Sunday, November 28, 2010

Tunaposhindwa kujitosheleza kwa umeme

Ili nchi iweze kuendelea, nishati ya umeme ni lazima ipewe kipaumbele. Nchi nyingi nilizowahi kutembelea hasa Ulaya. Suala la kukosa umeme hata kwa dakika tano tu halijawahi kutokea. Hapa nyumbani ukatikaji wa umeme ni kitu cha kawaida kabisa. Umeme unaweza kukatika hata kwa miezi mitatu na bado kusiwe na uhakika wa kupatikana. Kibaya ni pale ambapo tunapopata maelezo yanayobadilika kila kukicha kutoka kwa mamlaka husika. Leo, Transformer ya Kipawa imeharibika, kesho mtambo wa Songas umeshindwa kuzalisha umeme. Keshokutwa IPTL imekosa mafuta ya kuendesha mitambo, mtondogoo kina cha maji Kidatu kimeshuka. Tatizo ni nini hasa? Kwa kukosa umeme uzalishaji katika sekta zote huathirika. Siyo wakati wa kuweka mkakati. Tunahitaji umeme wa uhakika.

Dar inaoza!

Jana katika pitapita zangu maeneo ya Kariakoo hasa mtaa wa Msimbazi nilikuta uchafu wa kutisha. Mitaro imeziba na maji machafu yalikuwa ya kitiririka.Ni balaa kabisa. Kama unatembea na viatu vya wazi ni rahisi kabisa kugusa maji hayo machafu na yanukayo.

Tatizo nilionalo ambalo ni kiini cha uchafu uliokithiri jijini ni watu wenyewe. Mitaro imezibwa kwa chupa za maji takataka za mazao mabalimbali na mifuko ya plastiki.

Jambo jingine ni kwamba jiji halina utaratibu mzuri wa kuliweka jiji katika hali ya usafi.Hivi kuna mabwana afya wa jiji kweli. Ah, jamani inabidi kulinda afya za wananchi, aidha jiji lazima livutie kwa usafi. Tujizatiti sote kuiweka DAR ssfi.

Monday, November 22, 2010

Hawa ndiyo wabunge wako


Huu ndiyo mtazamo wa bunge jipya!

Hatujamuelewa Papa kuhusu matumizi ya Kondom


Baba Mtakatifu Benedict xvi hajahalalisha matumizi ya kondom kama wengi wanavyodai. Alichosema pale inapobidi ili kuokoa UHAI Kondom inaweza kutumika. Inabidi tutafakari kwa kina vinginevyo tunaweza kupotosha.

Utamu wa pweza uonje!


Zamani nilikuwa sili pweza lakini siku hizi nikiwaona tu wamekaangwa na kuwekwa mezani pale Buguruni au Mbagala sikosi kuonja kipande kimoja au viwili. Kuna vipande vinavyouzwa sh.100/= (kidogo) na kikubwa sh. 200/=. Ukitaka kumfaidi pweza lazima uweke chachandu. Angalia bakuli la chachandu pichani.

Alipohutubia walitoka



Wakati Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia Bunge jipya kwa mara ya kwanza Novemba mwaka huu. Wabunge wa CHADEMA walitoka ukumbini. Kisa? Hawamtambui RAIS. Hivi muswada ukipitishwa Bungeni mtu wa mwisho kusaini ni nani?

Thursday, November 4, 2010

What are the signs of high blood Pressure?

How do you know if you have it or not?
The bad news is that in most cases you simply can't tell-high blood pressure, or hypertension, usually has no symptoms that you can detect.

Hypertension is called "the silent killer" because with time, untreated, it can lead to a variety of health problems, and does so without you noticing anything.

High blood pressure can lead to increased heart size, aneursyms, kidney failure and arthelescerosis, where your arteries become damaged - and other serious health problems. (cont...)

Blood Pressure

Wasomaji wangu, leo nimeona niwaletee hii makala bila ya kuitafsiri kwani ni ya maana sana kwa maisha yetu.

What is Blood Pressure?

Blood pressure is the measure of how much pressure your blood puts against the various blood vessels of your body. It is important because if it is too high, your body, and especially your heart, will slowly start to become damaged.

The damage this causes takes a lot of time to happen but can be very serious-it can lead to issues like coronary artery disease, stroke and kidney damage, among other things.

Heart disease is a single worst killer of people in many parts of the world. (cont....)

Zawadi kutoka kwa Wazazi


Wazazi wa Eric walikuwa wa kwanza kutoa zawadi. Wao walimvisha Rosari!

Mjomba hakosi zawadi


Ningekuwa Matombo ningepeleka kuku au mbuzi na mke wangu asingekosa kikapo cha mpunga. Kwa kuwa shughuli hii ilifanyika katika mazingira ya kileo tena mjini Morogoro zawadi yangu ilikuwa ni hii. Msiniulize kilichomo ndani ya box!

Wednesday, November 3, 2010

Tukishatoa zwadi tunapongeza wazazi


Ni kawaida yetu tukishatoa zawadi tunawapongeza watu muhimu kama vile wazazi.Pichani Baba mkubwa wa Eric Prof.Moshi akimpongeza mama Eric. Hongera shemeji!

Prof. Moshi kanisani Kigurunyembe

Haitoshi tu kuserebuka. Inatupasa kuhuduria ibada pia.

Monday, November 1, 2010

Kutunza na kutunzwa


Wazazi walitunzwa na Amina alitunzwa. Ndivyo ilivyokuwa siku ya Send Off ya Amina usiku wa tarehe 23/10/2010 katika ukumbi wa VETA - Mikumi.

Ulikuwa mwezi wa shughuli


Tulianza kwa kumwaga Joyce Kyando Luhungu. Baadaye Ushemasi wa tarehe 23/10/2010Jakka Oscar wa Morogoro.Jioni kule Mikumi Send-Off ya Amina Omary Jakka. Kesho yake 24/10/2010- Morogoro, Komunio ya kwanza ya Eric Mkoba. Watu ni wale wale ilibidi wengine wagawane kwani kote kulituhusu. Lakini kuna wale waliobahatika kuhudhuria shughuli zote tatu Mungu awabariki. Pichani Amina Jakka(kulia) akiwa na mmewe kwenye Send-Off ya Mikumi.