Mkutano wa Mwaka wa Kijiji cha Kisemvule ulifanyika jana tarehe 5/2/2012 kijijini Kisemvule. Hapo yalizungumzwa mambo mengi ya msingi. Nikiwa mwanakijiji wa Kisemvule nilifurahishwa na kiwango cha uaandaji wa taarifa za kijiji. Uongozi ulitoa taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2011 na kuwasilisha Bajeti ya mwaka 2012 itakayoishia mwezi Desemba kipaumbele namba moja kikiwa ni kujenga zahanati ya kijiji ambayo itagharimu takribani tshs 21,000,000/=. Kwenye kikao hicho wanakijiji wengi walihudhuria wakiwemo wake kwa waume, vijana na wadau mbalimbali wa maendeleo kati yao ni wakuu wa shule za msingi na sekondari, Bwanashamba wa Kijiji na Mganga Mkuu wa Dispensary ya St. Vicent Vikindu.
Wanakijiji walipata taarifa za mapato na matumizi ya kijiji kwa mwaka 2011 ambapo mapato yaliyopatikana ni kiasi cha Tshs 37 milioni.Takribani asilimia zaidi ya 70 ya mapato haya yalitumika kuimarisha ofisi ya kijiji kwa kujenga ukumbi wa mikutano, vyumba vya biashara na ukarabati. Ukumbi wa mikutano unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwaka huu. Nyingine zilitumika katika kuboresha miundo mbinu ya shule za msingi (Kisemvule) hasa kutengeneza madawati. Sekondari ya Vikindu aliyopo kijijini ambayo ni ya kata walipata fedha za kujenga bohari ya shule.
Changomoto kubwa iliyojitokeza suala la ulinzi wa kijiji kwa wakati huu ambao wahamiaji ni wengi na shughuli ni nyingi.Migogoro ya ardhi ni moja ya changamoto inayoikumba serikali ya kijiji yote haya yalijadiliwa na kupendekeza njia ya kuweza kukabiliana nazo.
Katika kuleta mabadiliko na kuboresha kipato cha wanakijiji ushauri ulitolewa kwa wanakijiji kujiunga katika vikundi vya maendeleo na kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya kilimo na ufugaji.
Kijiji cha Kisemvule kilichopo mkoani Pwani wilaya ya Mkuranga ni kijiji kinachokua kwa kasi ya haraka kutokana na wawekezaji kupendelea kuwekeza katika kijiji hicho kutokana mazingira mazuri yanayopatikana katika kijiji hiki kama vile ardhi,barabara nzuri, umeme na maji mengi na yenye ladha nzuri.
Mwenyekiti wa Kijiji Bw. Omari Makunge akifafanunua jambo.
Katibu Mtendaji wa Kijiji Bw. Mzome(wa kwanza kushoto)akisikiliza kwa makini hoja.
Vijana wakiwa mkutanoni
Mama Eric (mwenye khanga begani)mwanakijiji wa Kisemvule akiwa mkutanoni amechangia hoja nyingi zenye manufaa hasa za kilimo na ufugaji.
Akina mama nao walijumuika na wanakijiji wengine katika mkutano huo na kuchangia hoja mbalimbali hasa elimu.
Meza kuu ilikuwa makini na kujibu hoja kutoka kwa wanakijiji.
Kama kawaida idadi ya wanaume mkutanoni ilizidi ile ya wanawake hivyo hivyo kwa hoja.
1 comment:
waathirika wazidi kijiji ya juu ....
Post a Comment