Monday, July 6, 2009

Watafiti wastaafu waagwa rasmi

Tafrija kabambe ya kuwaaga wastaafu watafiti kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ilifanyika siku ya Ijumaa tarehe 3 Julai 2009 kwenye makao makuu ya Wizara yaliyoko Temeke Tazara Veterinary. Jumla ya watafiti 8 waliagwa katika hafla hiyo akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Dkt. Jeremiah Haki. Wengine ni Dkt Alfred Moshi aliyekuwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kanda ya Mashariki, Bw. Onesmo Ishumi aliyekuwa Afisa Kiungo wa Utafiti na Ugani Kanda ya Mashariki, Bw. Cyprian Ponjee aliyekuwa Afisa Kiungo Utafiti na Ugani Kanda ya Kusini, Afisa Mipango wa Idara Bw. Ahmed Juma Ahmed, Aliyekuwa Afisa Manunuzi wa Idara Bw. David Mkanta,Bw. Habel Chambo na Bi Beatrice Gembe aliyekuwa Katibu wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo. \

Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Bi. Sophia Kaduma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ambaye aliwatunukia zawadi mbalimbali wastaafu hao.

No comments: