Tuesday, April 29, 2014
DAR Express mkombozi wa usafiri kaskazini
Kampuni ya mabus ya Dar Express bado yanaoongoza kwa kutoa huduma bora na ya uhakika kwa abiria waendao mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Pichani bus likiwa Korogwe huku abiria wakipata chochote kile cha kula.
Thursday, April 24, 2014
Matukio ya Ijumaa Kuu Parokia ya Vikindu 2014
Baadhi ya vituo vya Njia ya Msalaba vilivyopitiwa na waumini kutoka Jumuiya Ndondogo za Kigango Mama cha Parokia ya Vikindu kutoka Kisemvule hadi Kanisani.
Askofu Mdoe akimkabidhi mshumaa Paroko mpya wa Vikindu
Siku ya Alhamisi Kuu Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam alimkabidhi mshumaa Paroko mpya wa Parokia ya Vikindu Fr. Stephen
Askofu Titus Mdoe akitoa mahubiri Kanisani Vikindu
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam Askofu Titus Mdoe akitoa homilia yake siku ya Alhamisi Kuu Parokiani Vikindu
Makamu Mwenyekiti Parokia ya Vikindu aoshwa mguu
Siku ya Alhamisi Kuu 17/04/2014 Mhashamu Baba Askofu Titus Mdoe wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam aliwaosha miguu baadhi ya waamini wa Parokia ya Vikindu akiwemo Bw. Linus Kihawa, Makamu wa Mwenyekiti Halmashauri ya Walei Parokia ya Vikindu (aliyenyoosha mguu).
Wednesday, April 23, 2014
Kwaya ya Mt. Petro yaanzishwa Vikindu
Parokia ya Mt. Vinsenti wa Paulo Vikindu inazidi kukua. Hivi sasa Kwaya mpya ya Mt. Petro imeanzishwa Parokiani na kuanza kutoa huduma parokiani. Kutakuwa na mchuano mkali kati ya Kwaya Mama ya Mt. Vinsenti na hii ambayo inaundwa na vijana wengi!
Tuesday, April 22, 2014
Kumbukumbu ya mateso ya Bw. Yesu Kristo
Kumbukumbu ya Injili ya mateso ya Bw. Yesu Kristo siku ya Jumapili ya Matawi , Parokiani Vikindu, Jimbo Kuu la Dar Es Salaam
Athari ya mafuriko Dar Es Salaam
Hii ndiyo moja ya athari ya mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar Es Salaam sehemu za Mbagala
Wananchi wakipita juu ya daraja la mto Mzinga
Mvua zinazonyesha jijini Dar Es Salaam, zimeathiri miundombinu ya barabara nyingi likiwemo daraja la mto Mzinga baada ya sehemu kuchimbika na hivyo kusababisha magari kushindwa kupita. Pichani wananchi wakipita juu ya daraja hilo baada ya TANROADS kurekebisha sehemu zilizochimbika.
Kizaazaa cha mvua kubwa Dar
Haijawahi kutokea kwa miaka mingi. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye bonde la mto Mzinga-Kongowe, Dar Es Salaam
Athari za mvua Dar Es Salaam
Maporomoko ya Udongo, Mbagala. Nyumba hii ipo kabisa na Kiwanda cha zamani cha TANITA. Kanda ya barabara ya Kilwa pale mlimani Kokoto. Mvua zikiendelea kunyesha. Nyumba hii itadondoka.
Mvua mvua-Pwani
Mvua kubwa inaendelea kunyesha ukanda wa Pwani hasa mikoa ya Dar Es Salaam na Pwani. Majumba yetu yalifurika maji, vyombo vyote vya kutunzia maji vilijaa.
Bustani ya Mwembeyanga
Hii ni bustani ya Mwembeyanga inayomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Bustani hii ina miti ya kutosha inayotoa kivuli na kufanya mahali pazuri pa kumpuzika, kufanya mazoezi. Lakini kuna baadhi ya wananchi huitumia bustani hii kwa matumizi mabaya kama vile uvutaji bangi. Isitoshe bustani hii inatakiwa kuboreshwa zaidi kwa kuongeza miundo mbinu mingine kama vile viwanja vya kucheza watoto wadogo, viti vya kupumzikia na ikiwezekana ndani ya bustani hii kukawa na sehemu ambapo magazeti yanapatikana ili watu waweze kujisomea.
