Saturday, March 24, 2012

Ndani ya nyumba ya asili ya Kiswazi

Nyumba hii haina madirisha lakini haivuji wala haingizi maji. Ulinzi ni wa kutosha wa ndani anamuona wa nje na wa nje hamuoni wa ndani. Huezekwa wa wanawake majukumu ya kazi ya kijinsia, Afrika tumeanza zamani!

Kwenye Utamaduni wa Waswazi


Nikiwa hapa Swaziland nilibahatika kutembelea kijiji cha utamaduni wa Waswazi kijulikanacho kwa jina la Mantenga cultural village. Moja ya vitu nilivyoshirikishwa ni kucheza ngoma ya asili ya kiswati (pichani)

Chakula sh 1500/=


Watanzania tumebahatika kuwa na vyakula vya ainA mbalimbali na vizuri. Ona chakula hiki gharama yake ni sh 1500/= tu. Picha kutoka Mjengwa Blog

Friday, March 23, 2012

The Mananga Experience

This is Mananga Centre of Regional Integration and Development Management located at Ezulwini,Swaziland. The location, staff,environment, training and the international look it has, certainly you need to taste Mananga Experience!


Bwawa la Maguga-Swaziland


Waswazi wanajivunia bwawa la Maguga lilojengwa katika mto wa Komati unaounganisha Swaziland (40%) na Afrika ya kusini (60%). Bwawa hili linamanufaa kadhaa kwa Waswazi.
1)Hutoa umeme 19.5MW
2)Chanzo kizuri cha upatikanaji wa kitoweo-Samaki
3)Maji kwa matumizi ya nyumbani na viwandani
4)Umwagiliaji wa mashamba
5)Kivutio cha utalii.

Thursday, March 22, 2012

Plan before you negotiate

Some planning tips
1)What do I want
2)What do they want?
3)What will/can I trade ?
4)Explore all the available options of the trade
5)Explore long and short term implications of each option for all parties involved
6)Set Objectives in terms of acceptable limits and that you have a realistic chance of achieving
7)Visualize possible gains, not losses
8)Be aware that the opposition might have a hidden agenda
9)Identify your supporting arguments that justify your objectives
10)What strengths and weaknesses do you take
11)What will be your opening gambit and how will you present it
12)How much time is there to negotiate (Time scale)
13)What will be your opening position, your fall back position and your final fall back position beyond which you will refuse to do business.


Hivi kweli huwa tunajiandaa na haya kabla hatujaanza 'negotiations' au tunakimbilia kuvaa suti na kufunga tai? Basi kama hatufanyi tujiandae.

If you want to be an effective negotioator


1)PLAN
2)PROPOSE
3)DEBATE
4)BARGAIN

Hivi tunaowapeleka kwenye 'negotiations' huwa wanatambua nini cha kufanya?

Procrastination

Nothing is so fatiguing as the general hanging on of uncompleted task- William James.

Kwa kweli tabia hii ya kutokamilisha kazi kwa wakati uliowekwa ni kilema kwa watu wengi hata Banzi wa Moro anayo ndiyo hiyo inayoitwa - PROCRASTINATION. Unapewa kazi unasema nitafanya kesho, kesho, kesho hatimaye inachelewa na matokeo yake ni mabaya si kazini hata nyumbani kwako kama umeamua kufanya kitu anza sasa muda haukungoji. Utafiti uliokwishafanyika unaonyesha kuwa 20% ya Wamerekani wanatabia hiisisi je? Pengine 80!

who is a good leader

Is the one who uses all leadership styles depending on the situation/condition, i.e. autocratic, democratic and delegative.

Delegative type of leadership

The leader allows the employees to make the decisions. However the leader is still responsible for the decisions that are made.

USED: When employees are able to analyse the situation and determine what needs to be done and how to do it.

Autocratic leadership style

Leaders tell their employees what they want done and how thay wat it accomplished, without getting the advice of their followers

APPLICATION:When leaders have all information to solve the problem. Also it is applied when the period of execution is short and when the employee are well motivated.

Participative leadership

This involves the leader including one or more employees in the decision making process (determining what to do and how to do it). However the leader maintains the final decision making authority.

CAUTION:Using this style is not a sign of weakness, rather it is a sign of strength that your employees will respect.

USED:When you have part of the information and employee have other parts.

NB. A leader is not expected to know everything-this is why you employ knowledgeable and skillful employees.

IMPORTANCE: Is a mutual benefit. It allows them to become part of the team and allows you to make better decisions.

