matombo ni moja ya shule zangu za msingi nilizowahi kusoma. Dirisha la nne kutoka kulia ni darasa mojawapo nililosoma mimi. Mwezi huu nimebahatika kurudi kijijini na kutembelea shule yangu.
Nyumba ya Martin Swangoni wa Kiswira Matombo
Nyumba hii ni moja ya nyumba za zamani kijijini Kiswira, Matombo, Morogoro. Nimesoma shule ya msingi nyuma ya nyumba hii ambapo sasa ni Matombo Sekondari. Nyumba hii nimeelezwa kuwa hapa zamani kulikuwa na duka kubwa! Hivi sasa imekarabatiwa lakini bati ni lilelile.
Kitu kiko Kiswira, Matombo
Kitu kimezungukwa na mazao mbalimbali-mapapai,migomba,minazi na michungwa. Hapa ni Matombo kijiji cha Kiswira, Morogoro
Saturday, March 22, 2014
Matombo maarufu kwa mazao ya tropiki
Hapa ni Matombo, kijijini Kiswira. Mazao ya aina mbalimbali ya kitropiki yanastawi kama inavyonekana pichani. Machungwa,migomba,minazi,muhogo,mashelisheli mananasi na maembe. Ugonjwa wa mnyauo unaoathiri migomba haujaingia sehemu hii. Kuna umuhimu wa kuweka mikakati ya uzalishaji wa zao la ndizi hapa Matombo kwa ajili ya chakula na kuongeza kipato cha wananchi wa sehemu hii na kuimarisha pato la taifa. Watafiti wa Kilimo wanatakiwa kuongeza juhudi ya kutathmini sehemu hii na kuishauri serikali jinsi ya kuwaendeleza wakulima wa eneo hili wakishirikiana na wagani.
Post yangu ya kwanza nikiwa Matombo
Jana tarehe 21/03/2014 niliwasili kijijini kwangu Matombo, Morogoro ni siku ya Ijumaa. Nilipata bahati kushiriki Njia ya Msalaba ndani ya kanisa hilo nilimobatizwa, kupata Komunio ya Kwanza na Kipaimara. Waumini wachche waliohudhuria wengi walikuwa ni wanawake kuliko wanaume. Hali hii inafanana sana na Parokia yangu ya Vikindu Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Wanawake wengi wanatenga muda wao kushiriki ibada sisi wanaume tuko 'busy'. Namshukuru Mungu hii ni post yangu ya kwanza nikiwa Matombo baada ya miaka mingi sehemu hii ya Tanzania sasa imepata umeme tangu mwaka 2013 mambo haya sasa yanawezekana.
Thursday, March 20, 2014
Zawadi za Kitchen Party
Zawadi za Kitchen Party ya Mwajuma Pembe wa Kisemvule. Jamvi, ungo, mwavuli,ndoo,glassess,sahani,sufuria,vikombe.......... Mwanamke amekamilika
Subscribe to:
Posts (Atom)