Monday, August 27, 2012

Na ngongoti je?

Huu nao ni utamaduni wetu wa kuvutia

Hakika usingeacha kununua

Nanenane 2012 viwanja vya Temi Arusha

Niko na mtafiti mkuu Bw. Kheri Kitenge kwenye eneo la banda la Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.
Kutoka kushoto Antipassy Bwakila (ARI-Selian, Arusha) na John Banzi (MAFC - HQ DSM)
Masista wakipata maelezo ya kitaalamu katika kilimo

Miatano! Miatano!

Kama kawaida mitumba na biashara ndogondogo hazikukusekana kwenye maonyesho ya aina yoyote hapa Tanzani. Ndivyo ilivyokuwa kwenye maonyeshio ya Nanenane 2012 viwanja vya Temi Arusha. Sauti za miatano, oh miatano! Miatano. Mpende mwanao! Za reoreo! buku!buku! Zilisikika kwenye vipaaza sauti vyao ambavyo vilikuwa ni burudani ya aina yake hata kama hukubahatika kununua chochote.

Kuna wabunifu

Tembelea maonyesho ya wakulima, hukosi kuwakuta wakulima wabunifu. Kwenye maonyesho ya Nanenane ya mwaka 2012 kanda ya kaskazini kwenye viwanja vya Temi walijitokeza wakulima wengi kuonyesha ubinifu wao katika teknolojia mbalimbali zenye lengo la kuongeza uzalishaji kwenye kilimo. Kuna waliobuni virusha maji 'sprinklers' na kuna waliobuni aina za mbolea
Mbunifu wa virusha maji 'sprinklers' kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga. Tukiwaendeleza kwa kuwawezesha wabunifu hawa tutasonga mbele katika kubuni teknolojia rahisi kwa wakulima.

Unaweza kumwagilia mazao kwa kutumia trekta

Kutoka banda la JKT- Oljoro

Ukiwa ndani ya banda la JKT Oljoro kwenye viwanja vya Temi Arusha. Mandhari wakati wa maonyesho ya Nanenane yalikuwa kama hivi.

Sunday, August 26, 2012

Africana Group kikao cha 7

Matukio ya kikao cha 7 cha Africana Group kilichofanyika nyumbani kwa dada Ghana Kunambi Ilala Flats-Dar Es Salaam
Wanakikundi wakipitia kumbukumbu za kikao cha sita
Kabla ya kikao kuanza wengine walipata fursa ya kusoma magazeti
Mwenyeji Dada Ghana akisubiri wageni
Baada ya kikao vinywaji ruksa!
Na hatimaye tulirejea makwetu. KIKAO KIJACHO CHA AFRICANA KITAFANYIKA KIJIJINI KISEMVULE KWA INNO BANZI TAREHE 30/9/2012 JUMAPILI SAA 6.00 KARIBUNI NA WAELEZE WANAKIKUNDI WENGINE. SIKU HIYO KUTAGAWIWA T-SHIRT ZA AFRICANA KWA WALE WALIOLIPIA NA PIA USIKOSE KUJA NA FEDHA ZA KUNUNUA SHARE ZA KIKUNDI.KWA WALE AMBAO WAKO NJE YA DAR WANAWEZA KUWASILIANA KWA E-MAIL AU SIMU.

Mafunzo ya mnyororo wa thamani-Morogoro

Watafiti wakiwa kwenye mafunzo ya mnyororo wa thamani (Value chain)

Saturday, August 25, 2012

Mafunzo shirikishi

Mtafiti Kisa Mwaisoba kutoka kituo cha Utafiti Uyole akiwasilisha kazi ya kikundi kwenye mafunzo ya mnyororo wa thamani yaliyofanyika mjini Morogoro mwezi Agosti 2012.

Mtaalamu wa mnyororo wa thamani

Mmoja wa wataalamu wachache mahiri wa mnyororo wa thamani hapa nchini Dkt Khalmadin Mutabazi (mwenye vazi nyeusi) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine kilichopo mjini Morogoro akitoa mada kwa wadau hivi karibuni

Mnyororo wa thamani wa mpunga-Wadau

Hivi karibuni, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika uliendesha mafunzo ya muda mfupi kuhusu mnyororo wa thamani wa zao la mpunga yaliyofanyika mjini Morogoro. Pichani na baadhi ya wadau walioshiriki mafunzo hayo.

Heshima ya mgeni kusindikizwa

Moja ya sifa kubwa ya Watanzania ni kupendana. Baada ya kusheherekea vizuri sikukuu ya Iddi 2012 nyumbani kwa Bw. Mkude Mbezi-Kibanda cha mkaa- Dar, tulisindikizwa kurejea kwetu Kisemvule, Vikindu, Mkuranga mkoa wa Pwani muda wa saa 11.30 jioni

Picha ya pamoja Eid Elftri 2012-Mbezi

Hii ndiyo picha ya pamoja ya kumbukumbu ya Sikukuu ya Eid Elfitri 2012 nyumbani kwa Bw na Bibi L.Mkude-Mbezi Kibanda cha mkaa jijini Dar Es Salaam

Wazee je?

Tulifarijika sana kwa mara nyingine tena kuwa pamoja. Kutoka kushoto Bi Zamwata Kasiba (mdogo wake Bi. Sango), Mr Mkude, Mr. Banzi na Nancy Banzi

Picha ya ukumbuso wa Iddi 2012-Watoto

Hii ni picha ya pamoja ya ukumbusho wa sherehe za Iddi nyumbani kwa Bw na Bibi Mkude. Angalia 'characters'!

Na baadaye michezoni

Ninahakiki

Kama kuna mtu aliyefurahia sikukuu ya Iddi nyumbani kwa Mzee Mkude basi mtoto Hemedi. Alikuwa kwenye kila Idara. Hapa anahakikisha kama msosi upo au umekiwsha!

Utamu wa tikitimaji

Baada ya msosi mtoto John alijirusha na tikiti maji

Naomba nyama

Baada ya kushioba ilikuwa ni kutaniana

Utamu wa soda uinywe kwa mikono miwili!

Ndivyo ilivyo kwa mtoto Hemedi a.k.a Mzee Kasiba wakati aliposheherekea sikukuu ya Iddi El Fitri nyumbani kwa baba yake mkubwa Mzee Mkude wa Mbezi- Kibanda cha mkaa jijini Dar.

Mgeni hafaidi mpaka siku ya Iddi

Familia ya Bw na Bi Mkude wa Mbezi-Kibanda cha mkaa iliwaalika wageni mashuhuri nyumbani kwao kusherehekea kwa pamoja sikuukuu ya Iddi El Fitri. Na hivi ndivyo ilivyokuwa.
usinichekeshe baba Sisti! Ndivyo anavosema shem Zai wakati Banzi wa Moro akichukua akipata picha hii.
Sisti na Sheikh Msafiri (The pilot) walikaa chobingo!
Wakati Sisti anapata msosi. Mwahija alibakia kutafakari!