Friday, December 30, 2011

Nawatakia kila la Kheri mwaka mpya 2012


Leo Ijumaa ni siku yangu ya mwisho ya kazi hapa ofisini kwa mwaka huu wa 2011. Mwaka huu umekuwa na milima na mabonde katika maisha yangu. Kuna wakati nililia sana hasa mwezi huu wa 12 na kuna wakati nilifurahi sana.Mwaka 2011 nimeshughulika na kusafiri sana kwa shughuli za kikazi. Sikukosa katika masuala ya jamii katika familia yangu kwenye kikundi chetu cha Africana pia nilikuwa kwenye mstari wa mbele kushiriki katika masuala ya dini hasa katika Parokia yangu ya Vikindu.Hata hivyo kuhusu blog ni mwaka wa mafanikio. Nimeweza kuvunja rekodi ya miaka iliyopita nimening'iniza 476!. Mwezi ambao sikufanya vizuri ulikuwa ni mwezi Septemba. Nawashukuru wadau wote wa Banzi wa Moro. Kupitia blog hii watu wamefahamiana, wameshauriana na kupata vitu vipya.NAWATAKIA MWAKA MPYA WENYE MAFANIKIO

Bwana mdogo na shemeji

Hapa ilikuwa ni Segerea. Bw na Bibi Joseph Kamsopi Mdimi wakitabasamu kwa furaha. Nakupeni shavu hasa kwa hiyo sare yenu kama vile mmefunga ndoa jana! Safi sana nawatakia mwaka mpya wenye mafanikio.

Wednesday, December 28, 2011

Wasifu wa Bibi Anastazia Hugo Chuma

Kuzaliwa: 18 Julai, 1919
Kufariki: 19 Desemba, 2011

Bibi Annastasia Hugo Chuma alizaliwa tarehe 18 Julai, 1919 Matombo, Morogoro.
Katika uhai wake, Bibi Annastasia Chuma Hugo hakuwahi kupata malezi ya moja kwa moja ya mama yake mzazi, bali alilelewa kwa upendo na Baba yake mkubwa, Mzee Clemence Pius Boko.
Bibi Chuma alipata bahati ya kusoma elimu ya msingi hadi ngazi ya Standard IV (akiwa ni miongoni mwa waasisi wa Shule ya Msingi ya Matombo).
Bibi Annastasia Chuma Hugo alibahatika kufunga ndoa na Mwl. Paul Lugonzo na kubahatika kupata naye watoto 7 kati ya mwaka 1934 na mwaka 1954.
Watoto hao ni:
1. Sister Philomena Mluge
2. Dk. Gregory Mluge
3. Bibi Janeth Kaaya Kishongo
4. Bibi Beatrice Mhango
5. Frederick Mluge
6. Bibi Rosemary Mokiwa
7. Bibi Maria Dolores P. Mdimi
Kwa mipango ya Mungu Mume wa Marehemu, Mwl. Paul Lugonzo na watoto wanne kati ya saba (Sister Philomena Mluge, Bibi Janeth Kaaya Kishongo, Bibi Rosemary Mokiwa na Frederick Mluge) wamekwishatangulia mbele ya haki, Raha ya Milele uwape Ee Bwana, na Mwanga wa Milele uwaangazie, wapumzike kwa amani, Amina.
Kwa kuwa mumewe alikuwa ni Mwalimu, Marehemu Bibi Annastasia Chuma Hugo aliambatana na mumewe katika maeneo mbalimbali ya nchi alipowahi kufanya kazi mumewe, ikiwa ni pamoja na Bagamoyo na Singiza.
Bibi Annastasia Chuma Hugo pia alipata bahati ya kusafiri hadi nchi za ng’ambo kwa nyakati mbalimbali kwa matibabu ya macho na kutembelea watoto na wajukuu zake huko Uingereza na Saudi Arabia kati ya 1979 na 1985.
Annastasia Hugo Chuma alikuwa ni mcheshi na aliyependa kusimulia masuala mbalimbali ya historia, hasa zilizogusa maisha yake kwa karibu. Bibi Annastasia Chuma Hugo ana kumbukumbu za kutokewa “katika njozi” na mtu aliyemfananisha na mama yake, wakati huo akiwa na umri wa miaka mitatu, ambaye alimuasa kuwa na upendo na heshima kwa watu wote, na kumcha Mungu. Mambo yalikuwa nguzo kuu katika uhai wake wote wa jumla ya miaka 92 na miezi mitano, aliyojaliwa kuishi hapa duniani.
Afya ya Bibi Annastasia Chuma Hugo ilianza kudorora mwaka 2001 ambapo alianza kusumbuliwa na maradhi ya kichwa. Pamoja na kupatiwa matibabu, bado hali yake ya afya haikuweza kuimarika sana. Hali ya afya ya Bibi Annastasia Chuma Hugo iliendelea kudorora na hatimaye matatizo yake yalizidi na kumfanya ashindwe kutembea, akawa ni mtu wa kulala zaidi na aliyehitaji zaidi kusaidiwa kwa karibu kila kitu.
Hali ya Bibi Annastsia Chuma Hugo ilibadilika zaidi katika wiki ya pili ya mwezi Desemba ambapo kula kwake kulikuwa kwa tabu. Aidha, alipumua kwa tabu.
Ilipofika tarehe 19 Desemba, 2011, bibi Annastasia Chuma Hugo alifariki dunia majira ya saa kumi alfajiri. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe. Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele Umwangazie, Apumzike kwa amani. Amina.
Bibi Annastasia Chuma Hugo ameacha watoto watatu (3), wajukuu kumi na saba (17) na vitukuu ishirini na mbili (22). Watoto wa Bibi Chuma(Dolores na Beatrice) pamoja na mjukuu wake (katikati) mwandishi wa wasifu huu Bw. Frank Shaniel Mdimi

