Thursday, June 14, 2012

Ibada fupi langoni

Mapadri waliendesha ibada fupi na kuingiza mwili Kanisani

Jeneza la Dr. P.Mluge langoni mwa Kanisa

Misa ya kumuombea marehemu Dr. Mluge kabla ya safari kuelekea nyumbani Matombo, Morogoro ilifanyika kwenye kanisa Katoliki la Mbezi Beach (Mt. Gasper)

Tumempoteza Dr. Gregory Paul Constanci Mluge

Tarehe 9/6/2012 itabakia kuwa siku ya majonzi makubwa baada ya kuipoteza nguzo ya familia yetu Dr. Gregory Paul Constanci Mluge (Pichani kulia akiwa na mkewe wakati wa uhai wake)

Tuesday, June 5, 2012

Wamepokea Sakramenti ya NDOA

Takribani ni mwaka mmoja sasa tangu Bw na Bi Cleophas wapokee Sakaramenti ya Ndoa Parokiani Vikindu, Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Vijana wengi wanaogopa kufunga ndoa kwa kutaka makuu. Nilishuhudia ndoa hii isiyokuwa na makeke wala vitimbi. Tulikula, tulikunywa na kucheza.Wanandoa wanaendelea na maisha yao bila mfarakano. Hongereni sana.

Kituo cha Mabasi Kivukoni-DAR

Unapokuwa kivukoni au 'FERRY' Dar pale kwenye kituo cha mabasi ni vurugu tu. Hujui bus linaloondoka au linaloingia. Ukiwa mgeni utashangaa sana

Watoto wanapendana

Tukiwafundisha mapendo watapendana

Watoto na Ibada

Kila unapopata fursa ya kuhudhuria ibada ni vizuri kwenda na watoto

Majani ya Kaskasi

Kwenye maonesho ya NaneNane (Siku ya Wakulima)mwaka jana (2011) wakulima wa kutoka Kibungo JUU wilaya ya Morogoro Vijijini kwenye banda lao walionyesha matumizi bora ya ardhi.Moja ya teknolojia waliyoionyesha inayotumika kuhifadhi ardhi ni upandaji wa mmea unaoitwa kaskasi au kwa lugha ya Kiluguru 'usoti' (pichani) kuzuia mmomonyoko wa ardhi milimani. Licha ya kuhifadhi ardhi, kaskasi hutumika kuezeka nyumba.

Mambo ya Teknolojia

'LCD Projector' ni chombo cha kisasa cha elektroniki kinachotumika kurushia mada. Pichani kulia Mkurugenzi Msaidizi Utafiti wa Mimea kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Dr. Hussein Mansoor akifurahia jambo.

Makubwa!

Anauliza proforma invoice ya gari! (Picha kwa hisani ya cartoonist NOAH YONGOLO).

Monday, June 4, 2012

Traffic Police mmemuona huyu?

Jijini Dar usafiri wakati wa asubuhi ni mgumu sana. Banzi wa Moro imeinyaka hii leo asubuhi dadala la kutoka Bagala Rangi 3 kwenda Mwenge. Traffic Police mpo?

Ni hatari kwa watoto hawa

Hii inahatarisha maisha.Wanafunzi wengi na vijana hupenda kudandia magari ili wapate kitu kinachoitwa 'lift' lakini gharama yake mara nyingi ni kuhatarisha maisha. Angalia picha hizi ambazo zimenyakwa na Banzi wa Moro kuanzia kituo cha Kongowe hadi Mbagala Rangi 3 jijini DAR ES SALAAMNdani ya lori wanajiandaa kushuka chini Wanapanda

Matokeo ya kutomuaga mkeo

Baadhi ya wanaume wanatatabia yakutoka majumbani kwa bila kuwaaga wake zao. Tabia hii huwachukiza sana wanawake, hasira wanazokuwa nazo kwa wale wasiokuwa na busara hufanyiwa alichofanyiwa afande 'kulakula' (Picha kwa hisani ya Cartoonist NOAH YONGOLO)

