Wednesday, June 22, 2011

ASA-Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Tayari Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) wameshaandaa. Mkataba wa Huduma kwa Mteja. Ndani ya Mkataba imewekwa bayana huduma zitolewazo na Wakala hii na jinsi huduma anavyopaswa kuhudumiwa. Lengo ni kutoa huduma za mbegu zenye ubora wa hali ya juu ili kuweza kuongeza tija katika kilimo.

Dakawa-Kituo cha usambazaji wa Teknolojia


Kituo kipya cha usambazaji wa teknolojia za kilimo kimejengwa Dakawa-Morogoro kwa msaada wa Serikali ya China kimefunguliwa mwaka huu na Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete

SARO- Nyumbani kwake Cholima-Dakawa


Moja ya vituo vya Utafiti wa Kilimo kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Kituo hiki kilizinduliwa mwaka 1985 na Rais wa awamu ya Kwanza Mhe. Julius K.Nyerere. Kimejengwa kwa ushirikiano na wa Jamhuri ya Korea Kaskazini. Shughuli zake kuu ni utafiti wa mpunga. Aina ya mbegu ya mpunga SARO nyumbani kwake ni hapa.

Ni madaraja



Ukisafiri kwa kutumia gari kutoka Mikumi kwenda Ifakara kitu kimoja ambacho ni dhahiri kukiona ni madaraja. Mojawapo ni hilo hapo juu la Mikumi ambapo reli inapita juu na hili la kulia la Ruaha.

Friday, June 17, 2011

Chini ya Daraja la Umoja

Ukitembelea kijiji cha Mtamba swala-Nanyumbu na kuliona daraja la Msumbiji utashangaa sana.Pichani- Mshana,Kadeng'uka na Banzi chiniya daraja la Umoja.

Mgahawa wa Kituo cha mabus-Masasi

Huu ni mgahawa maarufu Masasi.Hapa nilipata chapati moja,na supu ya kuku wa kienyeji!

Zawadi kutoka Msumbiji

Kweli imetengezwa Msumbiji!

Nangurukuru

Hapa ndipo panaitwa Nangurukuru ni maarufu kwasamakiwakukaanga. Ni kituo maarufu sana wakati unaelekea Lindi kupitia barabara ya Kilwa. Kiko njia panda ya kwenda Kilwa Masoko. Angalizo usikurupukekununua samaki wakukaanga hovyo hovyo hapa na kubugia. Mimi yalinikuta!

Nyama choma na supu ya mbuzi ok!


Endapo utafiti wa kupata aina bora za mbuzi utafanikiwa,tutaongeza uzalishaji wa mbuzi na kufaidi matunda yake kama hivi.

Mbuzi wa utafiti - Mnima


Hawa ni mbuzi wa utafiti waliopo kwenye kituo cha majaribio ya utafiti kilichopo Mnima huko Newala.Hapa ndipo panapotarajiwa kutoa aina mpya ya mbuzi kwa miaka ijayo kwani ili kupata aina ya mbuzi kwa kuzingatia sifa zinazotakiwa utafiti huchukua muda mrefu.Ili kufikia lengo lazima uwekezaji katika utafiti uongezeke zaidi kwa kuongeza wataalamu na vitendea kazi.

Unapoingia mjini Lindi

Mara unapoingia mjini Lindi ukitokea Dar unapata mandhari hii.Kwambali upande wa kushoto ni bahari ya Hindi.

Tunasali na kutafakari

Ndivyo tufanyavyo Jumuiya ya Mt.Joseph- Parokia ya Vikindu.Kila Jumamosi jioni tunakutana kwenye nyumba ya mwana jumuiya mmoja tunasali na kutafakari neno la Mungu kwa pamoja. Jumuiya zinatuweka karibu zaidi.Tunajifunza mengi na kusaidiana.

'Kocha'akiwakambini Nyegezi Mwanza

Kocha anapokuwa kambini na wachezaji na huku kukiwa na mechi ngumu kesho jioni.Kwa hali hii hakuna mategemeo ya ushindi.

Kise Kids wanasubiri zawadi

'Kise Kids Soccer Club' ni Klabu ya soka ya vijana iliyopo kijijini Kisemvule,Vikindu,wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.Mapema mwaka huu iliweza kushika nafasi ya tatu kwenye mashindano yaliyoandaliwa na kijiji cha Kisemvule.Pichani wachezaji na washabiki wakisubiri zawadi ya mshindi wa tatu (walipata mpira mmoja).

Daraja la Umoja - Msumbiji naTanzania

Hili ni daraja la kujivunia kati ya nchi mbili maskini za dunia ya tatu- Tanzania na Msumbiji.Limejengwa kwa fedha zetu wenyewe kwa kutumia wa wataalamu kutoka China.Pichani Omary Shomari akiwa kwenye daraja hilo alipotembelea kijiji cha Mtambaswala mpakani mwa Tanzania na Msumbiji,wilayani Nanyumbu.

Tunakwenda kusali kwenyeJumuiya

Baba na mwana wanaelekea kwenyeJumuiya huko Vikindu Kisemvule.Jumuiya zetu ziko mbalimbali sana kutoka nyumba hadi nyumba.

Na hii ndiyo familia yangu

Maisha poa kabisa!

Mamaa ananipa pongezi

Mamaa alinipa pongezi ya Birthday niliporudi nyumbani!

Tuesday, June 7, 2011

HA! LEO 'BIRTH DAY' YANGU


Leo ni 'Birth day yangu'. Na leo natimiza post ya 1000 katika blog yangu. Namshukuru Mungu kwa kunipa uhai hadi kufikia siku ya leo Jumanne 7/6/2011. Nimefurahi pia kuingiza post ya elfu moja tangu kuanza kwa Blog hii. Mwezi huu ni mwezi wa mafanikio kwangu kwa mara ya kwanza kwa mwezi mmoja nimeingiza zaidi zaidi ya post 60!

Monday, June 6, 2011

Hili ndilo daraja la Mkapa

Daraja hili ni refu sana na huwezi kulinganisha na daraja la mto Mfizigo lilipo Matombo, Morogoro vijijini.Ni kazi nzuri ya Rais wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa.Ndivyo anavyothibitisha Mtafiti wa Kilimo Bw. Laurent Kadeng'uka alipotembelea mikoa ya Mtwara na Lindi hivi karibuni.