Tuesday, December 27, 2011

Embe dodo-zawadi kutoka Matombo

Zawadi kutoka Matombo ni embe dodo. Nilizinunua maeneo ya Kimboza baada ya kupita njia panda ya Kinole.Embe moja Tshs 200/=.Embe nzuri zilizoivia mtini ni tamu kwelikweli!

Familia ilikutana

Frank Mdimi na mama zake (kushoto Dolores, kulia Beatrice Mhango)
Emma Kishongo na mama zake- Kushoto Dolores Mdimi na kulia Beatrice Mhango. Baada ya mazishi ya Bibi Chuma

Kanisa la Matombo

Mwili wa Bibi Chuma ulipowasili kwenye Kanisa la Matombo


Hili ndilo jengo la Kanisa Katoliki Parokia ya Matombo- Jimbo la Morogoro. Lina zaidi ya miaka 110.Banzi wa Moro amebatizwa, kupata komunio pamoja na Kipaimara ndani ya Kanisa hili katika vipindi tofauti.

Wakati mwingine gari iliserereka


Tulipokuwa Matombo Morogoro mvua kubwa ilinyesha na wakati mwingine magari yaliserereka na kuacha barabara kutokana na utelezi.

Mazishi ya Bibi Anastazia Hugo

Kuweka mashada ya maua juu ya kaburi kabla ya kumalizia kujengea kaburi na kuweka mfuniko
Waombolezaji makaburini
Padri anafukizia ubani kwenye ibada ya makaburini

Mwili wa Bibi Chuma ndani ya kaburi



Kuelekea makaburini
Mwili wa Bibi Chuma ndani ya Kanisa la Mtakatifu Paul Matombo Morogoro tayari kwa misa takatifu
Mwili wa Bibi Chuma unawasili nyumbani kwake Kiswira,Matombo Morogoro
Dr Gregory Mluge (kulia) mbele ya jeneza la mama yake

Mwili wa Bibi Chuma ukiwa nyumbani Makuburi-Dar Es Salaam

Tuesday, December 20, 2011

Apumzike kwa Amani Bibi Anastazia Hugo (Bibi Chuma)

Alfajiri ya tarehe 19/12/2011. Bibi yetu mpendwa- Anastazia Hugo (Bibi Chuma) alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 92. Maandalizi ya mazishi yanafanyika nyumbani kwa Bw. na Bibi Mangengesa Mdimi wa Makuburi-Dar Es Salaam. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda kijijini Kiswira-Matombo, Morogoro, asubuhi Jumatano tarehe 21/12/2011 na mazishi yatafanyika tarehe 22/12/2011 siku ya Alhamisi. Banzi wa Moro atakuwa kwenye msafara huo. Amina.

Friday, December 16, 2011

Chodo anapounguza chips

Katika harakati zake Chodo anaunguza chips hivyo kuleta taharuki watu wakizana nyumba inaungua!

Thursday, December 15, 2011

Hana mpango wa ndoa huyo

Hizi ni alama zinazoonyesha kuwa umtegemeaye hana mpango wa kukuoa achana naye!

You Have Been Reduced to Begging: For the woman who has been doing some serious hinting about getting married; it is often very hard to realize that conversations about marriage have been replaced with begging and pleading. If you have been reduced to begging, it is time to move on. Not only does he not plan on marrying you, but the type of guy who strings a woman along like this is likely to move on to more complex stalling tactics that can drag on for years without ever tying a not.

An Engagement with No Date Set: Many guys find that presenting a woman with a diamond ring is a great stalling technique. The men that have the financial means, can often get years worth of stall time with a large enough diamond. If you've been engaged for more than a few months and you still don't have a date set, then the odds of you walking down the aisle with this man are extremely slim. The same goes for dates set two or more years into the future.

Waiting for the right Time to Get Married:It sounds very responsible for your guy to say that he will ask you to marry him as soon as it is "the right time," but this is usually another stalling tactic. People manage to tie the knot during less than perfect circumstances all the time, so why can't he?

All of His Exes Are "Crazy":
Be wary of a man who refers to his former girlfriends as crazy, pyscho, or clingy-because what's the common denominator here? Him, he never really wanted the relationship to work in the first place and probably has commitment issues.

He's hot and cold on the phone:
He'll: text you 10 times in a night, then go MIA for days. He'll chat on the phone for an hour, and then ignore your messages for the rest of the week. Wondering what the hell is going on? We're going to be brutally honest:He's mostly likely busy dating other women.

Stuff is missing from his face book profile:has he untagged any photos of you and him? Does he post updates often, yet never mention hanging out with you? Is this relationship status hidden? We smell a rat. A guy who's leery of commitment will make sure there are no traces of you on his page.

He hasn't asked you (no explanation needed):

(Kutoka gazeti la DailyNews 15/12/2011 uk.8)

Ubinafsi unapojengewa hoja

Sometimes you have to put yourself first and make your needs known.....Closed mouths don't get fed and if you can't speak up and express your desires........

Hivi ndivyo mwandishi mmoja alivyokuwa akijaribu kujengea hoja ubinafsi (Soma dailynews 15/12/2011-pg5 woman magazine)

Mama 'Great Lakes'

Balozi Liberata Mulamula ni mmoja kati ya viongozi wanawake mahiri tuliobahatika kuwa nao nchini Tanzania. Kwa bahati nzuri nilihudhuria reception yaharusi yake na Bw. George Mulamula pale Silversands Hotel Dar Es Salaam kama sikosei mwaka 1985 (sikumbuki sawasawa).Ni moja kati ya reception bomba nilzowahi kuhudhuria katika maisha yangu.
Kwa uchapaji kazi wake akiwa Katibu Mtendaji wa 'International Conference on the Great Lakes Region' (ICGLR). Liberata anajulikana kama 'Mama Great Lakes'

Je huu ndiyo mwisho wa Torres?


Chelsea inatarajia kumuuza Torres kwa kitita cha pound 20 milioni ifikapo Januari mwakani. Tangu aliponunuliwa na Chelsea kutoka Liverpool,mchezaji huyo aliyekuwa tishio wa kupachika magoli akiwa Liverpool, ameifungia Chelsea mabao matatu tu kwenye ligi Kuu ya Barclays ya Uingereza.

Chodo na zoezi la hesabu


Hivi ndivyo hesabu zinavyosumbua watoto wetu si kwa Chodo tu!

Tuesday, December 13, 2011

Azam ilivyojipanga miaka 50 ya uhuru

Sehemu ya mapokezi na bidhaa zipo!
Watoto waliliminika kwenye banda la Azam kupata vinywaji baridi, cake na biscuits



Thursday, December 8, 2011

Ukulima wa kisasa-Toleo la Uhuru


Hili ndilo lilokuwa toleo la Uhuru gazeti la Ukulima wa Kisasa mwaka 1961. Waziri wa Kilimo alikuwa Mh. Paul Bomani

Mkurugenzi Mstaafu bandani


Mkurugenzi Msaidizi wa Mifumo ya Kilimo na Uchumi Jamii Bw. Timothy Kirway (mwenye shati jeusi)pamoja na watoto wake walitembelea banda la Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika mchana wa leo. Anaipenda sana Wizara yake.

Mgani Mwandamizi na Mwenyekiti wa Ilolo


Furaha iliyoje kukutana na Mwenyekiti wangu! Ndivyo anavyosema Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Wakulima Bw. Nyangi alipokutana na Mwenyekiti wake wa Wilaya ya Ilolo kwenye banda la Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.

Watafiti wakilimo waandamizi bandani


Watafiti waandamizi wakijadiliana jambo kwa lengo la kuboresha maonyesho.Kutoka kushoto Dr. Huseein Mansoor (Mkurugenzi Msaidizi -Utafiti wa mazao), Bw. Ninatubu Lema (Mkurugenzi Msaidizi-Mifumo ya Kilimo na Uchumi Jamii) na DR. Janet Kaaya (Mkuu wa Kitengo cha Habari na Utunzaji Nyaraka-Utafiti).

Miwa-Utafiti hadi Sukari




Hapa unapata mtiririko kamili wa uzalishaji wa sukari kuanzia utafiti wa miwa hadi sukari. Sukari inauzwa pia bandani kilo moja Tshs 1900/= wahi sasa!

Kahawa au Chai


Ukifika kwenyen banda la kilimo unaulizwa unataka kahawa au chai? Ndiyo, kwenye banda hilo unapata maelezo kamili ya uzalishaji na usindikaji wa kahawa au chai. Lakini ukitaka kupata kikombe cha kahawa au chai ruhusa masaa 12!

Hawa ndiyo 'queleaquelea'


Queleaquelea ni ndege waharibifu wa mazao wanapokuwa wengi na kuvamia shamba lenye mimea hasa nafaka.Ndege hawa kwetu Morogoro wanajulikana kama 'Nguya' sisi huwa tunawakamata kwa kuwatega au kuwapiga na manati kisha tunawala ni watamu. Ni kuku wadogo tu! Lakini kwetu sisi wataalamu ni ndege hatari huwa tunatumia raslimali nyingi kuwadhibiti. Fika kwenye banda la Kilimo uwaone ndege hawa 'live'

Maembe mazuri


Kwenye banda la Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wageni hupata fursa ya kujionea aina mbalimbali za mazao yakiwemo maembe

Matunda ya MATI-Ukiriguru



Leo nikiwa katika banda la Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika napata fursa ya kukutana na wataalamu wenzangu tuliosoma pale Chuoni Ukiriguru mwaka 1981-1983.Picha ya juu Bw. Alex Semgalawe sasa mtaalamu wa matunda yupo Mpiji na picha ya chini ni Bi.Joan Kasuga mtaalamu wa utafiti mbegu za mafuta.Safi sana mates!