Tuesday, March 23, 2010

Yapo mazingira yanayohitaji kiboko


Leo kwenye gazeti la Mwananchi kuna makala yenye kichwa cha habari 'Viboko havifunzi mwana.' Nakubali na kukataa. Inategemea aina ya viboko na mazingira yanayohitaji mtoto kuchapwa. Kuna watoto wengine hawaonyeki bila ya viboko. Tusichukue kila kitu kutoka kwa wazungu kuwa eti kuchapa hairuhusiwi. Asilimia 80 ya wanafunzi tuliomaliza shule miaka 20 iliyopita tulichapwa na tukaonyeka. Si kila ushauri kutoka nje ni mzuri. Kuchapa hakuui. Mtoto wangu nitaruhusu achapwe shuleni kwa kufuata taratibu za shule zilizopo. Wadau mnasemaje kwa hili.

3 comments:

sophia kizito said...

hi banzi wa moro, nakubaliana na wewe, mtoto wa kiafrika asifananishwe kimalezi na mtoto wa ulya, tuwalee watoto wetu kwa maadili tuliyolelewa sis, tofauti na hapo tutaharibu kizazi kijacho, inafika wakati mtoto lazima wachapwe ili anyooke,hata wanajeshi labda kuna mbinu inatumika kuwalazimisha wajitume.
nakufagilia ndugu yangu blog yako inatoa uhalisia wa mambo, kama itakuwa inasomwa na wengi ni changamoto kwa kilasekta, kwani unamgusa kila mtu wa kila rika na mapendekezo yake.
big up Banzi wa moro.
sophia O kizito

Innocent John Banzi said...

Asante sana shem Sophia. Nashukuru kwa comments zako. Si wengi wanaotoa comments wakimaliza kusoma. Comments zinatoa challenge kwangu.

Innocent John Banzi said...

Shem sophia, ni kweli samaki mkunze angali mbichi. Haya mambo ya kuiga ulaya kila kitu itatumaliza!