Friday, June 1, 2012

Wanamwita 'Mwabeshi'

Huyu anaitwa Shabani. Lakini hapa kijijini kwetu Kisemvule ni maarufu sana kwa jina la 'Mwabeshi' likiwa na maana ni mtu kutoka Ethiopia! Kwa maelezo yake mwenyewe ni kwamba, jina hilo amelipata hapo Kisemvule kwa kuwa alikuwa anafanya kazi kwa mtu aliyefananishwa na waethiopia lakini kumbe alikuwa ni mchangayiko wa damu ya kihindi na watu kutoka Tabora. Shabani kazi yake ni biashara ndogondogo hasa matunda kwa kuzingatia msimu kuna wakati anauza embe, kuna wakati mwingine machungwa. Hapa alikuwa anauza mahindi ya kuchoma. Huyo ndiye Shabani 'Mwabeshi' ameoa na ana watoto watatu

Nyumba hadi nyumba

Ndivyo inavyofanya kazi Jumuiya Ndogondogo za Kikristu. Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mgaya wa Soweto-Vikindu. Jumuiya Ndogondogo zinaimarisha upendo, kutambuana na pia hutumika kulieneza Neno la Mungu.Jumuiya Ndogondogo ikitumiwa vizuri huleta maendeleo.

Shemeji zangu

Wote wawili ni akina Binti Pembe, hawa ni shemeji zangu msiulize maswali mengi - period!

Alama za kiwanja

Unaponunua viwanja vizsivyopimwa ni vizuri kuweka alama za kudumu na zinazoeleweka ili kuepusha mgangano wa mipaka ya viwanja hapo baadaye

Na hii ndiyo misemo ya Waluguru

1. 'Bita ako si miyage' - Si vizuri kuacha mtu akafanya kitu kivyake vyake 2. 'Chikwili ng'awingagwa na Seko'- Huwezi kumfukuza mnyama anayeitwa 'Chikwili' huku ukiwa unacheka 3. 'Chimbulumbulu kokwila mti gwagumanyile'- Mnyama anayeitwa Chimbulumbulu hupanda mti anaoufahamu. Tafakari kuhusu semi hizi za Kiluguru!

Miundo Mbinu ya Umwagiliaji

Kuendesha kilimo cha umwagiliaji inahitaji miundo mbinu ya uhakika
Banio la Umwagiliaji liloloko mto wa Ruaha- Ruaha Mbuyuni, Kilolo.
Banio la umwagiliaji maji kijiji cha Itimba
Mfereji wa umwagiliaji unaotunzwa vizuri
Baada ya kuvuna mahindi, shamba limepandwa maharage (Kijijini Itimba, Utengule-Mbeya vijijini). Hii inawezekana kupitia kilimo cha umwagiliaji.

Hapa ni Umalila-Mbeya

Isangati Agricultural Development Organization (IADO) kijijini Santilya, Umalila, Mbeya Vijijini. AIDO ni Shirika lisilo la Kiserikali (NGO) linalofanya kazi katika wilaya ya Mbeya Vijijini. AIDO wamewezeshwa na ASDP kupitia DADPs katika kuleta mageuzi ya kilimo wilayani Mbeya. Baadhi ya Miradi ya Kilimo inayosimamiwa na IADO ni:- Upandaji wa Miche Bora ya Kahawa, Ufugaji wa Ng'ombe wa Maziwa, Ufugaji bora wa Nguruwe, Uboreshaji wa Kuku wa Asili, Ufugaji wa samaki. Aidha IADO hutoa mafunzo ya Utawala Bora yanayowawezesha wanavijiji kufuatilia matumizi ya fedha za umma ngazi ya kijiji.
Uboreshaji wa kuku wa asili
Nje ya Ofisi ya IADO
Tunapata taarifa ya IADO kutoka kwa uongozi wa shirika.
Ukaguzi wa banda la machinjio kijijini Santilya, Mbeya vijijini.