Thursday, April 9, 2009

CAADP YATATHMINI UBORESHAJI WA KILIMO

Wadau wa mfumo wa kukuza na kuendeleza Kilimo barani Afrika (Comprehensive African Agriculture Development Programme (CAADP)) iliyoanzishwa na NEPAD na Umoja wa Afrika(AU) walikutana Afrika ya kusini kuanzia tarehe 23-27 Machi 2009 kujadili mikakati ya kuwezesha Bara la Afrika kukua kiuchumi kupitia Kilimo kama njia mojawapo ya kutimiza ahadi iliyotolewa na wakuu wa nchi za Afrika huku Maputo, Mozambique. Wakuu hawa walitoa tamko la kutoa mgao wa asilimia 10 ya bajeti kila mwaka kwa ajili ya Kilimo ifikapo 2008. Ilani hii ilitolewa sambamba na kuiwezesha bara la Afrika kuweza kutimiza malengo ya milenia ya kupunguza umaskini na njaa ifikapo 2015.

Kukutana kwa Wadau hawa kwa mara ya nne sasa ni kuwawezesha nchi husika kwa wadau kujumuika pamoja na kutafakari utekelezaji wa CAADP katika maswala ya Kilimo na uchumi barani Afrika.

CAADP inatambua Kilimo kama kiini katika mikakati ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini barani Afrika. Muundo wake unatokana na azma ya waafrika wenyewe. Hivyo basi inashamiria mwelekeo mzima wa kanuni za NEPAD za kuangalia kwa undani zaidi ufumbuzi wa matatizo ya Kilimo.

Majumuisho ya Mkutano huo ni pamoja na kupitia ripoti zilizo wasilishwa kutoka kwenye nchi tofauti barani Afrika, Kuthathini majarida ya nguzo za CAADP pamoja na kiashirio cha utekelezaji wa majukumu ya CAADP.

Pamoja na hayo Mkutano uliangalia swala la kuboresha na kuwezesha nchi kushiriki katika mfumo huu wa CAADP.

Kikubwa kilichofanyika kwenye Mkutano huu ni kuundwa kwa mfuko wa dhamana (multi-donor trust fund) ambao ulipitishwa na kuidhinishwa kuanza kutekelezwa.

Dkt Maeda anatoa mwito kwa watanzania hasa wadau wa kilimo kufahamu umuhimu wa CAADP na shughuli zake na jinsi inavyoweza kuongeza nguvu katika mkakati wa kitaifa wa kukuza Kilimo.

No comments: