Friday, October 21, 2011

Nani aanze kupita?

Tatizo la msongamano wa magari katika jiji la Dar Es Salaam ni kubwa sana. Hapa ni katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela pale Tazara. Nani aanze kupita?

Wachina nao


Tarehe 19/10/2011 ujumbe mzito kutoka Akademia ya Sayansi ya Kilimo ya China (CAAS)ilitembelea Makao Makuu ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Dar Es Salaam na kfanya mazungumzo na watendaji wakuu wa Wizara jinsi ya kuanzisha mashirikiano katika sayansi ya kilimo kwa lengo la kuboresha kilimo hapa nchini hasa kwa upande wa Utafiti wa Kilimo. Pichani wataalamu hao wakiwa katika mazungumzo na wataalamu wetu.

Thursday, October 20, 2011

Miaka 50 mawaziri 16 wa Kilimo


Waheshimiwa hawa 16 kwa vipindi tofauti wameiongoza wizara ya Kilimo yenye dhamana kubwa ya kuhakisha kuwa chakula kinapatikana,ajira kwa asilimia kubwa ya wananchi wake pamoja na uhakika wa kipato na uchumi wa Taifa hili la Tanzania. Kwa kipindi hicho chote Wizara imeongozwa na mwanamke mmoja!

Mhitimu anapovishwa taji

Mwajuma akivishwa taji na dada yake baada ya kuhitimu kidato cha nne.

Mama na mwana kwenye Mahafali ya Kidato cha Nne Vikindu

Mwajuma Pembe akipongezwa na mama yake baada ya kuhitimu Kidato cha Nne

Utamu wa ngoma


Ngoma inapopigwa juu ya kifua!

BoT na miradi ya Kilimo


Mwaka 1973 Benki Kuu (Bank of Tanzania) iliweza kuchangia shughuli za uwekezaji katika kilimo (ufugaji wa nguruwe)hapa nchini. Hali ya sasa je?

Wednesday, October 19, 2011

Kambare na Kitoga


Kamabare na Kitoga ni aina ya samaki wapatikanao kwenye maji baridi. Si rahisi sana kuwatofautisha wanapokuwa wakubwa hasa wakipasuliwa.Hatan hivyo wengi tunawatambua kambare wadogo waliokaushwa na kukunjwa mikia yao ikitafuna midomo na vichwa vya vikubwa vyenye sharubu. Lakini pia minofu ya kambare ina miiba midogo midogo mingi tofauti ya Kitoga. Wengine husema pia kambare ana shombo! Vinginevyo wote ni samaki wa tamu ingawa mimi napenda zaidi Kitoga. Pichani darajani Ruvu Kambare na Kitoga wakiwa sokoni.

Demographic Dynamics in Tanzania


-Rural areas currently house 75% of Tanzania's population
-Over the next 40 years, Tanzania's urban population is projected to grow rapidly(at 3.5% per year), from 11 million in 2010 tp 46 million in 2050.
-In contrast, the rural population will grow at only about 0.5% per year.
-By 2050, a majority of Tanzanians will live in urban areas.
Pichani Prof. Steven Haggblade kutoka Marekani akitoa uchambuzi kwenye warsha ya wadau wa mradi wa iAGRI tarehe 17/10/2011 kwenye ukumbi wa Hilux mjini Morogoro.

Analysis of Food Systems Dynamics in Tanzania




-Tanzania's food consumption patterns will change dramatically over the coming decades.
-Rising urbanisation and growing percapita incomes will double the marketed volumes of foodstuffs every 12 to 14 years and ramp up demand for high-value foods.
-As an increasingly commercial agriculture develops to meet this growing market demand, farm input demand for improved seeds, fertilizer, herbicides, feeds and veterinary services will expand rapidly.
Fueling the necessary productivity increases in this growing and modernizing food system will require a steady flow of trained scientific and technical skills in support of farm production, feed industries, storage, supply chain management and food-processing industries. Public investments and regulatory structures will also be needed to support innovation and agribusiness growth.

Tulikuwepo, tulisikia na sasa tufanyie kazi. Hii ndiyo hali halisi ya mtazamo wa upatikanaji wa chakula nchini Tanzania kwa miaka 10 mpaka hamsini ijayo.

Milima ya Uluguru

Milima ya Uluguru inapendeza.Ndiyo.Milima ya Uluguru kuna vyanzo vingi vya mali ya asiliikiwemo misitu, vyanzo vya maji na madini pia. Tatizo ni kwamba bado hatujakuwa makini kwa kuwa na programu zitakazoleta tija kwa sekta nilizozitaja. Hivi sasa mji wa Morogoro una matatizo ya maji, hivi sasa si rahisi kupata mbao nzuri kutoka Morogoro.Misitu imefyekwa!Sote tuamke tuanze kuandaa programu endelevu za milima ya Uluguru.

Tuesday, October 18, 2011

Haya ndiyo tuliyoyaona




Leo wakati tukirudi Dar Es Salaam tukitoka Moro haya ndiyo tuliyoyaona kuhusu kilimo.Hivi vinapatikana Ruvu darajani na hulimwa katika bonde la mto Ruvu. Banzi wa Moro alinunua karoti,bilinganya na pilipili hoho. Vijana hawa wasaidiwe ili waweze kuzalisha zaidi na kupata soko la mazao yao wameonyesha kukipenda na kuthamini kilimo.

Hapa ndipo tulipofikia

Moja ya noti chakavu ya Tshs 500 niliyoipata juzi. Noti hii imenyofolewa utepe unaong'ara. Eti wanasema utepe huo unakilevi ndiyo maana hunyofolewa na wanatumia kilevi hicho! Ikumbukwe kuwa noti hii ni moja ya aina mpya za noti zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania. Hivi kweli hapa ndipo Watanzania tulipofikia?

Geofrey Kirenga


Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Mazao Wizara ya Kilimo na Chakula na Ushirika alipata fursa ya kuzungumza baada ya kumaliza shughuli ya kuweka vipaumbele vya iAGRI.

Prof. Gillah akitoa closing remarks


Prof. Gillah alipata fursa ya kutoa closing remarks baada ya kazi ngumu ya kuandaa vipaumbele vya mradi wa iAGRI.

N je ya Ukumbi

Nje ya ukumbi baada ya miaka 31 nakutana na moja ya vichwa vya 'Tosamaganga High School' Peter Gillah. Sasa hivi ni Professor kwenye masuala ya misitu lakini pia ni Deputy Vice Chancellor-Academics wa Sokoine University of Agriculture. Tulikumbushana mambo mengi sana ya Tosa. Prof.Gillah ni yule yule mcheshi,wa kawaida kabisa lakini amebeba dhamana kubwa ya elimu katika nchi yetu ya Tanzania. Hongera sana Gillah. Mimi najivunia sana matunda ya Tosa.Furaha iliyoje kukutana tena!

Neno kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.

Washiriki kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika katika uzinduzi wa Mradi wa iAGRI waliongozwa na Dr. Fidelis Myaka (Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo)kwa niaba ya Katibu Mkuu. Pichani Dr.Myaka akitoa ujumbe wa Wizara.

Mradi wa iagri wazinduliwa

Mradi wa Miaka mitano wa 'Innovative Agricultural Research Initiative' (iAGRI)wenye lengo la kuanzisha program ya ushirikiano katika utafiti wa Kilimo kati ya Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) na Taasisi za Utafiti wa Kilimo nchini, kutoa mafunzo ya fani ya kilimo ngazi ya shahada uzamili(MSc) na uzamivu (PhD), kujenga uweza wa SUA katika kutoa huduma za mafunzo pamoja na kukuza uhusiano kati ya SUA na Vyuo Vikuu vya Amerika ya Kaskazini (USA) na Vyuo Vikuu vilivyo kusini ya Dunia umezinduliwa rasmi jana tarehe 17/10/2011 mjini Morogoro kwa kupitisha vipaumbele vya utafiti na mafunzo kwa kuwashirikisha wawakilishi wa wadau wa Kilimo hapa nchini na mfadhili wa mradi huo USA.Makao Makuu ya Mradi yatakuwa mjini Morogoro pale SUA. Pichani Mkurugenzi wa Mradi Prof. David Kraybill akitoa mada.

