Friday, July 24, 2009
Jengo la Bunge- Dodoma kama meli vile
Umeshawahi kufika Dodoma? Moja ya vivutio vya majengo katika mji huo ambao ndiko Bunge la nchi hii linako endesha vikao vya Bunge ni jengo la Bunge. Jengo hili ni zuri sana kwa ndani na nje. Kama sikosei ni bora Afrika Mashariki na ya kati. Hebu angalia kwenye picha linavyovutia kama meli vile!
Kilimo yawatunuku wafanyakazi bora mwaka 2009
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika usiku wa tarehe 22/07/2009 uliwatunukia vyeti vya ufanyakazi hodari wafanyakazi 16 wa wizara hiyo katika sherehe kabambe iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Dodoma Hotel. Pamoja na Vyeti kila mmoja alipata Hundi yenye thamani ya Tshs 300,000/= pichani Mtafiti Mkuu Bw.Ninatubu Lema akijatayarisha kupewa cheti na aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo Mhe. Stephen Wasira, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika.
Thursday, July 23, 2009
Uchafu unatugaharimu USD 23.5 billion kwa mwaka
Uchafu unaigharimu Afrika USD 23.5 billion kwa mwaka - kwa ajili ya kutibu magonjwa, vifo visivyotarajiwa, uzalishaji duni,tatizo la kukusanya maji, na kwa kuharibu vyanzo vya utalii.
Mwandishi wa Habari maarufu Afrika Mashariki Charles Onyango Obo alikuwa na hili la kuhitimisha- That's TIDY SUM!
Mwandishi wa Habari maarufu Afrika Mashariki Charles Onyango Obo alikuwa na hili la kuhitimisha- That's TIDY SUM!
Uchafu unaua watoto wa kiafrika 600,000 kwa mwaka
Imebainika kuwa uchafu na maji yasiyo salama ni chanzo cha vifo vya watoto 600,000 wanaofarika barani Afrika kila mwaka. Hebu fikiria watoto 600,000 ni mabus mangapi ya abood ya kwenda Morogoro? 10,000 yenye maiti!
Rwanda wanahifadhi misitu-Mkuranga wanatekeza Mwandege
Licha ya kupigana vita ya wenyewe kwa wenyewe, Rwanda inapiga kasi katika maendeleo. Ni nchi ndogo lakini mara kwa mara inatusumbua katika soka. Nasikia pia mji wa Kigali ni msafi sana. Wanajifunza kwa haraka sana mambo mengi. Na hili la kuongoza kwa kuhifadhi misitu linalipa kwenye mazingira. Mambo kwa vitendo, mipango pekee haitoshi. Wakati Rwanda wanahifadhi misitu Wamkuranga hawaoni umuhimu wa msitu wa Mwandege.
Kikwete kufungua "seacom fibre optic cable" leo
Hii maana yake nini kwa wananchi wa Tanzania? Tunategemea kushuka kwa gharama za mawasiliano. Tusubiri tuone.
Msukuma aliyekataa kufunga mkanda ndani ya ndege
Gazeti la kila siku la Habari leo tarehe ya leo ilikuwa na habari nzuri sana ya Msukuma aliyekataa kufunga mkanda akiwa ndani ya ndege ya Precision Air kwenda Mwanza. Alikataa kata kata hadi alipofungwa kwa nguvu na wahudumu wa ndege. Aidha Msukuma huyo alipanda na bakora yake na alikataa kabisa kuiacha. Kwa habari zaidi soma Habari leo la tarehe 23 Julai 2009. Vipi mtani nasikia ulifiri umo ndani ya nyumba kubwa!
Tabia ya uongo si nzuri
Kusema uongo ni dhambi dini zote zinasema hivyo. Jamii pia haipendi mtu mwongo. Uongo unarudisha nyuma maendeleo ya mtu binafasi, jumuiya na Taifa. Hebu fikiria pale wananchi wanapoahaidiwa na serikali yao kujengewa barabara safi kwa muda fulani halafu haijengwi! Fikiria mzazi unapoahidi kumsomesha mtoto wako kwenye sekondari za kulipia halafu wakati unapofika hutimizi ahadi hiyo. Inakuwaje? Tabia ya uongo zi nzuri.