Huyu utamwita kiongozi

Kiongozi
-hana ushawishi
-hana motisha, hana malengo
-hafanyi jitahada zozote kuhakikisha mambo yanafanikiwa
-haongozi
-haweki mambo sawa
-haandai shughuli kwa ufasaha.

Sasa unapokaribishwa karibu sana kiongozi wetu wakati wewe sifa zako ni hizo hapo juu hebu jichunguze mwenzetu. Ili uitwe kiongozi badilisha hizo sifa ziwe chanya.

Usimwite Meneja kama hana sifa za umeneja

Wengi tumezoea na kukubali kuitwa meneja. Tanzania tunao mameneja wengi sana. Meneja wa baa, meneja mama ntilie, meneja wa timu ya mpira, meneja wa kiwanda cha sukari n.k.. Sina ubishi kuwa meneja anaweza kuwa mahali popote jikoni, shuleni, hospitali, ofisini,kiwandani. Lakini ni sharti tujiulize wanafanya kazi hizi?
1) Wanapanga?
2)Wanaratibu?
3)Wanaongoza?
4)Wanaandaa?
5)Wanasimamia raslimali?

Kama hawafanyi kazi nilizotaja hapo juu hawastahili kuitwa meneja hao jina kubwa lakini hakuna wanalofanya!

Tuesday, March 20, 2012

Waswazi na Utamaduni wao


Waswazi wanatunza utamaduni wao. Taifa lao linaongozwa na Mfalme (King Mswati III).
Utamaduni una nguvu sana hapa Swaziland ingawa umagharibi unaingia kwa kasi hasa kwa vijana.Waswazi wanapenda sana lugha yao Kiswati. Wanapenda kukonyesha ngoma zao za asili, nyumba zao, mavazi yao na mambo kadha wa kadhaa. Mfalme anaongoza nchi pamoja na mama yake.

Wednesday, March 14, 2012

Siyabonga kakhulu-Asante sana


Mawasiliano ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu.Hapa Swaziland wenyeji wanawasiliana kwa lugha ijulikanayo 'Kiswati'.Unapotaka kushukuru kwa huduma nzuri i
uliyopewa unasema 'Siyabonga kakhulu' maana yake asante sana. Pia unapotaka kumsalimia mwenzako unamwambia 'kunjani.' Hii ina maana habari yako au mambo!Ndiyo hivyo tena lazima lugha ipande ukitaka kuishi na watu ugenini. Siku njema. (Pichani Bw. Collins mmoja wa wawezeshaji wa Mananga Centre akimtunuku cheti mmoja wa washiriki wa course za Mananga)

Monday, March 12, 2012

Masomoni Swaziland

Nimewasili nchini Swaziland jana tarehe 11/03/2012 kwa madhumuni ya mafunzo ya muda mfupi. Nipo chuoni Mananga kilichopo mji mdogo ujulikanao Ezuilini. Swaziland ni nchi ya vilima vilima.Nimefahamishwa kuwa idadi ya watu nchi nzima ni watu milioni 1.2 ni watu wachache sana karibu hii ni robo ya idadi ya watu walioko jijini Dar Es Salaam.Uchumi wa nchi hii hutegemea kilimo cha miwa. Swaziland inaoongozwa na King Mswati. Pasaka tutakula wote hapo nyumbani. Mkiona kimya nimetingwa na shule!1600

Thursday, March 1, 2012

Kilimanjaro kanuna

Kuna wakati mwingine mlima kilimanjaro unaonekana vizuri sana vilima vyote viwili Kibo na Mawenzi, kuna wakati unaona kilima kimoja tu na kuna wakati huoni kitu kabisa na wakati mwingine hauonekani vizuri. Nikiwa njia panda ya Himo niliweza kupata picha hii ya mlima Kilimanjaro hali haikuwa nzuri. Kweli Kilimanjaro kanuna.

Waulize watoto watakwambia

Watoto hawa tuliwakuta njiapanda ya Himo mkoani Kilimanjaro. Bw. Omary alipata fursa ya kuzungumza nao. Kwa mujibu wa Bw. Omary Kizito watoto hao walijeleza wao ni nani na wako hapo kituoni wakisubiri gari la kwenda shuleni na kwa kuwa ilikuwa siku ya Ijumaa walikuwa wamevalia sare za michezo. Angalia njumu mguuni!

Mambo ya field

Wakati mwingine inabidi kwenda nyumbani ya kwa wakulima na kuhojiana. Inaposhindikana kwend na magari basi hivi ndivyo inavyokuwa.