Friday, January 30, 2015

Chambezi-Kituo kidogo cha Utafiti wa Kilimo

Hiki ni kituo kidogo cha Utafiti wa Kilimo  Chambezi wilayani Bagamoyo kinachosimamiwa na Kituo cha Utafiti Mikocheni kilichopo Dar Es Salaam. Kituo hiki kilianzishwa wakazi wa Mradi wa Taifa wa Kuendeleza  Zao la Mnazi kwa ufadhili wa Ujerumani. Kituo hiki kwa sasa hutumika zaidi kwa utafiti wa Muhogo ingawa tafiti za mazao mengine kama vile korosho na minazi unafanyika kwa kiasi kidogo. Kituo hiki kina eneo kubwa kwa shughuli za utafiti wa kilimo endapo kiyawezeshwa kupata raslimali za kutosha  kinaweza kuvutia shughuli nyingi za utafiti wa mazao  kanda ya mashariki.

4 comments:

Ebenezer Farm said...

habari nashukuru kwa blog yako ya kuelimisha. Mimi ni mkulima Bagamoyo Mazizi, Msata mwaka huu ninataka kulima miembe ya kisasa Alphonso, Apple au Kent je kituo hiki bado kina zalisha mbegu za miembe. Nilipita Kiromo kwa wae wanaouza barabarani sio mbegu za ksasa. Nafahamu kitalu cha Amagro Gerezan ila ningependa na itakuwa rahisi nikichukulia hapo kwenu. Naomba contacts zenu au wakulima wanaouza mbegu hizo

Innocent John Banzi said...

Ebnezer Farm. Asante kwa kuwa mdau wa blog ya banzi wa moro. Kwa bahati mbaya ndiyo leo ninaiona comment yako. Mimi nafanya kazi Makao Makuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Idara ya Utafiti na Maendeleo. Napenda kukupatia contact ya mtaalamu ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti Mikocheni, Dar anaweza kukusaidia kuhusu suala la miche na ushauri mwingine wa kitaalamu. Huyu ni Dr. Joseph Ndunguru - jndunguru2003@yahoo.co.uk simu ni 0764554458. Karibu.

Unknown said...

Heri ya mwaka mpya. Nafuatilia historia ya wajerumani hapa Bagamoyo na mradi waliyokua wanafanya enzi zao. Je kuna documentation yote mnisaidie. Marie binti Shaba mdau wa urithi wa utamaduni Bagamoyo.pamoja na email nina whatsup 0762001949

Unknown said...

Nahitaji miche ya minazi mbegu fupi dwarf yakijani namba yangu ya whatsapp ni +255655138770