Nishati ya Jua gharama ziwe nafuu
Moja ya magazeti ya kila siku hapa nchini limeandika kuwa Serikali imepania katika kuhakikisha kuwa nishati ya Jua inapewa kipaumbele kinachostahili. Huu ni mtazamo mzuri. Jambo jema ni utekelezaji wake. Iwapo tutafanikiwa katika hili nina uhakika tutasonga mbele kimaendeleo kwa kasi zaidi. Upatikanaji wa jua hapa nchini si wa mashaka kama ilivyo kwa nchi za ulaya. Hii ndiyo sababu kubwa ya kuweka msisitizo wa uendelezaji wa nishati ya jua. Kwa hili mijini na vijijini watanufaika sana lakini endapo tu gharama za nishati hii zitakakuwa nafuu kwa wananchi wa vipato mabalimbali.
Tuesday, July 14, 2009
Hotel Accra bado
Nipo hapa Accra Ghana tangu tarehe 11 Julai 2009 usiku kwa mwaliko wa SADC/ICART kushiriki kongamano linalohusu Habari na Mawasilino katika Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Afrika. Naanza kwa kusema kuwa kwenye hoteli hii niliyofikia naona huduma zimezorota kidogo hasa katika maakuli pamoja na kuwa kweli Hotel ni nzuri lakini utendaji wa wahudumu wa sehemu ya chakula ni wa mashaka sana.Sijui kwa mahotel mengine lakini hii haijafua dafu na kwetu Tz!
Monday, July 6, 2009
Kilimo cha Mpunga Kanda ya Kaskazini kinalipa
Kutokana na tafiti zilizofanywa hivi karibuni wataalamu wa uchumi jamii na mifumo ya kilimo wamebaini kuwa kwa eneo la hekta moja, kilimo cha mpunga kinalipa zaidi ya mahindi na mtama iwapo mkulima atatumia mbegu bora na pembejeo muhimu za kuzalisha mazao hayo ikiwemo mbolea. Imedhihirika kuwa kwa hekta moja mkulima anaweza kupata faida ya Tshs 1,412,100/= akilima mpunga wakati mahindi yanaweza kutoa faida ya Tshs 1,269,400 na mtama Tshs 163,200/= . Mahesabu haya yamefanywa kwa kuzingatia bei za mwaka 2006/07.
Sielewi kwa nini Michael Jackson alichukia kuwa mweusi
Mimi ni mwafrika tena ni mweusi. Najivunia kuitwa Mwafrika, na pia najivunia kuwa mweusi. Kwa marehemu Michael Jackson mambo hayakuwa hivyo alitumia fedha nyingi kujibadili kutoka rangi nyeusi kuwa nyeupe.
Quincy Jones mtaalamu wa muziki aliyekuwa akimtayarishia Michael album zake nyingi za muziki alisema kuwa mwimbaji huyo aliongopa kuhusu ngozi yake na kwamba alikuwa hapendi kuwa mweusi.
Quincy Jones mtaalamu wa muziki aliyekuwa akimtayarishia Michael album zake nyingi za muziki alisema kuwa mwimbaji huyo aliongopa kuhusu ngozi yake na kwamba alikuwa hapendi kuwa mweusi.
Mahakama ya Kadhi isiwe sababu ya kutoelewana
Watanzania tumeishi kwa miongo mingi bila kuwa na Mahakama ya Kadhi. Na sijui tumeathirika vipi kwa kutokuwa nayo. Leo hii serikali inapokataa kuwa na Mahakama hiyo imetafakari kwa kina kuhusu jambo hilo. Kwahiyo kuwepo na kutokuwepo kwa Mahakama ya Kadhi isiwe sababu kwa Watanzania kukosa kuelewana.
Watafiti wastaafu waagwa rasmi
Tafrija kabambe ya kuwaaga wastaafu watafiti kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ilifanyika siku ya Ijumaa tarehe 3 Julai 2009 kwenye makao makuu ya Wizara yaliyoko Temeke Tazara Veterinary. Jumla ya watafiti 8 waliagwa katika hafla hiyo akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Dkt. Jeremiah Haki. Wengine ni Dkt Alfred Moshi aliyekuwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kanda ya Mashariki, Bw. Onesmo Ishumi aliyekuwa Afisa Kiungo wa Utafiti na Ugani Kanda ya Mashariki, Bw. Cyprian Ponjee aliyekuwa Afisa Kiungo Utafiti na Ugani Kanda ya Kusini, Afisa Mipango wa Idara Bw. Ahmed Juma Ahmed, Aliyekuwa Afisa Manunuzi wa Idara Bw. David Mkanta,Bw. Habel Chambo na Bi Beatrice Gembe aliyekuwa Katibu wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo. \
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Bi. Sophia Kaduma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ambaye aliwatunukia zawadi mbalimbali wastaafu hao.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Bi. Sophia Kaduma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ambaye aliwatunukia zawadi mbalimbali wastaafu hao.
Subscribe to:
Posts (Atom)