Wanakijiji walipata taarifa za mapato na matumizi ya kijiji kwa mwaka 2011 ambapo mapato yaliyopatikana ni kiasi cha Tshs 37 milioni.Takribani asilimia zaidi ya 70 ya mapato haya yalitumika kuimarisha ofisi ya kijiji kwa kujenga ukumbi wa mikutano, vyumba vya biashara na ukarabati. Ukumbi wa mikutano unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwaka huu. Nyingine zilitumika katika kuboresha miundo mbinu ya shule za msingi (Kisemvule) hasa kutengeneza madawati. Sekondari ya Vikindu aliyopo kijijini ambayo ni ya kata walipata fedha za kujenga bohari ya shule.
Changomoto kubwa iliyojitokeza suala la ulinzi wa kijiji kwa wakati huu ambao wahamiaji ni wengi na shughuli ni nyingi.Migogoro ya ardhi ni moja ya changamoto inayoikumba serikali ya kijiji yote haya yalijadiliwa na kupendekeza njia ya kuweza kukabiliana nazo.
Katika kuleta mabadiliko na kuboresha kipato cha wanakijiji ushauri ulitolewa kwa wanakijiji kujiunga katika vikundi vya maendeleo na kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya kilimo na ufugaji.
Kijiji cha Kisemvule kilichopo mkoani Pwani wilaya ya Mkuranga ni kijiji kinachokua kwa kasi ya haraka kutokana na wawekezaji kupendelea kuwekeza katika kijiji hicho kutokana mazingira mazuri yanayopatikana katika kijiji hiki kama vile ardhi,barabara nzuri, umeme na maji mengi na yenye ladha nzuri.
1 comment:
waathirika wazidi kijiji ya juu ....
Post a Comment