Kaghorofa kazuri
Unaweza kujenga ghorofa hasa kama eneo lako ni dogo. Usiogope, ni kuwa na plan nzuri tu. Gorofa hii iko Tandika karibu kabisa na Chuo cha Bandari. Zamani eneo hilo kulikwa na nyumba za NHC ndogo. Angalia kaghorofa kalivyopendeza!
Mitaro imeziba Tandika
Angalia jinsi maji yasivyotembea katika mitaro iliyopo Tandika. Angalia jinsi kiroba cha uchafu kilichopo pembeni. Hii ina maana kuwa taka hizo zinaweza kumwagika ndani ya mtaro na hivyo kuufanya uzibe. Hivi kuna ugumu gani wa kusafisha mitaro ya maji machafu?
Nimeipenda bustani ya nyumba hii
Kila nikipita barabara hii iliyopo Tandika navutiwa na bustani ya majani inayotunzwa vizuri kando ya nyumba hii. Nyumba hii haiko Masaki iko Tandika lakini bustani yake inavutia. Cha ajabu jirani zake wameshindwa kuiga. Si vibaya kuiga jambo zuri. Swali ninalojiuliza, je viongozi wa mtaa huu hawaioni bustani hii na kuwashawishi wenye nyumba kando ya barabara hii kutengeneza bustani ndogo kama hii. Itapendeza na itavutia. Tuwe wabunifu kwenye makazi yetu. Si dhani kuwa kuitunza bustani hii ni gharama kubwa.
Huduma ya Maji kwa kutumia nguvu ya jua
Baadhi ya Vijiji vya wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani vimeanza kunufaika na huduma ya maji safi kwa kutumia visima vinavoendeshwa kwa nguvu ya jua (solar energy). Moja ya kijiji hicho ni cha Kisemvule.
Usafiri jijini Dar Es Salaam
Hali hii ya usafiri ni ya kawaida kabisa jijini Dar Es Salaam. Ni msongamano wa magari, baisskeli na pikipiki. Hivi kweli tumeshindwa kuwa na utaratibu wa kurahisisha usafiri jijini? Hivi askari wa usalama barabarani wanafanya nini? Hivi SUMATRA kazi yake nini?
Usafiri na usafirshaji Dar Es Salaam
Malori makubwa na usafiri wa pikipiki jijini Dar Es Salaam. Pasipo na utaratibu mzuri ajali zitazidi kuongezeka
Tuesday, April 8, 2014
Viongozi katika dua
Ninaamini kuwa kiongozi bora ni yule anayemuamini Mungu na ni mtu wa sala.. Pichani bila kujali nyadhifa zao Viongozi wetu wa Taifa wakiomba dua wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume huku wakiwa na vitabu vya sala. Kwa haraka haraka naweza kuwatambua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania -Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr. Mohamed Shein, Makamu wa Rais Dr. Mohamed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Haasan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Amani Abeid Karume, na Makamu wa Pili wa Serikali ya Zanzibar Balozi Seif Iddi Ali (Picha kwa hisani ya Gazeti la Daily News 8/4/2014)
Tanzania 'Bingwa wa Kandanda wa Dunia' 2014
Bingwa ni Bingwa tu. Ndiyo, Tanzania tumekuwa Bingwa wa Kandanda wa Dunia kwa Watoto wa Mitaani mwaka 2014. Ni gazeti la Daily News pekee lililoipa umuhimu wa kwanza habari hii katika ukurasa wake wa michezo toleo la tarehe 8/4/2014. Hii ni habari kubwa katika michezo. Nashangaa kuona hata magazeti ya michezo hayakutoa kipaumbele kwa habari hii kwenye magazeti yao. Mengi yanaandaika habari za Manchester United, Barcelona, Chelsea, Liverpool! Zinatuhusu nini Watanzania. Watoto wa Mitaani wametuletea sifa Watanzania. Waliondoka