Wakulima wengi wa zao la mbaazi hapa nchini hupanda mbazi kwa kutumia mbegu walizonazo. Wnapanda kwa mazoea. Hata ukuwauliza aina ya mbegu hizo pamoja na sifa zake hawajui. Mara nyingi mbegu hizo ni mchanganyiko. Hali hii husababisha uzalishaji duni wa zao la mbaazi. Kituo cha utafiti wa Kilimo Selian kilichopo mkoani Arusha Kanda ya Kaskazini kimefanya utafiti wa muda mrefu wa kilimo cha mbaazi si kwa mbegu tu bali mazingira yanayotakiwa ya kustawisha mbaazi (udongo na hali ya hewa) pamoja na kufanya utafiti wa kichumi kuhusu kilimo cha mbaazi.
No comments:
Post a Comment