Monday, April 20, 2009

Jamani DECI

Sijui niite umaskini, sijui niite uvuvi, sijui niite kukosa elimu. Mimi nachagua la tatu kuelezea hali halisi ya DECI kwa sisi Watanzania.

Sote tunapenda fedha akiwemo mmiliki wa blog hii. Lakini ni fedha gani zinazopatikana bila kujishughulisha? Hata huko kupanda je mbegu pekee inatosha kuvuna tena mara mbili zaidi ya kile ulichopanda? Kipando chochote kina masharti yake. Lakini hili la DECI lilivuka misingi ya uhalisia. Swali dogo kabisa, inawezekanaje mtu upande kiasi kidogo halafu uvune kiasi kingi tena zaidi ya mara mbili! Huu ni uvivu. Watanzania wengi tu wavivu na ndiyo maana wengi walijiunga na DECI. Huko hawakuenda maskini peke yake, hawakuenda vilaza peke yake. Nasikia hata baadhi ya wasomi wa Chuo Kikuu walikuwa wamejiingiza kwenye DECI. Viongozi wa vyama na serikali walijiingiza kwenye DECI. Mama ntilie na wapiga debe waliingia DECI. Sasa ni kilio. Kama alivyokwisha sema Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda "This thing has never succeeded any where.." mwisho wa kunukuu. Ni ujanja ujanja tu wa maisha.

No comments: