Ni kweli hivi karibuni nilikuwa pale Moro mjini, kikazi. Lazima niseme.
Kitu kilichonifurahisha ni jinsi MANISPAA inavyotunza ile mizunguko ya kupita KUSHOTO iliyopo barabarani pale mjini (KEEP LEFTS). Kwanza kuna mzunguko mkubwa kabisa pale MSAMVU, bustani ya maua ni safi na kijana yule anayehudumia pale kwa kweli anachapa kazi.Bustani ile inavutia.
Unakuja hapa MASIKA napo wawaaaa na kibao kimesimikwa USITUPE TAKATAKA na kweli hakuna TAKA.
Unashuka pale stendi ya zamani. Kwenye kituo cha Mabasi ya Kwenda MATOMBO bustani safiii. Kijani kibichi kabisaa na ukiangalia milimani nako maji yatiririka basi raha mpaka kisogoni. Sawa, ukienda Posta karibu na NBC bustani nzuri imetunzwa vizuri. Basi hiyo ndiyo mandhari ya Moro mji kasoro bahari na kiswahili chetu cha kuimba, Utatupenda! Jamani!
Angalizo kwa Uongozi wa Manispaa
- Kituo cha mabasi cha Msamvu inabidi kuboreshwa zaidi, wakati wa mvua na jua ni shida tupu.
- Soko kuu la mjini pale Kikundi linataka ubunifu zaidi. Watu wanaongezeka bidhaa zinaongezeka na mahitaji yanaongezeka.
- Barabara ya kwenda Kilakala Sekondari iwekwe lami
Vinginevyo Moro wawaaa, mashindano ya Abood Bus naHood ni burudani tosha ukiwa pale Msamvu!
1 comment:
Dear Banzi wa Moro!!
We are, or let me be specific I am very proud of ufagiliaji wako wa Moro!! Naomba nikusaidie kushikilia huwo mfagio kuendelea kufagia ili nasisi tuendeleze mji wetu!!!
Waaawaa
Post a Comment