Monday, October 27, 2014
Ujana raha tupu!
Unamuona huyo mwenye fulana ya kijani. Kijana anapenda muziki huyo acha tu. Alitupa burudani ya aina yake jana kwenye ukumbi wa Maaskofu-Kurasini jijini Dar. Enzi zangu miaka ya 80s nilikuwa kama yeye. W-end niko Silversands Hotel na kaka yangu Lawrence Mkude nikisakata Disco la nguvu. Ah nikwambie nini ujana raha tupu!
Ulifika wakati kwa Bw. Remmy kupeleka keki ukweni
Mara nyingi kwenye sherehe za kuwapongeza maharusi kuna tendo la kupeleka keki kwa wakwe. Hii maana yake nini hasa. Kwa ufahamu wangu ni ishara ya ukarimu na kuwa tayari kujitoa na hasa chakula. Wakwe wanahitaji kutunzwa na kuwakarimu. Tuwakarimu wakwe na ndugu na watu wengine. Pichani Bw. Remmy akikabidhi keki ukweni siku ya sherehe ya harusi yake - 26/10/2014
Madada wasindikiza harusi kutoka Mwandege
Kikosi hiki cha madada wasindikiza harusi kutoka Mwandege, Mkuranga. Mama mwanakamati wa maandalizi ya sherehe ya harusi ya Remmy Shayo alijitolea kukileta kikundi hiki ili kipendezeshe mapokezi ya harusi hiyo iliyofanyika jana (26/10/2014). Kwa kweli walikonga nyoyo za waalikwa. Walicheza kwa furaha na walikuwa very simple! Kweli Mungu yu Mwema.
Harusi ya Remmy ilivyofana kwenye Ukumbi wa Maaskofu Kurasini-Dar
Bw & Bibi Remmy Shayo wa Vikindu- Dar Es Salaam jana tarehe 26/10/2014 walifunga ndoa kwenye Kanisa la TAG Vikindu na baadaye tafrija ya Nguvu ilifanyika ndani ya Ukumbi wa Maaskofu Kurasini. Hakukuwa na kinywaji chochote cha kilevi lakini watu walifurahi na kuserebuka kama unavyowaona pichani. Banzi wa Moro alikuwa ndani ya ukumbi.
Saturday, October 25, 2014
Misa ya Mavuno Jumuiya ya Mt. Vincent Parokia ya Vikindu - 25/10/2014
Leo 25/10/2014 asubuhi, Padri Jinu wa Parokia ya Vikindu aliendesha ibada ya misa takatifu ya mavuno iliyodhinishwa kwenye Jumuiya ya Mt. Vincent. Kwenye mahubiri yake alisema kuwa, mara nyingi binadamu tunamsahau MUNGU. Tunapofanikiwa katika maisha yetu tunafikiri ni kwa sababu ya akili zetu au juhudi zetu binafsi. MUNGU TUNAMUWEKA KANDO. Tujiulize katika maisha yetu, hivi hatuna chochote cha kumwambia MUNGU ASANTE? Na hii ndiyo maana ya MAVUNO ni kutoa SHUKRANI KWA MUNGU. Tumsifu YESU KRISTU.
Subscribe to:
Posts (Atom)