Thursday, April 30, 2015

Hapa ndipo anapopumzika uncle Dr. Gregory Mluge

Ninapopata fursa ya kurudi nyumbani Matombo Morogoro huwa natenga muda wa kufika makaburini walikozikwa ndugu zangu na kusali pamoja na kuwaombea. Hapa wamezikwa ndugu zangu,majirani na marafiki wengi. Hili ni kaburi la mjomba Dr. Gregory Constance Paul Mluge. Inakaribia miaka  mitatu sasa tangu mjomba Dr. Mluge afariki na kuzikwa nyumbani kwetu Matombo, Morogoro. Leo kwa namna ya pekee kabisa nimemkumbuka na kwabahati mwaka wa jana mwishoni (wakati wa Christmass) nilikuwa Matombo na kubahatika kupiga picha ya kaburi la marehemu Dr.Mluge. Huyo ni mjomba wangu kwani mama yangu na mama yake ni mtu na mdogo wake tumbo na baba mmoja. Dr. Mluge ni mmoja waliochangia katika masomo yangu hadi kufikia hatua hii. Dr. Mluge licha ya kuwa daktari wa binadamu aliyetoa huduma ndani na nje ya nchi lakini alikuwa anapenda kilimo sana. Aliporudi nyumbani alijishughulisha sana na kilimo. Siku zote tulipkuwa tunazungumzia kilimo alikuwa akisema 'uncle' sioni kama mnafanya vizuri sana kwenye sekta hiyo si unao wenzetu Ulaya wanavyofanya? Nimeambiwa pia uncle Mluge alikuwa mpigaji mzuri wa kinanda kanisani. Ni kweli,Dr. Mluge alikuwa anapenda muziki sana. Nyumbani kwake Mbezi alikuwa na chumba kilichosheheni vifaa vya muziki kikiwemo kinanda kikubwa. Pumzika mjomba Dr. Gregory Mluge umetuletea heshima kwenye familia na kutoa huduma ndani na nje ya nchi.

Nakukumbuka Mjomba Balozi Daniel Mloka

Hii ni picha ya kaburi alilozikwa Balozi Daniel Narcis Mtonga Mloka. Haya ni makaburi ya Parokia ya Mt.Paulo ya Matombo. Ndugu zangu wengi wamezikwa hapa akiwemo mama yangu mzazi.Ni miaka zaidi ya 21 sasa tangu Balozi Mloka atuache ghafla wakati ambapo wengi tulikuwa tunamtegemea. Kitu kimoja ambacho Balozi Mloka alinifundisha ni kuandika na kweli alikuwa ni mwandishi mzuri ingawa fani yake halisi ni uchumi. Nakumbuka nikiwa likizo nyumbani kwake Stockholm - Sweden wakati huo mimi nasoma Soviet Union au Urusi, tuliweza kuandika kitabu (Nitawaeleza siku nyingi title ya kitabu hicho nadhani hatkufanikiwa kukitoa).Balozi Mloka alikuwa anatambua azungumze nini na mbele ya nani. Pamoja ya kwamba alikuwa uncle wangu, mumewe shangazi yangu dada wa baba yangu. Balozi Mloka alikuwa ni rafiki yangu wa kweli. Pumzika uncle Balozi Mloka.

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo





Picha hizi nilizipiga kwenye mazingira ya shule. Hapa ni shule ya Msingi Kisemvule, si mbali na mahali ninapoishi. Picha za mbili juu  ni watoto wa asili ya kutoka Pwani wao ni mpira. Huyu mtoto aliyekumbatia vitabu na madaftari ni Malik Ulomi. Ni mtoto wa Kichagga. Unaweza kuandika hadithi ndefu kuhusu picha za watoto hawa. Toa maoni yako

Ifahamu "Bright Angels" Sec. School






Unaifahamu "Bright Angels" Sec. School? Nifuate.
Shule hii ya Sekondari iko Mkoa wa Pwani wilaya  ya Mkuranga, kijiji cha Kisemvule - Takribani Kilometa 40 kutoka jijini Dar Es Salaam. Shule hii huchukua wanafunzi wa bweni na wa kutwa na kwa sasa ni ya mchanganyiko (wavulana na wasichana).
Mawasiliano:- P.O.Box 11292,Dar Es Salaam
                        Barabara ya Kilwa, Vikindu Campus-Kisemvule Village
                        simu: office 076202027993,0717151664,0762800470,0784853100
                        Web:www.brightangels.ac.tz
'Bright Angels' Motto- Shine with Actions
Reg. No. 3556

Watoto wa Utatu Mtakatifu Parokia ya Vikindu wakiwa na Askofu Msaidizi Nzigilwa



Kanisa linawalea watoto wa Kanisa kiimani wangali wadogo. Hawa ni watoto wa Utatu Mtakatifu - Parokia ya Vikindu wakiwa katika picha ya Pamoja na Askofu Msaidizi Nzigilwa wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Askofu Nzigilwa  alifika Parokiani Vikindu  mwezi Juni 2014 kutoa Sakramenti ya Kipaimara kwa walioandaliwa.

Wamepata Kipaimara lakini wako wapi sasa?

Mwanangu John Linus Banzi (wa pili kutoka kushoto) alipata kipaimara mwaka jana. Kanisa linajiuliza, je, watoto wetu wanaendelea kufuata mafundisho ya kanisa na kusali kwa mujibu wa taratibu za Kanisa? Hili ni changamoto kwa Kanisa. Wazazi tunawajibu mkubwa kuhakikisha kuwa watoto wetu  wanaendeleza imani ya Kanisa letu KATOLIKI.

