Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Mh.Joseph Simbakalia alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo - Naliendele, Mtwara alikuwa na hitimisho hili:-
1)Bado kilimo ni msingi wa maendeleo na kwa Mtwara upatikanaji wa gesi asilia (na huenda mafuta) kutasababisha wageni kuingia kwa wingi na hivyo mahitaji ya chakula yataongezeka. Mkoa unatakiwa kujipanga kukabiliana na changamoto hii, na kituo cha Utafiti kinaweza kutoa mchango mkubwa wa namna ya kuongeza chakula kutokana na majukumu yake.
2)Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele ambacho ni cha daraja la kwanza duniani (first class worldwide) katika utafiti wa zao la korosho. Hata hivyo, bado kilimo cha zao hilo hakijafikia hatua au kiwango ambacho taifa lingependa kuona. Bado kuna matatizo katika uzalishaji wa zao hilo ambayo hatuna majibu aidha kama wataalamu au kama serikali.
Mkuu wa Mkoa anapochukua fursa ya siku nzima kuona shughuli za watafiti na kuzungumza nao, unapita picha ya jinsi gani anavyotoa kipaumbele kwa masuala ya teknolojia katika maendeleo ya nchi.
No comments:
Post a Comment