Monday, April 20, 2009
Ole wenu Yanga kwa magoli ya LPO!
Ole wenu Yanga. Jana ilikuwa mmekwisha. Shukruni magoli ya LPO moja penalti lingine mpira umekwisha mmetunza heshima kwa sare!
Kwa mara ya kwanza nauli njia ya Mkuranga imeshuka!
Kwa abiria wanaosafiri kwa magari madogo yaendeayo njia ya Mkuranga kutoka Mbagala Rangi 3 nauli imepungua kwa asilimia 36. Kwa mfano Mbagala Vikindu sasa shilingi 300 badala ya shilingi 500 na Mbagala-Kisemvule sasa shilingi 400 bei ya zamani shilingi 600. Hii ni kwa mara ya kwanza kwa gharama za usafiri kushuka kwa njia hiyo. Mara kwa mara abiria wengi ambao ni wakulima wamekuwa wakipata wakati mgumu kwa kutozwa nauli za juu kutoka Mbagala kwenda Mwandege, Vikindu, Kisemvule na Mkuranga.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wanavijiji wa sehemu hizo kupatiwa jedwali kutoka SUMATRA inayoelezea viwango vya nauli na kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wake.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wanavijiji wa sehemu hizo kupatiwa jedwali kutoka SUMATRA inayoelezea viwango vya nauli na kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wake.
Jamani DECI
Sijui niite umaskini, sijui niite uvuvi, sijui niite kukosa elimu. Mimi nachagua la tatu kuelezea hali halisi ya DECI kwa sisi Watanzania.
Sote tunapenda fedha akiwemo mmiliki wa blog hii. Lakini ni fedha gani zinazopatikana bila kujishughulisha? Hata huko kupanda je mbegu pekee inatosha kuvuna tena mara mbili zaidi ya kile ulichopanda? Kipando chochote kina masharti yake. Lakini hili la DECI lilivuka misingi ya uhalisia. Swali dogo kabisa, inawezekanaje mtu upande kiasi kidogo halafu uvune kiasi kingi tena zaidi ya mara mbili! Huu ni uvivu. Watanzania wengi tu wavivu na ndiyo maana wengi walijiunga na DECI. Huko hawakuenda maskini peke yake, hawakuenda vilaza peke yake. Nasikia hata baadhi ya wasomi wa Chuo Kikuu walikuwa wamejiingiza kwenye DECI. Viongozi wa vyama na serikali walijiingiza kwenye DECI. Mama ntilie na wapiga debe waliingia DECI. Sasa ni kilio. Kama alivyokwisha sema Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda "This thing has never succeeded any where.." mwisho wa kunukuu. Ni ujanja ujanja tu wa maisha.

Thursday, April 9, 2009
CAADP YATATHMINI UBORESHAJI WA KILIMO
Wadau wa mfumo wa kukuza na kuendeleza Kilimo barani Afrika (Comprehensive African Agriculture Development Programme (CAADP)) iliyoanzishwa na NEPAD na Umoja wa Afrika(AU) walikutana Afrika ya kusini kuanzia tarehe 23-27 Machi 2009 kujadili mikakati ya kuwezesha Bara la Afrika kukua kiuchumi kupitia Kilimo kama njia mojawapo ya kutimiza ahadi iliyotolewa na wakuu wa nchi za Afrika huku Maputo, Mozambique. Wakuu hawa walitoa tamko la kutoa mgao wa asilimia 10 ya bajeti kila mwaka kwa ajili ya Kilimo ifikapo 2008. Ilani hii ilitolewa sambamba na kuiwezesha bara la Afrika kuweza kutimiza malengo ya milenia ya kupunguza umaskini na njaa ifikapo 2015.
Kukutana kwa Wadau hawa kwa mara ya nne sasa ni kuwawezesha nchi husika kwa wadau kujumuika pamoja na kutafakari utekelezaji wa CAADP katika maswala ya Kilimo na uchumi barani Afrika.
CAADP inatambua Kilimo kama kiini katika mikakati ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini barani Afrika. Muundo wake unatokana na azma ya waafrika wenyewe. Hivyo basi inashamiria mwelekeo mzima wa kanuni za NEPAD za kuangalia kwa undani zaidi ufumbuzi wa matatizo ya Kilimo.
Majumuisho ya Mkutano huo ni pamoja na kupitia ripoti zilizo wasilishwa kutoka kwenye nchi tofauti barani Afrika, Kuthathini majarida ya nguzo za CAADP pamoja na kiashirio cha utekelezaji wa majukumu ya CAADP.
Pamoja na hayo Mkutano uliangalia swala la kuboresha na kuwezesha nchi kushiriki katika mfumo huu wa CAADP.
Kikubwa kilichofanyika kwenye Mkutano huu ni kuundwa kwa mfuko wa dhamana (multi-donor trust fund) ambao ulipitishwa na kuidhinishwa kuanza kutekelezwa.
Dkt Maeda anatoa mwito kwa watanzania hasa wadau wa kilimo kufahamu umuhimu wa CAADP na shughuli zake na jinsi inavyoweza kuongeza nguvu katika mkakati wa kitaifa wa kukuza Kilimo.

