Kwa mkazi wa wilaya ya Temeke, au kwa yeyote yule aliyekwisha fika Tandika kwa kupitia Sokota anaifahamu sehemu korofi pale kwenye kituo cha mafuta - Sokota unapoacha barabara ya Mandela na kuingia Sokota kuelekea Kituo cha Polisi Chang'ombe.
Nasema korofi kwa nini? Mvua ikinyesha kidogo tu basi maji kibao, maji yakikauka huacha korongo kubwa. Ukarabati wa kibabaishaji umekuwa ukifanyika mara kwa mara. Mara wamwage kifusi- ambacho hugeuka tope mara wafanye hivi lakini haikusaidia. Shida, karaha wakati wote na wakati mwingine uharibifu huu wa barabara umekuwa ukisababisha ajali zisizo za lazima.
Mkandarasi amepatikana tokea mwaka jana kujenga "culvert" au kwa lugha ya kawaida ya mtaani kalavati (mtaro wa maji chini ya ardhi). Cha kushangaza mtaro huu umechukua miezi minne kukamilika. Jamani, kalavati moja tu hilo, miezi 4 sasa kweli huo ndiyo uwajibikaji? Kwa miezi 4 usafiri kupitia sehemu hiyo ulikuwa umefungwa, fikiria mwenyewe usumbufu karaha na mambo mengine. Kweli kwa mtindo huu Watanzania tutafika? Tena zabuni hiyo amepewa mzalendo. Kujenga kalavati moja miezi 4? Akinyimwa oh hatuna uzalendo. Mimi ninachojali bwana huduma safi mtu apewe kazi kutegemea uwezo siyo kubebana bebana hapa tumechoka na hali hii. BoT wabebane hata kwenye kalavati?
2 comments:
Hivi wilaya ya TEMEKE imeikosea nini serikali barabara za kwenda YOMBO,TANDIKA,MBAGALA zote mbovu kwa ujumla MIUNDOMBINU yote iko hoi.Umesahau barabara ya SAM NUJOMA(UBUNGO-MWENGE) ina urefu wa 2km lakini inatengenezwa kwa miaka 2 kwa hiyo hilo karavati muda bado.LAKINI TATIZO NI NINI WHY?
Post a Comment