Thursday, March 25, 2010
Gozi litakalotumika Afrika ya Kusini ni 'JABULANI'
Ikiwa zimebakia takribani siku 77 kabla ya fainali za kombe la soka la dunia 2010 kupigwa katika ardhi ya Afrika huko Afrika ya kusini. Unalifahamu jina la mprira utakaotumika katika fainali hizo? Unaitwa "JABULANI.' unaoonekana pichani.
Fainali ya kwanza ya Kombe la dunia 1930
Mpira uliotumiwa kwa mashindano ya kwanza ya kombe la dunia mwaka 1930 ulijulikana kwa jina la tiento. Fainali zilifanyika nchini Uruguay. Wakati huo ilikuwa ni muhimu kubeba pump. Bin gwa wa fainali hizi ilikuwa ni nchi ya Uruguay. Mipira miwili ilitumika ya nchi tofauti. Nusu ya kwanza ulitumiwa wa Argentina matokeo ya nusu ya kwanza Argentina ilikuwa ikiongoza kwa bao 2-1 baada ya mapumziko mpira wa Uruguay ulitumika na kuibuka na ushindi wa mabao 4-1. Mimi nilicheza huo mpira wa rangi ya chungwa!
Tuesday, March 23, 2010
Benki ya Kanisa Katoliki yazinduliwa
Ili iweze kujitegemea zaidi Kanisa Katoliki Tanzania limeamua kuanzisha Benki ya Biashara ijulikanayo kwa jina la Mkombozi Commercial Bank. Benki hii iliyoanzishwa rasmi mwezi Agosti 2009 kwa mtaji wa Tshs 6.5 bilioni haichagui mteja.
Kwa kushirikiana na Benki za Azania Bancorp, Tanzania Investment Bank, Twiga Bancorp, Dar Es Salaam Community Bank, BOA, Akiba Commercial Bank, Uchumi, Tanzania Women Bank na Access Bank unaweza kutumia ATMs zao kutoa fedha. Benki hii imeanza kutoa mikopo ya biashara na elimu wote wanakaribishwa kufungua akaunti kwenye Benki hiyo.
Yapo mazingira yanayohitaji kiboko
Leo kwenye gazeti la Mwananchi kuna makala yenye kichwa cha habari 'Viboko havifunzi mwana.' Nakubali na kukataa. Inategemea aina ya viboko na mazingira yanayohitaji mtoto kuchapwa. Kuna watoto wengine hawaonyeki bila ya viboko. Tusichukue kila kitu kutoka kwa wazungu kuwa eti kuchapa hairuhusiwi. Asilimia 80 ya wanafunzi tuliomaliza shule miaka 20 iliyopita tulichapwa na tukaonyeka. Si kila ushauri kutoka nje ni mzuri. Kuchapa hakuui. Mtoto wangu nitaruhusu achapwe shuleni kwa kufuata taratibu za shule zilizopo. Wadau mnasemaje kwa hili.
Kipanya bwana!
Kuku hawauzwi hivi
Mifereji iko wapi hapa?
Hii ndiyo barabara ya Kilwa sehemu ya Mbagala inayojulikana kama Kipati. Mifererji haijakamilika kwahiyo mvua zinazoendelea kunyesha zinaharibu barabara hiyo iliyojengwa hivi karibuni. Kwa nini hatuwi makini katika utekelezaji wa mambo yetu. TAFAKARI (Picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi la tarehe 23/3/20100
Si ushamba anawajibika
Kwa makabila mengi ya Tanzania ni nadra sana kumuona mwanaume akimbeba mtoto. Kazi ya kubeba mtoto jamii inaiona kama ni kazi ya mwanamke. Lakini hebu tujiulize, yule mtoto ni wa mwanamke tu? Kuna ubaya gani kushirikiana katika kulea watoto wetu. Huo si ushamba kama wengine wanavyouona. Hebu angalia kwenye picha jamaa kambeba mwanae hana wasiwasi anakatisha mitaa.