Tuesday, April 7, 2009
"Maisha Plus" ukokotoaji?
Kuna mchezo unaendelea katika luninga ya TBC 1 unaitwa "Maisha Plus" Hivi mchezo huu una lengo gani ? ni ubunifu au ukokotoaji kutoka "Big Brother?"
Huria iwe na mipaka
Neno huria maana yake ni kufanya utakavyo mradi huvunji sheria. Lakini neno hili likitumiwa vibaya linaweza kuzaa tabia ya kufanya vitu kiholela. Matokeo yake mara nyingi si mazuri. Mara nyingine huzua vifo, mtafaruku na kuathiri kabisa maisha ya jamii. Watu wanauza bidhaa feki ukiuliza utaambiwa hujui bwana soko huria? Watu wanaanzisha dini mbalimbali bila utaratibu- unaambiwa soko huria. Watu wanakojoa barabarani hovyo hovyo -unaambiwa huria. Wenye vyombo vya kusafirisha abiria wanapandisha bei za usafiri wapendavyo kisa soko huria. Huria iwe na mipaka.
Kweli Macha Afrika mtu hali pesa peke yake
Gazeti jipya la Kwanza Jamii liko mitaani. Mchana huu nimebahatika kulisoma gazeti hili kupitia mtandao.Moja ya makala nilizosoma ni ile iliyoandikwa na Freddy Macha "Wenzetu wazungu." Ameeleza maisha ya wazungu yalivyo kwa sasa. Maisha ya kibnafsi sana. Utashangaa mtu maarufu kama mwanamuziki Boy George anakuwa msenge. Anakula madawa ya kulevya na mambo mengi ya aibu tu.
Lakini amegusia kuwa Afrika mtu akiwa tajiri ni nadra sana kutumia utajiri huo peke yake atawasaidia ndugu na jamaa, marafiki na watu wengine. Hapa Tanzania kwa mfano ukipanda daladala unaweza kuwalipia nauli hata watu watano! Ukifika kwa mama ntilie unaweza kutoa ofa kwa watu saba hata kama uliwakuta hapo na mipango yao lakini kwa kuwa ni marafiki zako na kwa kuwa leo unacho basi unatoa tu. Ukifika bar unamwaga ofa hata crate 2! Kweli Macha, Afrika mtu hali pesa peke yake. Na kwa kufanya hivyo tunajisikia raha. Huu ndiyo utamaduni wetu ni mzuri. Tuendelee kutoa mradi huumii.

Sasa wananchi wameamka
Ni leo hii mchana wakati nilipofika kituoni Kisemvule kupanda bus la kwenda Mbagala nilikuta bango lililoandikwa- Kisemvule Mbagala - sh 400/- huku wazee kwa vijana pamoja na viongozi wa kijiji wakisimamia tangazo hili na kutuelekeza wananchi tunaosafiri kuwa tusiwe tayari kulipa zaidi ya shilingi 400/-.
Jana nililipa shilingi 600/-. Leo mambo yamebadilika kabisa. Wananchi wamechachamaa, wanaona wanadhulumiwa kabisa. Bei zilitangazwa kushushwa lakini wenye magari hawakutaka kushusha. Ssaa wananchi wameamka na nguvu yao ni kubwa. Umoja ni nguvu.

Monday, April 6, 2009
Wanapokuwepo zaidi ya watu mmoja
Binadamu tumeumbwa na huruka zetu. Kuna waongeaji sana, kuna walalamikaji, kuna wapole kuna wambeya, kuna wenye huruma, kuna wajanja n.k. n.k. Ili tuweze kuishi vizuri tunahitaji kujiwekea taratibu na taratibu lazima zifuatwe. Iwe kazini, kwenye chama, kwenye dini.............
Kweli utalijua jiji
Jiji la Dar kwa sasa halitamaniki. Sehemu nyingi zimetota kwa maji. Nenda Kariakoo kuchafu, nenda Manzese chafu, rudi Mbagala chafu, tembelea Tandika chafu, sogea Magomeni oh chafu. Ama kweli sasa utalijua jiji kwa uchafu.
Kondic alichosema ni kweli
Mara tu baada ya kurejea nyumbani kutoka Cairo, Misri kwenye mechi ya kutafuta Klabu Bingwa Barani Afrika kati ya Yanga na Al-Ahly, Kocha wa Yanga Dusan Kondic alikiri kuwa kiwango cha wapinzani wao kilikuwa ni kikubwa na matarajio ya kushinda mchezo wa marudiano tena kwa magoli mengi ni ndoto.
Kweli tulichoshuhudia Jumamosi ni ukweli wa maneno hayo. Al-Ahly walionyesha kiwango cha hali ya Juu cha soka.
Muda mfupi uliopita nilikutana na rafiki yangu Msuya shabiki wa Yanga pale "Kempiski" leo hakuwa na maneno mengi alisema kuwa alitamani kuendelea soka lile japokuwa walikuwa wamefungwa. Kumbe alichosema Kondic ni kweli. Wakati mwingine tuwe wa kweli tu kama Kondic.

Watoto huwa wananuna
Si mshabiki wa Yanga lakini amesikitika kufungwa
Abiria tusubiri vituoni
Barabara ya Kilwa iendayo Mbagala Rangi 3 imekamilika kwa asilimia 95. Tatizo ni kwa abiria kusubiri mabus kwenye vituo walivyovizoea. Hii si tabia nzuri hata kidogo. Kwa mfano pale Mbagala Zakhem abiria husubiri bus karibu na Benki ya NBC ambako hakuna kituo. Kituo kimesogzwa mbele kidogo tu lakini watu wa kutoka Kiburugwa wanaona pale ndo kituo. Acheni hizo tuwe wastaarabu, tutumie vituo vizuri tulivyojengewa.
Hivi ni lazima vilabu vya pombe za kienyeji kuwa hovyo
Vikindu kuna vilabu vingi vya pombe za kienyeji (mnazi, kibuku....). Vilabu vya pombe za kienyeji hutumika zaidi na watu wa kipato cha chini. Licha ya kuwa pombe hizi ni za kienyeji hata hivyo zina wateja wengi hasa kutokana na ukweli kuwa bei yake ni rahisi ukilinganisha na pombe za viwandani.
Blog hii inachotaka kifahamike na wasomaji wake ni hali duni ya vilabu hivi. Mara nyingi utakuta zimeezekwa ovyo ovyo hata vyoo vyake huwa ni vya kubabaisha kabisa. Kunywa pombe ya kienyeji haina maana kuweka mazingira inakopatikana pombe hiyo katika hali dun i. Ni hatari kwa afya zetu. Pichani moja ya klabu cha pombe - Vikindu, Mkuranga.
Barabara safi - lakini maji machafu?
Kamsopi akiwa Chalinze
Subscribe to:
Posts (Atom)