wakiwa na maandalizi hafifu. Hawakukata tamaa. Safari tu kwao ni motisha. Kutoka mtoto wa mitaani hadi kupanda ndege kuna tofauti kubwa sana. Kutoka mitaani hadi kwenda kuishi hoteli zenye hadhi ya Kimataifa ni hadhi kubwa sana. Mimi nimefurahishwa sana na matokeo haya. Kijana pichani anayepeperusha bendera ya Taifa hata jina halijulikani anaonekana kuwa na furaha ya pekee. Iko siku atakuja kuwa maarufu. Tunasoma kuwa wachezaji wengi kutoka Amerika ya Kusini wametoka kwenye familia duni na kuwa maarufu katika Soka Duniani. Hawa huwa na bidii sana wanapopata kitu cha kushika. Hivi bado hatujafumbuka macho na kuweza kuanza kuwekeza huko mitaani. Kuwa mtoto wa mtaani si dhambi, yote ni maisha. HONGERA TANZANIA KWA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA. (Picha kwa hisani ya gazeti la Daily News 8/4/2014)
Friday, April 4, 2014
Ndege mpya ya ATCL yaongeza ufanisi
Ndege mpya ya kukodi ya Shirka la Ndege la Taifa (ATCL) aina CRJ-200 yenye uwezo wa kubeba abiria 50 imeweza kuongeza uwezo wa Shirika wa kusafirisha abiria kwa asilimia 57 hayo yameelezwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Captain Milton Lazaro. Aidha Lazaro ametangaza 'offer' maalumu wakati wa Pasaka kwa abiria watakaosafiri kwa anga kwa shirka lake Dar-Mtwara-Dar kuwa itakuwa ni Tshs 250,000/=. (Picha kwa hisani ya gazeti la DailyNews 4/4/2014 - Tafsiri ya Kiswahili ya habari -Banzi wa Moro)
Msongamano wa magari barabara za Mandela na Kilimo jijini Dar
Hapa ni makutano ya barabara ya Kilimo na Nelson Mandela karibu kabisa na yalipo makao makuu ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wilayani Temeke eneo la Veterinary. Kuanzia saa nane hadi 12.30 jioni kila siku kwenye makutano haya mpaka mpale TAZARA kunakuwa na msongamano wa magari. Hivi hakuna utaratibu wa kuyafanya magari yanayotoka Bandari kutumia barabara ya Mandela kwa masaa maalumu? Je ni nani aliyempa Mamlaka mmiliki wa Kampuni ya Magari ya Dandho kuweka malori yake kwenye barabara ya Kilimo na kuwafanya Wafanyakazi wa Kilimo kukosa amani katika kufanya kazi wakibugudhiwa na kelele za magari hayo na msongamano?
Nguvu ya Jua yasukuma maji Kisemvule-Mkuranga
Asilimia kubwa ya nchi yetu ya Tanzania inapata mwanga wa jua kwa muda mrefu kwa siku. Mwanga huu ukitumiwa vizuri kwa kuzingatia teknolojia zilizopo zinazoendeshwa kwa nguvu ya juu utasaidia sana kuboresha maendeleo ya watu wetu vijijini. Nguvu ya jua (solar power) inaweza kusukuma pump za maji, kutoa umeme kwa matumizi ya nyumbani na hata viwanda vidogovidogo. Miaka ya hivi karibuni Shirika lisilo la Kiserikali la African Reflections kutoka Marekani limekuwa likichimba visima vya maji katika mkoa wa Pwani hasa wilaya ya Mkuranga. Pichani mtaalamu akifunga panel ya solar kijijini Kisemvule itakayotumika kutoa nguvu ya kusukuma pump ya maji ya kisima. Kinachotakiwa ni utunzaji wa miundo mbinu hiyo. Kwa kutumia solar power wananchi watapata huduma ya maji wakati wowote. Hii itapunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya kulipia bill ya umeme wa TANESCO.
Subscribe to:
Posts (Atom)