Gazeti jipya la Kwanza Jamii liko mitaani. Mchana huu nimebahatika kulisoma gazeti hili kupitia mtandao.Moja ya makala nilizosoma ni ile iliyoandikwa na Freddy Macha "Wenzetu wazungu." Ameeleza maisha ya wazungu yalivyo kwa sasa. Maisha ya kibnafsi sana. Utashangaa mtu maarufu kama mwanamuziki Boy George anakuwa msenge. Anakula madawa ya kulevya na mambo mengi ya aibu tu.
Lakini amegusia kuwa Afrika mtu akiwa tajiri ni nadra sana kutumia utajiri huo peke yake atawasaidia ndugu na jamaa, marafiki na watu wengine. Hapa Tanzania kwa mfano ukipanda daladala unaweza kuwalipia nauli hata watu watano! Ukifika kwa mama ntilie unaweza kutoa ofa kwa watu saba hata kama uliwakuta hapo na mipango yao lakini kwa kuwa ni marafiki zako na kwa kuwa leo unacho basi unatoa tu. Ukifika bar unamwaga ofa hata crate 2! Kweli Macha, Afrika mtu hali pesa peke yake. Na kwa kufanya hivyo tunajisikia raha. Huu ndiyo utamaduni wetu ni mzuri. Tuendelee kutoa mradi huumii.
No comments:
Post a Comment