Saturday, March 20, 2010
Simba yaibanjua Lengthens ya Zimbabwe 3-0
MUNGU MPELEMBAJI NA MTATHMINI No 1
Nipo hapa Pretoria- Afrika ya Kusini kwa muda wa siku tano sasa nikipata msasa katika taaluma ya Kupelemba na Kutathmini Shirikikishi (Participatory Monitoring and Evaluation). Mafunzo haya yameandaliwa na SADC . Washiriki ni wadau kutoka katika nchi zinazounda SADC (South Africa haina mwakilishi. Kuna wawakilishi wawili kutoka Tanzania. Pamoja na mambo mengine nimepata kufahamu kuwa MUNGU ni Mpelembaji na Mtathmini namba moja. Kwani sisi ni wadau wake na ana nyenzo mbalimbali za kufanya hiyo kazi. Tunapopelemba na kutathmini shughuli yoyote ile lengo lake ni kukusanya taarifa zitakazotuwezesha kufahamu mwenendo wa utekelezaji wa kazi,mradi katika muda fulani kwa kuzingatia malengo tuliyojiwekea. Tunapata kutambua mafanikio na changamoto ambazo zinaweza kutusaidia katika kufanya maamuzi. Lakini shughuli ili iwe na mafanikio inabidi kushirikisha wadau hii hasa ndiyo maana ya 'Participatory'Je, wewe unayesoma blog hii una amini?
Sunday, March 14, 2010
Tutafurika hivi uwanja wa UHURU?
Taifa Queens wametutoa kimasomaso Watanzania kwa kuibugiza timu ya soka ya wanawake ya Ethiopia mabao 3-1 nyumbani kwao. Lakini Waethiopia walionyesha uzalendo wa hali ya juu. Uwanja ulifurika kuwapa nguvu wanawake hao. Sisi je? Banzi wa Moro anaahidi kuingia uwanjani siku ya mechi ya marudiano. Tuombe Mungu.
Miundo mbinu yetu choka mbaya
Lori limekwama! Mvua za masika zimeanza kunyesha kwa wingi nchini kote. Kwa vyovyote vile zimewahi sana, pengine ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Barabara zetu huathirika sana wakati mvua zinaponyesha. Hii husababisha hata bidhaa kuadimika na kuuzwa kwa bei ya juu katika sehemu nyingi. Anayeathirika zaidi na mwananchi wa kijijini. Tutafakari.
Kata kiu yako kwa dafu!
Hawa watapata elimu nzuri waliosalia je?
Unamkumbuka huyu?
Soko Kuu la Morogoro
Nilishawahi kuandika kwenye blog hii kuwa soko la Morogoro ni chafu hasa wakati mvua zinanyesha. Huwezi kuamini kuwa soko hilo ndilo tegemeo kwa wakazi wa Morogoro kwa aina mbalimbali za vyakula. Iwapo viongozi husika wameshaanza kulifanyia kazi tatizo hilo basi ni vizuri. Lakini kama mambo yenyewe ni kama inavyoonekana pichani kazi bado ipo. Picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi la tarehe 13/3/2010.
Monday, March 8, 2010
Mahindi debe shilingi 7,000/ tu!
Eti debe la viazi ni shilingi 2500/=
Blog ya Mjengwa leo imejaa picha za mazao yanayouzwa kwa bei ya kutupwa huko Makambako Iringa. Debe la viazi mviringo linauzwa kwa bei ya shilingi 2500/= . Maana yake ili aweze kununua bati moja itambidi auze madebe yasiyopungua sita. Madebe 180 ya viazi ndiyo yanayotosheleza kununua mabati 30 yanayotosho kuezeka nyumba ndogo.Katika hali hii si rahisi kukipenda kilimo.
Wednesday, March 3, 2010
Wachina na biashara ya magogo
Hivi karibuni sehemu ninayoishi mimi miembe kadhaa imeangushwa na kukatwa vipingili vidogo vidogo. Wilaya ya kilosa pia biashara ya magogo hasa ya miti ya mazao kama vile miembe na minazi imeshamiri. Na imebainika kuwa matajiri wa biashara hiyo ni Wachina. Wanavifanyia nini vigogo hivyo hatujui. Nani karuhusu biashara hiyo. Pia hatujui. Tusije kushangaa kukosa embe. Tusije kushangaa kukosa nazi. Haya yote ni ya kujitakia.
Pombe na UKIMWI
Hivi unywaji wa pombe unachangia kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa wa UKIMWI. Huko Iringa wanasemaje? "Msimu wa Ulanz\i huwa unauzwa bei rahisi ambayo hakuna inayemsinda ndo maana watu wengi hulewa hivyo kuwa rahisi kwao kufanya ngono bila kujiandaa kwani wanawake wengi wakishanunuliwa kinywaji hicho huwa wapesi kukubali," anasema Richard Mwenda. (Nukuu na picha kutoka gazeti la Mwananchi la 15/01/2010)
Tulikula mananasi
Wakulima wadogowadogo wanailisha Tanzania. Miezi mitatu iliyopita ilikuwa miezi ya mananasi. Jiji la Dar lilitapakaa kwa mananasi. Bahati mbaya mengi yalioza kwa kukosa teknolojia za kuhifadhi matunda au za kuongeza thamani.
Wakulima walio wengi wanalima kwa mazoea, wanalima kwa kubahatisha. Kilimo hapa Tanzania hakilipi sana. Miundo mbinu ni mibovu. Hakuna mitandao mizuri ya kuwawezesha wakulima kupata mikopo. Bila mikopo kilimo hakina faida. Huwezi kulima zaidi ya ekari mbili!
Ulanga kujenga nyumba za watumishi
Hivi karibuni wilaya ya Ulanga imetangaza mpango wa kujenga nyumba 14 za watumishi ambazo zitakaliwa na familia zipatazo 28. Kwa mujibu wa Mhandisi wa ujenzi wa wilaya hiyo, Hassan Matua mkakati wa ujenzi wa nyumba hizo umekuja baada ya kubaini kuwa watumishi wa sekta mbalimbali waliokuwa wakipangiwa kufanya kazi katika wilaya hiyo kukimbia kutokana na mazingira magumu pamoja na ukosefu wa nyumba. Huu ni mfano mzuri wa kuigwa na ni kivutio kwa wafanyakazi.
Miundo mbinu ya Jiji la Dar Es Salaam hoi!
Angalia pichani jinsi wananchi wanavyoteseka kutokana na miundombinu mibovu iliyoko Jijini Dar Es Salaam. Leo katika gazeti la Mwananchi nimeinyaka picha hii ikionyesha mkazi wa Rieta eneo la Makoka Mwisho jijini Dar Es Salaam akimvusha msichana wa shule katika daraja lililobomolewa kutokana na mafuriko ya mvua zilizonyesha hivi karibuni.
TAIFA STARS UBISHOO!
Wafadhili wa nguvu wamejitokeza kuihudumia Taifa Stars ( NMB, Serengeti Breweries). Kocha wa kimataifa Maximo wanaye. Wapenzi wapo wanaishangilia kwa nguvu inapocheza. Mshiko mwanangu wa uhakika.Hebu angalia pichani wachaezaji wa Taifa Stars wakifanya mazoezi wakiwa na pamba za Serengeti wanapendeza eti! Tatizo inapokwa kwenye mashindano upuuzi mtupu. Tatizo ni ubishoo na kujifanya wamefika. Hebu mwangalie huyu mchezaji wa mbele tayari ameshafuga nywele kama Valderama!
Nguvu ya CCJ inatoka wapi?
Subscribe to:
Posts (Atom)