Nilipokuwa mdogo nilivutiwa sana na Brass Band. Shule ya Msingi Matombo ilkuwa na vifaa vizuri sana vya band kama unavyoviona kwenye hiyo Brass Band ya Polisi. Ingawa nilikuwa mdogo na mfupi lakini nilitamani kupiga ngoma ndogo,kubwa na pia kuwa Bandmaster (huyo aliyeshika gongo). Hii ndiyo moja ya sababu iliyonifanya kuanza shule mapema. Na kweli nilipoingia shule nikiwa darasa la nne tu niliweza kuwa mpiga ngoma ndogo, nikiwa darasa la sita ngoma kubwa (huku nikibebewa) na hatimaye Band master (ingawa gongo lilikuwa zito na wakati mwingine kushindwa kuzungusha kwa manjonjo).
Friday, November 27, 2015
DC Josephine wa Shinyanga akuta dawa kibao kituo cha Afya Kambarage
Katika ziara ya ghafla aliyoifanya DC Josephine Matiro kwenye kituo cha afya cha Kambarage. Yeye pamoja na Katibu Tawala wa Wialya (Pichani) walipigwa butwaa kukuta dawa zimejaa kibao huku wagonjwa wakiambiwa hakuna dawa hivyo wajinunulie wenyewe.chukua ni kumsimamisha kazi mmoja wa wauguzi wa zahanati hiyo (Picha kwa hisani ya Mahunde blog)
Hii ndiyo Lyamungo Guest House-Moro
Moja ya Guest Houses nzuri zinazopatikana mjini Morogoro- Lyamungo Guest House. Siipigii debe, lakini kwa kweli Guest hii ni nzuri, safi na usalama wa hali ya juu. Kinachofurahisha zaidi ni uchapa kazi wa watoa huduma wa nyumba hii ya wageni wakiongozwa na Meneja wao Bw. Malamsha. Bei ya chumba kwa siku ni Tshs 25,000/= inajitegemea na chenye kiyoyozi. Ipo karibu kabisa na "msikiti wa Mahita"
Friday, November 20, 2015
Wengi hatupendi kuandika na wala kusoma
Ukitaka kuwa na ufahamu wa kutosha katika maeneo mengi ni lazima ujifunze kusoma na ikiwezekana na kuandika pia. Ukitaka kuwa mtafiti mahiri lazima usome na kuandika. Pichani ni baadhi ya taarifa mbalimbali na Thesis za MSc na PhD zinazotunzwa kwenye maktaba ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika-Idara ya Utafiti na Maendeleo.
Maembe yanavyooza kiwanda cha Azam
Hivi ndivyo inavyoonekana kwa moja ya lori lililobeba shehena ya maembe nje ya kiwanda cha Azam (Bakharesa Group) likingoja zamu ya kuuza maembe hayo. Maembe mengi yamekuwa yakioza nje ya kiwanda hicho kwa sababu ya mchakato wa muda mrefu ya kuyanunua kiwandani. Aidha usafirishaji wa maembe hayo ni wa kiholela sana. Ona jinsi yalivyojazwa kwenye viroba na kufungwa na kamba. Kwa vyovyote uwezekano wa kuharibika ni mkubwa sana.Wasafirishaji wanatakiwa kuelimishwa kuhusu hili.
Tuesday, November 17, 2015
Wednesday, November 4, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)