Leo jioni nikiwa kazini katika kijiji cha Mabogini, Moshi vijijini nilidondosha noti ya shilingi mia tano. Watoto hawa waliiona na kuikota kisha waliniita, "mzee umedondosha hela." Nikaitikia wito nikapokea noti hiyo kisha nikawarudishia na kuwaambia asante watoto wazuri.Jambo la maana nililojifunza kutoka kwa watoto hawa ni kwamba wana malezi mazuri kutoka kwa wazazi/walezi na walimu wao.Wangeweza kuificha noti hiyo kisha wakagawana.Hongera kwa wazazi na walimu wa watoto hawa.
1 comment:
Ni kweli wazazi wa watoto hawa wanastahili pongezi. Ni aghalabu sana kukuta watoto wa aina hii kwa kipindi hiki tulichonacho
Post a Comment