Friday, November 7, 2014

Ufaulu darasa la saba 2014 - Morogoro Vijijini hali ni tete




























 





NAFASI YA SHULE
  Matombo Gozo Kibangile Kibungo Juu
waliofanya mtihani 63 33 31 32
Kiwilaya (149) 70 39 55 80
Kimkoa (520) 483 305 410 547
Kitaifa(15867) 10577 6809 9094 11955
  3 1 2 4










Hebu angalia takwimu za ufaulu kwa baadhi ya shule za msingi maarufu Morogoro vijijini-Hali ni tete. Tukae na tuone jinsi ya kujikwamua kutoka kwenye hali hii. Mwaka wa jana pia hali ilikuwa si nzuri. Hata wanafunzi wanaofanya mtihani kwa darasa la saba ni wachache ukilinganisha na shule nyingine. Basi kwa uchache huo nilitegemea kuwa watoto wangefanya vizuri. Wanaweza wasifanye vizuri kwenye somo la kiingereza lakini hesabu Je?



















Queen wa Mzinga Shule ya Msingi apasua A tupu!

Mwanafunzi Queen Damian Mpangwa wa darasa la saba kutoka shule ya msingi Mzinga-Temeke Vijijini, Mkoa wa Dar Es Salaam anatisha! Amepasua  vibaya kwenye matokeo ya darasa la saba 2014. Hebu angalia matokeo yake.

Kiswahili -  A
English-      A
Maarifa -    A
Hisabati-    A
Science -   A
Wastani -  A

Hii ni shule ya  kawaida ya umma. Nimeambiwa na mwalimu wa shule hiyo kuwa mwanafunzi huyu anatoka familia ya kipato cha chini na anaishi na mama yake. HONGERA sana Queen  umezipaisha shule za umma.

Tusiime yaongoza tena STD VII-DAR 2014

Tusiime students (picha ya maktaba - mtandao)
Shule ya Tusiime iliyoko wilaya ya Ilala mkoa wa Dar Es Salaam  katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba Kitaifa 2014 imefanya hivi:-

 Wanafunzi waliofanya mtihani 168
 1st Wilaya ya Ilala- shule 101
1st Mkoa wa Dar Es Salaam- 506
8 Kitaifa- 1586

Kweli TUSIIME ni shidaaaaa!

KELVIN K.SIMKOKO-KICHWA CHA MARIAN BOYS SEC

Kelvin K.Simkoko  ametunukiwa tuzo ya kufanya vizuri katika taaluma Kidato cha 4 2014 shule ya Marian Boys'  Secondary. Hongera Kelvin ongoza hadi utakapopata PhD lakini pia usimsahau MUNGU aliyekuumba na kukupa kipaji hicho si kweli kuwa wengine hawataki kuwa vichwa MUNGU ndiye hupanga haya na kwa bidii yako pia.

Wednesday, November 5, 2014

Tupo kwenye Mauldi

Bi Laika Pembe wa Kisemvule akiwa na mjukuu wake wakisubiri Maulidi ya harusi.

Watu wa Pwani

Abdallah na shangazi yake



Shehe mdogo


Mahindi kutoka kwa watafiti wa Selian

Ni kweli zipo aina bora ya mbegu za mahindi zenye uwezo wa kuzaa mahindi mengi na bora. Kituo cha utafiti  wa Kilimo Selian kilichopo Arusha kwa muda mrefu kimekuwa kikitafiti aina bora za mbegu za mahindi zinazofaa mazingira ya wakulima wa Kanda ya Kaskazini hapa nchini moja ya mbegu zilizokwisha pendekezwa ni Selian H208 na Situka. Kwa maelezo zaidi wasiliana na kituo cha Utafiti Selian( Contact. Dr. Mafuru (ZD) -0756657316)

Vipeperushi vya kilimo cha mahindi na mbaazi

Vipeperushi hivi vimeandaliwa na kituo cha Utafiti wa Kilimo Selian, Arusha. Kinaelezea jinsi mkulima anavyoweza kulima mbaazi na mahindi (intercropping) kwa kurutubisha udongo, kuzalisha mazao kwa wingi hatimaye kuongeza kipato cha mkulima

Hizi ndizo aina bora za mbegu za mbaazi

Wakulima wengi wa zao la mbaazi hapa nchini hupanda mbazi kwa kutumia mbegu walizonazo. Wnapanda kwa mazoea. Hata ukuwauliza aina ya mbegu hizo pamoja na sifa zake hawajui. Mara nyingi mbegu hizo ni mchanganyiko. Hali hii husababisha uzalishaji duni wa zao la mbaazi. Kituo cha utafiti wa Kilimo Selian kilichopo mkoani Arusha Kanda ya Kaskazini kimefanya utafiti wa muda mrefu wa kilimo cha mbaazi si kwa mbegu tu bali mazingira yanayotakiwa ya kustawisha mbaazi (udongo na hali ya hewa) pamoja na kufanya utafiti wa kichumi kuhusu kilimo cha mbaazi.

