Monday, August 27, 2012

Kuna wabunifu

Tembelea maonyesho ya wakulima, hukosi kuwakuta wakulima wabunifu. Kwenye maonyesho ya Nanenane ya mwaka 2012 kanda ya kaskazini kwenye viwanja vya Temi walijitokeza wakulima wengi kuonyesha ubinifu wao katika teknolojia mbalimbali zenye lengo la kuongeza uzalishaji kwenye kilimo. Kuna waliobuni virusha maji 'sprinklers' na kuna waliobuni aina za mbolea
Mbunifu wa virusha maji 'sprinklers' kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga. Tukiwaendeleza kwa kuwawezesha wabunifu hawa tutasonga mbele katika kubuni teknolojia rahisi kwa wakulima.

No comments: