Thursday, August 28, 2014

Zamoyoni Mogella -Tunda la Moro

Asubuhi ya leo nakutana na Zamoyoni Mogella 'Golden Boy' katika pilika za kutafuta riziki. Mogella yuleyule, mchangamfu na mwenye nidhamu. Tunasalimiana na kuongea naye kwa dakika chache na bila kuchelewa namuelekeza anakotaka kwenda. Nidhamu yake, uchangamfu wake,utafutaji na malengo yake unamfanya Mogella kuwa 'Golden Boy'  hadi sasa'
Zamoyoni Mogella'Golden Boy' enzi zake akichanja mbuga

Zamoyoni Mogella akiwaasa wachezaji wa Simba hivi karibuni

Zamoyoni Mogella katika misele jijini Dar

Zamoyoni Mogella akiwa na timu ya Taifa

Zamoyoni Mogella akiwa na mashabiki wa Simba akiangalia moja ya mechi ya timu hiyo uwanja wa taifa

Zamoyoni Mogella 'Golden Boy" alivyo sasa

Zamoyoni Mogella na Nico Njohole wote kutoka Moro

Mogella akimtoka Yusufu Bana wa Dar Young Africans

Zamoyoni Mogella na kocha mchezaji  Hassan Haffif  wakiwa Simba Sports Club

Zamoyoni Mogella akiwa na Ben Kinyaiadd caption

Tuesday, August 26, 2014

Norbert Banzi na mpira

Si rahisi kumtengenesha Norbert Macarios Banzi na mpira. Soka ni mchezo anaoupenda. Norbert hutumia mguu wa kushoto kupiga mpira. Huenda akawa mchezaji wa Taifa Stars na wa kulipwa pia.

Norbert Banzi na baba yake


Kila mtu na pozi lake

Pozi la uncle Loveness

Pozi la Dulla Pembe

Mama Cathy

Unapotembelewa na ndugu zako ni raha na baraka

Elizabeth George Banzi

Wajukuu- kutoka kushoto Love (mtoto wa Elizabeth) na Catherine mtoto wa Maureen

Maria Banzi na ndugu zake

Raha iliyoje kuwa nyumbani kwa babu Banzi!

Elizabeth Banzi na mtoto wake Love

Maureen  na mtoto wake (mtoto wa Marehemu dada Goreth Banzi)




Unapotembelewa na ndugu ni raha na Baraka. Jumapili ya tarehe 24/08/2014 nilitembelewa na mtoto na mpwa wangu (Elizabeth na Maureen) na watoto wao. Maureen mtoto wa dada yangu marehemu Goreth Banzi sijamuona kwa siku nyingi kwani anaishi Mbeya  kwa baba zake. Wote wana watoto. Watoto wote walikuwa wananiita Babu, babu, babu! Raha iliyoje?

Mboga salama-Kisemvule

Mboga za maboga salama kutoka Kisemvule. Havimwagiliwi kwa maji machafu ni kutoka katika chemichemi zinazobubujika kijijini Kisemvule, Wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani

Kikao cha Halmashauri ya Walei Parokia ya Vikindu


Tarehe 23/08/2014  Halmashauri ya Walei Parokia ya Vikindu ililikutana kuweza kupanga na kutathmini shughuli za Parokia. Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na Paroko wa Parokia hiyo Fr. Stephen walitaarifiwa kuwa Sikukuu wa Somo wa Parokia itafanyika tarehe 29/09/2014 siku ya Jumapili. Kipaimara ni tarehe 1/11/2014 siku ya Jumamosi

Hakika mazingira yanavutia


Kila nipitapo barabara hii ya Tandika kuelekea Mbagala huwa navutiwa na mazingira ya nyumba hii. Bustani ndogo ya maua inayotunzwa vizuri. Huhitaji maji mengi kumwagilia eneo hili la bustani. Ni kujipanga tu. Hivi wengine hawaoni kuwa panapendeza? Au mpaka hapo aishi mzungu ndipo muone kuna kitu cha kuigwa? Tubadilike.

Vijana kwenye maonesho ya Nanenane 2014 mkoani Lindi

Wakulima wa kesho wakipata taarifa za teknolojia za kilimo kwenye mabanda ya kilimo mkoani Lindi ambako Sikukuu ya Nanenane  2014 kwa mara ya kwanza ilifanyika kitaifa mkoani Lindi.

Viazi vya asili vilivyo na sumu

Maonyesho ya klilimo ya Nanenane  2014 nchini Tanzania yaliyofanyika kitaifa mkoani Lindi yalikuwa na manufaa makubwa kwa wananchi. Kwa mfano kwenye mabanda ya kilimo vilioneshwa viazi vya asili visivyo na sumu. Ni mara ngapi tumesikia kuwa baadhi ya watu wamefariki kutokana na kula mazao aina ya mizizi ambayo ni sumu. Hiyo haikuwa makusudi yao. Tatizo hawakuhabarishwa tofauti ya viazi vyenye sumu na visivyo na sumu.

Viazi vya asili

Viazi vya asili aina ya 'Mnyuvele' kwenye maonyesho ya kilimo maarufu kwa jina la Nanenane 2014 yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo -Lindi

Hivi Tanzania tumeshindwa kumuungamiza mbu!

Ni mdudu mdogo sana. Lakini anaonekana kwa macho. Bakteria  haonekani kwa macho,kirusi haonekani kwa macho lakini nguvu nyingi zinatumika kupambana nao. Huyu mdudu mbu anayeonekana kwa macho kwanini tumeshindwa kumuungamiza wakati anatuletea maafa makubwa? Si wengi ambao wanaogua ukimwi hapa nchini. Lakini ni nani asiyegua Malaria? Vifo vingi hapa nchini vinasababishwa na Malaria hasa vya watoto. Hivi kweli tumeshindwa kuwaangamiza mbu kwa kuboresha usafi? Tumeshindwa kuwaangamiza mbu kwa kuwaua na madawa? Vyandarua sawa, lakini ni nani anyetumia ipasavyo?Ni wangapi wenye uwezo wa kununua vyandarua?

Tukae chini tuanze upya na tuanze sasa kuangamiza mbu kwa nguvu zote, tutafanikiwa. Tusisubiri misaada ya kutoka nje inasaidia lakini haitotokomeza adui mbu. Hebu tujiulize hivi kweli kama mbu angekuwa tishio ulaya wangekaa kimya? Hata, Nguvu zote zingeelekezwa huko. Hili linaniumiza na imebidi niliandike.

Aflatoxin ni sumu

Niwakumbushe tu. Aflatoxin ni sumu na inashusha thamani ya mazao yetu hasa mahindi na karanga.

Mwaka wa familia tuige familia ya Joseph



 Familia ya Joseph Yesu na Maria ilipenda na kuthamini kazi. Tufanye kazi wakati wa kuadhimisha mwaka wa FAMILIA

Hakika 100% -Moro

Maji yatiririka kilimani-Moro
Mbuga za wanyama- Moro
Matunda kama vile ndizi na machungwa- Moro
Misitu na ndege wa kuvutia - Moro
Mpunga a.k.a ubwabwa kwa wingi-Moro
Soka safi-Moro
Muziki na starehe - Moro

Banzi wa Moro najivunia  kuwa asili yangu ni Moro. Morogoro naipenda!

Na mtoto Maria

Jamani hii ni ukumbusho wa Banzi na semeji yenu Nancy tukiwa na mtoto wetu Maria Banzi kwenye tafrija ya komunio ya akina Danielle.

Ah. Kumbe Mapenzi kama Treni ya Mwakyembe!


Ajali na riziki hapohapo

Lori hili la mafuta lilianguka Kimara hivi karibuni. Kwa kuwa llilikuwa limebeba mafuta ya kula, wananchi walihangaika kusomba mafuta hayo. Angalia umati unavyoshughulika, kila mmoja kwa nafasi na uwezo wake. Najiuliza, wateja wa mafuta haya ni akina nani? Kwa  vyovyote vile ni mama ntilie na familia za kipato cha chini. Hata hivyo kuna wengine huenda waliweka katika vifungashio vipya na kuuza madukani.Kwa hiyo inawezekana kabisa wengi wetu tumepata kutumia mafuta haya bila kufahamu. Kweli ajili na riziki hapohapo!

Tuesday, August 19, 2014

Gusa pindo - kibao cha Rose Mhando



    Watoto hawa wa Vikindu walionyesha show ya nguvu ya  pindo la Yesu  kibao kipya cha Rose Mhnado    wakati wa sherehe ya kuwapongeza maharusi waliofunga ndoa tarehe 02/08/2014 kanisani Vikindu Parokia ya Mt. Vinsenti wa Paulo na kisha kusherehekewa katika Jumuiya ya Mt. Inyasi nyumbani kwa Mama Kileo. Sherehe ilifana sana!

Wazazi na Binti

   Bw & Bi A. Mmore na binti yao mara baada ya kufunga ndoa tarehe 02/08/2014

Umahiri wa kucheza

    Kijana akionyesha umahiri wake wa kusakata muziki

Mwalimu na mwanafunzi

Mwanafunzi ni mtoto wa Bibi na Bw. A.Mmore. Mwalimu wa mwanafunzi  ni Mama Banzi msimamizi wa harusi ya wazazi wa mwanafunzi bahati iliyoje? (Picha ya ukumbusho tarehe 2/08/2014 siku ya harusi ya Bw & Bi. Mmore

Wanameremeta


Bi  na Bw. Anthony Mmore  wa Vikindu sasa ni wanandoa. Ndoa ilifungwa tarehe 2/08/2014 katika kanisa katoliki ya Mt. Vinsenti wa Paulo-Vikindu na wasiamamizi ni Bw. na Bibi I.J.Banzi.Bahati iliyoje kwani nasi tulikuwa tunasheherekea miaka 17 ya ndoa yetu. Mungu na ashukuriwe sana.

Inakuwaje kwa mabibi harusi

Kabla ya ndoa kufungwa shera za mabibi harusi hufunika uso. Kwanini?