Saturday, October 15, 2011

Wanaimba tenzi


Wanafunzi wa Bright Angels Secondary School wamejaliwa vipaji mbalimbali. Hapa wanaonekana wakiimba tenzi wakati wa mahafali ya kidato cha Nne Jumuiya ya Wakristu chuoni hapo.

Na huyu ndiye mwenyeji wetu

Tulipata bahati ya kumtembelea mgeni katika familia yetu. Shem Maria Mbawala amejifungua mtoto wa Kike (aliyepakatwa)

Nipo na shems!

Wote shemeji zangu kasoro huyo mwenye blauz ya pinc ni mtoto wa shemeji mkubwa na mtoto wake. Raha iliyoje kuzungukwa na shemeji (Hapo mke wangu yupo!)

Tajiri wa shemeji


Na hawa ni mashemeji zanngu Wangoni tulipokutana nyumbani kwa Shemeji Maria Mbawala (mwenye gauni rangi ya blue wapili kutoka kulia ni shemeji mkubwa) kumpongeza kwa kujifungua salama mtoto wa kike. Hongera sana shem Mary na dogo Kassim !

Thursday, October 13, 2011

Na hapa ndipo Mkata



Hata kama utakuwa umesinzia.Ukizunduka na kuona kijiji chenye nyama ya mbuzi kama hivi katika barabara ya Segera Chalinze ujue upo Mkata.

Ni wakati wa kununua vigoda


Tulipokuwa tukirudi DAR, wajumbe walipata fursa ya kununua vigoda. Bei ni maelewano lakini vikubwa ni Tshs 4,000/=.(Angalizo uwe mwangalifu na aina ya mti havikawii kupekechwa na wadudu!)

Tunajiandaa kurudi Dar


Wajumbe tulisafiri kwa Bus. Hapa baadhi yetu tulipata fursa ya kupiga picha ya kumbukumbu mbele ya Nyumbani Hotel.Mwenye vazi la pink ni dada Julietha Madenge wa Kilimo Makao Makuu Dar Es Salaam.

Huduma za nyumbani Hotel


Unapokuwa Nyumbani Hotel unahudumiwa na warembo watanashati!

Wajumbe wa BWKCU




Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika. Juu kabisa ni Patrick Ngwediagi (PBR) (kushoto) na Karim Mtambo (Ag.DNFS) (kulia). Inayofuata ni Bw. Semroki (CIA) ya chini yake ni Dr. Fidelis Myaka (DRD) na Bw. Geofrey Kirenga (DCD).Chini kabisa mwenye shati nyeupe ni Bw. Pyuza (Principal - KATC)

Lasaka Chica


Huu ni ukumbi maarufu wa Starehe Jijini Tanga unapatikana barabara ya kwenda Bombo Hospital karibu kabisa na Hotel mpya ya Nyumbani (Nyumbani Hotel).

Ninapopewa nafasi

Wakati mwingine napewa nafasi ya kutoa mada pia. Hapa ilikuwa katika ukumbi wa Nyumbani Hotels jijini Tanga nikitoa mada ya mahusiano kazini kwenye Baraza la Wafanyakazi, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika mwezi Septemba 2011.

Tuesday, October 11, 2011

Mibavu na Sultani

Mibavu Gungu na Sultani Athumani kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wakijadiliana jambo wakiwa kazini Morogoro hivi karibuni. Nani ni bosi kati yao?

Dar Es Salaam usiku

Hapa ni kwenye keepleft ya Uhuru na Msimbazi - Kariakoo wakati wa usiku. Ukiwa hapa unaweza kuunga safari zako kwenda popote jijini Dar Es Salaam hata kama ni saa sita usiku. Pochi yako tu

Jamani Morogoro!

Hapa ni maeneo ya Mwidu mkoani Morogoro kabla hujafika mizani ya mikese angalia milima ya Uluguru, check gari inavyokata ikishuka kwenye kona kali. kweli Moro ya pendeza.

Kumbukumbu ya mahafali ya Belo

Prosper Belo a.k.a Sabuni amekuwa mdau mkubwa wa blog hii. Mara kwa mara amekuwa akitoa maoni yake na hasa ninapomchokoza kwa mambo ya Yanga. Ni mnazi mkubwa wa Yanga. Belo ni mtaalamu wa IT alihitimu mwaka 2009 huko Arusha.Zaidi ya yote Belo ni shemeji yangu nimemuolea dada yake. Hivi sasa yuko pale Airport katika kampuni moja akicheck systems. Katika kupekua maktaba yangu nilikutana na picha hii. Kushoto ni mama mzazi wa Belo-Mama Mapunda na kulia ni shemeji yangu Mwamgeni alienda kumpongeza kaka yake Belo kwa kuhitimu masomo yake ya IT wakati ule akiwa Arusha sasa yuko Zanzibar kwenye mafunzo ya utalii na huduma za hotel.

Nikuulize Belo kwanini joho lenu lilikuwa na rangi nyeusi na zambarau? Na kwanini majoho mengi asilimia kubwa ya rangi ni nyeusi? Na kwanini hizo kamba zinazoning'inia kwenye kofia ya kisomi zimelalia mkono wa kushoto na zina maana gani? Wasomi mliovikwa majoho nipatieni majibu.

Watafiti waandamizi


Kutoka kushoto kwenda kulia Mary Lutkamu (Mkurugenzi Msaidizi Utafiti-Special Programme), Dr.Mary Shetto (Afisa Utafiti Kilimo Mkuu),Eva Kanyeka (Afisa Utafiti Kilimo Mkuu)baadhi ya wataalamu watafiti waliopo Makao Makuu ya Idara ya Utafiti na Maendeleo, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wakiandaa taarifa kwa pamoja ofisini kwa Mkurugenzi leo asubuhi. Nami nilishiriki kwenye jopo hilo la wataalamu. Ilituchukua takribani masaa 4 kuweka sawa taarifa ya awali ya mafanikio ya utafiti miaka 50 ya UHURU.Hatukwenda Hotelini hivyo ilibidi tupate chai humo humo ofisini huku kazi ikiendelea. Katika mazingira haya bajeti ya vitafunwa ni muhimu! Bi Rose Angelo msaidizi wa Ofisi alituhudumia.

Byamungu amefurahi

Mkurugemzi wa Utafiti kanda ya Magharibi Bw. Deusdedit Byamungu amefurahia jambo. Hii ilikuwa ni kwenye Kikao cha Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kilichofanyika jijini Tanga mwezi wa Septemba, 2011 Nyumbani Hotels.

Wahitimu wasichana Kisemvule

Pichani wahitimu wasichana wa darasa la saba wa shule ya Msingi Kisemvule, wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. Katikati ni binti yangu Catherine Banzi amenihakikishia kuwa atashinda mtihani wa darasa la saba na kuendelea na masomo ya Sekondari. Alitakalo na liwe kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Siku ya mahafali ya darasa la saba Kisemvule

Wanafunzi walifurika kuwaaga wenzao wa darasa la saba waliwaimbia nyimbo na kucheza ngoma
Mama na dogo wanafurahia binti yao kuhitimu elimu ya msingi na hivyo kumzawadia zawadi kemkem.

Monday, October 10, 2011

Unapoipenda familia

Hata kama unaishi Kisemvule, penda familia yako. Pichani rafiki yangu Hazbon Marara a.k.a Makishe wa Kisemvule akiwa na familia yake nyumbani kwetu Kisemvule.

Mandhari ya SUA

Kama nisngeweka kichwa cha habari hii. Ni wachache wangeshinda swali la hapa ni wapi. Hapa ni mbele ya jengo la Utawala Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine.

Jengo la Utawala-SUA

Na hili ndilo jengo la Utawala- Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine (SUA) kilichopo Morogoro.