Tuesday, December 31, 2013
Hongera Dogo Richard Banzi
Dogo Richard Banzi (a.k.a Mjeshi) akisakata rumba na kitu chake kwenye ukumbi wa Tanzania mjini Morogoro siku ya Tarehe 27/12/2013. HONGERA!
Ndafu, acha mchezo msee!
Huu ndiyo utaalamu wa kuchoma ndafu.Huhitaji kuwa na oven. Chimba shimo kipimo cha mbuzi na weka mkaa. Mbuzi anaiva kwa mvuke tu. Wenyewe wachagga!
Meab Mdimi na Catherine Banzi
Dada Meab Mdimi na binti yangu Catherine Banzi wakishangaa watoto wakiogelea nyumbani kwa mjomba Dr. G.Mluge (Marehemu) huko Mbezi Beach tarehe 26 Des 2013.
Mama Jack na Mtani Jembe!
Mama Jack wa Kisemvule ni shabiki wa kutupwa wa Simba Sports Club akiwa pamoja na Baba Herieth wakifurahi ushindi wa Simba kumchabanga Yanga 3-1
Mchoraji kazini
Aliitwa mchoraji na kuwachora watoto hata wakubwa pia jinsi walivyotaka na hapo ndipo walipotokea spidermen!
Dada Batsheba Sajan
Tarehe 26/12/2013 tulialikwa na dada Janet Mluge nyumbani kwao Mbezi Beach-Dar. Hapa nilikutana na ndugu zangu wengi pamoja na watoto zao ambao wengi wao walikuwa ni akina uncle! Mbele ya picha hii anaonekana dada Batsheba Sajan a.k.a Sheba! Alikuwa siku moja nzuri ya kukumbukwa kwa mwaka 2013. Asante Dada Janeth pamoja na shemeji yetu Tom kwa wazo zuri na kulitekeleza pia. Asante aunt Rest kwa kutukaribisha.
Karibuni wajukuu zangu
Hivi ndivyo Bi. R.Mluge alivyowakaribisha wajukuu zake siku ya tarehe 26/12/2013 (boxing day) nyumbani kwake Mbezi Beach.
Mtaro umefurika Tandika Dar
Licha ya kujenga mitaro mizuri lakini uchafu umefurika ndani ya mitaro. Je ni uzembe au ni kutokujali tu!
Tumepata goli moja tu!
Shabiki huyu wa Yanga haamini kuwa licha ya kuwa na akina Kiiza, Okwi, Ngassa, Kavumbagu wameambulia goli moja tu huku wakibugizwa magoli matatu.
Huyu alizawadiwa jezi nyekundu ya ZAMALEK!
Shabiki huyu wa Yanga wa Kisemvule alizawadiwa jezi nyekundu ya Zamalek na shabiki wa Simba baada ya mchezo wa Mtani Jembe kumalizika na Yanga kufungwa 3-1
Mambo ya kukumbukwa 2013-MTANI JEMBE
Tuesday, December 24, 2013
Monday, December 23, 2013
Uzembe wa Kaseja
Uzembe wa Kaseja katika mchezo wa Mtani Jembe ulivyoigharimu Yanga. Na hilo likawa goli la tatu- Goooo! (Picha kwa hisani ya gazeti la Mwanaspoti - 23/12/2013)
Tuesday, December 17, 2013
Wasichana wanakula kidogo tu
Inasemekana wasichana wanakula kidogo tu. Je ni kweli? (Picha na Dr. L.Kasuga, ARI-Naliendele, Mtwara)
Mtwara-Dar 'kuchimba dawa'
Safari ya Mtwara-Dar abiria "wanachimba dawa' (Picha kwa hisani ya Dr. L.Kasuga wa ARI-Naliendele, Mtwara)
Kumbukumbu ya mafuriko Mtwara Januari 2013
Mafuriko ni balaa. Hivi ndivyo hali ilivyokuwa eneo la Majengo mjini Mtwara Januari 2013(Picha kwa hisani ya Dr. L.Kasuga wa ARI-Naliendele, Mtwara)
Mwembe wa Dr. Kasuga
Dr. Kasuga anasema kilimo ni biashara haonjeshi hata embe moja. (Picha kwa hisani ya Dr. L.Kasuga wa ARI-Naliendele, Mtwara)
Gulio la samaki
Gulio la samaki. Hapa wapo wauzaji na wanunuzi wa samaki. (Picha kwa hisani ya Dr. Kasuga wa ARI-Naliendele, Mtwara).
Aina za karanga
Hizi ni aina mbalimbali za zao la karanga. Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele, Mtwara ni maarufu kwa utafiti wa zao la Karanga.
Subscribe to:
Posts (Atom)