Waliopata Sakramenti ya Kipaimara Parokia ya Vikindu -2014

Wenye majoho meupe na 'vipelani' vyekundu ni baadhi ya vijana wa Parokia ya Vikindu waliopatga Sakaramenti ya Kipaimara tarehe 1/11/2014  Parokiani Vikindu (Mt. Vinsenti wa Paulo) Jimbo Kuu la Dar Es Salaam.

Askofu Nzigilwa na macandidate wa Vikindu

Baada ya Ibada ya Kipaimara Parokia ya Vikindu, Baba Askofu Eusebius Nzigilwa kwenye picha ya ukumbusho na 'macandidate' wa shirika la Kitawa la masista wa Mlima wa Camel.

Parokia ya Vikindu-watoto wa utatu wanamtumikia Mungu

Kumekuwa na mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa Litrujia katika Parokia ya Vikindu Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Kivutio kikubwa kimekuwa ni kwa Watoto wa Utatu Mtakatifu. Watoto hawa hucheza mbele ya Altare kwa misa zote mbili kwenye Ibada ya Dominika.

Wachache wamekosa ushungi

Nilisikia sauti ya sheh ikitamka"Mwanamke wa Kiislamu shurti  kujifunika kichwa" ni wachache waliokosa ushungi hapa!

Bibi harusi na kungwi wake

Kungwi wa bibi harusi hukaa karibu naye, ndivyo Banzi wa Moro alivyomkuta Bi harusi na Kungwi wake wakati wa sherehe ya harusi kijijini Kisemvule nyumbani kwa akina Nyaubuguyu.

'Dufu' kwenye sherehe ya ndoa

Kwa bahati nzuri naishi mkoa wa Pwani ambako takaribani asilimia 90 ni Waislamu. Miaka ya hivi karibuni nimeshuhudia harusi nyingi za Kiislamu zikifanyika na kuwa na kisomo cha Maulidi huku 'Dufu' ikisherehesha badala ya rusha roho. Ni kweli 'Dufu' hupigwa kwa staha kubwa na watu huifurahia.

Kabla ya Soda tulikuwa tunakunywa soda


Kabla ya kuingia kinywaji cha soda, wenyeji wengi wa pwani walikuwa wakitumia togwa kama kinywaji baridi. Je tumesahau. Pichani togwa ikiuzwa wakati wa sherehe iliyofanyika hivi karibuni kijijini Kisemvule.

Nkem Owoh-Msanii machachari wa Afrika



Kwa wenye mazoea ya kuangalia sinema za Kinegeria, sura hii si ngeni kwenu. Huyu ni Nkem Owoh a.k.a asokofia. Huyu ni mcheza sinema mashuhuri kutoka Nigeria. Amecheza sinema nyingi na kutunikiwa  zawadi nyingi nyingi nyingi. Cha kushangaza Nkem  kwa taaluma ni Mhandisi. Lakini umaarufu wake haukutokana na uhandisi bali ni kwa sanaa. Mimi na wewe pengine tunafanya kazi ambazo hazitupi umaarufu au kutuongezea kipato. Pengine siyo Mungu alichotuumbia tukifanye hapa duniani.

Msanii wangu-King Majuto

Ningeambiwa kumpigia kura msanii bora hapa nchini, kura yangu ingekwenda kwa comedian King Majuto!

Huyu ndiye Salma Jabir wa Kipindi cha Mkasi

Mwanadada Salma Jabir ni mmoja waandaaji wa vipindi vya TV wenye vipaji. Porgramu yake ya Mkasi kwa kweli inavutia sana. Nikuulize swali moja dada Salma. Mkasi ni kwa watu wa sanaa tu? Mkasi hauwezi kupita kwa wakulima au wanasayansi?