Jana jioni wakati natoka kazini kurudi nyumbani kwangu Kisemvule kwa kupitia barabara ya Kilwa, pale Mwandege kulitokea ajali mbaya iliyohusisha bus ndogo za abiria na shangingi moja (nasikia ni mali ya mahakama). Habari nilizozipata ni kwamba watu watatu walifariki papo hapo na wengine kuumia vibaya.
Ajali hizi za mara kwa mara zinaongezeka siku hadi siku.Watu wanapoteza maisha lakini mambo ni yale yale. Gari zina kwenda mwendo wa kasi bila sababu ya msingi. Katika kipindi cha mwezi mmoja kwenye barabara hiyo kumetoka si chini ya ajali 10 na kupoteza maisha si chini ya watu 10.
Hivi kweli tumeshindwa kudhibiti ajali za barabarani? Mimi naona inawezekana kabisa. Sheria za barabarani zipo zifuatwe. Magari yakaguliwe na anayekosa apate adhabu kali bila ya kuwapa muda wa kuzungumza au kumuona fulani ili kesi idhoofishwe. Ajali za barabarani ni kama mauaji ya Albino zinatumaliza Watanzania. Tutaogopa kupanda magari!
No comments:
Post a Comment