Wednesday, April 22, 2015

Harusi ya Bw & Bibi Joachim Ndunguru haikuwa na makuu




Tarehe 11 April, 2015, mimi na mke wangu Mwl. Nancy tulisimamia harusi ya Bw & Bibi Ndunguru tunaoishi nao hapa Kisemvule na kusali kwenye Kanisa la Mt. Vinsenti wa Paulo, Parokia ya Vikindu. Kilichonifurahisha katika harusi hii ni jinsi mipango ilivyoandaliwa na kutekelezwa kwa wakati. Tuliwahi kufika Kanisa, ibada ikafanyika. Mimi na mke wangu tulibahatika kusoma masomo ya siku hiyo. Waumini waliohudhuria walikuwa wachache, lakini kwaya ya Mt. Petro ilitumbuiza kuanzia kanisani hadi nyumbani. Hakukuwahi kufanyika hata kikao kimoja cha maandalizi. Lakini waliokaribishwa walipata chakula na vinywaji na usafiri kutoka kanisani ulikuwepo. Mimi nikiwa 'Best Man' katika harusi hiyo nilipata fursa ya kufungua champaigne na kuwagawia wageni waalikwa. Wanajumuiya ya Mt. Joseph Mfanyakazi ni moja ya kikundi kilichofanikisha harusi hii ambapo shughuli za kuwapokea maharusi zilifanyika nyumbani kwao Kisemvule. IDUMU NDOA HII. MILELE AMINA.

Enzi za usafiri wa mabus ya EAR (RAB)

Kwa mara ya kwanza nilisafiri kwa bus la EAR kwenda Njombe masomoni kidato cha kwanza Njombe Secondary School mwaka 1974. Safari yangu ilianzia Morogoro Railway Station. Mabus haya yalikuwa na utaratibu mzuri. Yalikuwa na madaraja mawili  la kwanza na la pili (mimi nilisafiri daraja la pili tena kwa kutmia 'Government warrant'). Madereva wake walikuwa ni watu wazima. Hawakuwa wakienda kwa mwendo kasi, kulikuwa na vituo maalum vya kuyakagua mabus hayo na kuyafanyia service pamoja na kuweka mafuta. Kituo kimojawapo ni Mikumi kabla hujaanza kuupanda mlima Kitonga ukitokea Morogoro. Ukifika Iringa  ilikuwepo station kubwa ya mabus ya railways. Hapa mabus hukaguliwa na abiria wanaoendelea na safari hupumzika kwa muda mrefu kabla ya kupatiwa bus lingine kwa safari. Barabara hazikuwa nzuri sana. Ninamshukuru Mungu kwa kipindi chote cha miaka sita nilioishi kama mwanafunzi mkoani Iringa nikisafiri kwa mabus ya 'RAB' ajali zilikuwa chache sana na wala sikumbuki kama iliwahi kutokea. Hivi sasa barabara zimeboreshwa, magari ni ya kisasa zaidi na kila mmoja wetu anaweza kuendesha magari ya abiria (buses). Kila kukicha ni ajali mbaya tena zenye kuua abiria. Hivi hatuwezi angalau kupunguza ajali hizi?

Askari hapewi shuka

Daladala hili linalofanya shughuli zake Ubungo-Mbagala Rangi 3 lina ujumbe unaosomeka 'Asakari hapewi shuka.' Ni ujumbe mzito. Askari kama tujuavyo kazi yake ni kulinda ni kupambana na hakuna kulala. Pengine mwenye kumiliki gari hii ana maana ya kupambana katika maisha hadi mafanikio yapatikane.

Anaipenda Simba Sports Club

Kwa wale ambao wamekwishasafiri kupitia barabara ya Kilwa, ukitokea  Mtoni Mtongani kuelekea Mbagala unapokuwa kwenye kituo cha Msikitini angalia upande wako wa kulia mlimani utaiona nyumba hii iliyoezekwa paa la rangi nyekundu. Ukipita usiku taa za nje za nyumba hii zote ni nyekundu. Huyu ni mpenzi mwenzangu wa klabu yetu ya Msimbazi- Simba Sports Club. Popote jitangaze, unaogopa nini?

Tuesday, April 21, 2015

Mpunga unaanza kuchanua shambani

Watanzania wengi tunapenda kula wali, lakini wali unatokana na kulima  mpunga. Ili uweze kufanikiwa katika kilimo cha mpunga  ni sharti ufuate utaalamu wa kilimo hicho kuanzia utayarishaji wa shamba,mbegu bora, jinsi ya kupambana na wadudu na magonjwa, uvunaji, utunzaji, kukoboa,kusafirisha na kutafuta soko ili walaji wapate kuutumia. Haya yote unaweza kuyapata kutoka kwa mshauri wa kilimo aliyeko kijijini,wilayani, taasisi za utafiti na mafunzo na hata Wizarani.

Raia wakigeni akishambuliwa Afrika ya Kusini

Hivi ndivyo inavyotokea Afrika ya Kusini hivi sasa. Raia wa kigeni amewekwa mtu kati anashambuliwa na watu wanaangalia tu. Hakuna mzungu hapo, wote ni weusi, wanamshambulia mweusi mwenzao. Afrika hii hii, tunabaguana kwa chuki tu, kwa ubinafsi wetu. Hivi kweli siku moja Afrika tunaweza kuwa wamoja? Inatakiwa tafakuri ya kina.

Nyumba ya gharama nafuu

Nimepokea picha hii kutoka kwa mtaalamu mmoja akinieleza kuwa  hii ni moja ya picha ya nyumba  ambazo tunaweza kuzijenga kwa gharama nafuu. Ushauri wangu hivi kwanini tunashindwa kutafuta sehemu ikapimwa vizuri na kuwezesha kikundi kumiliki eneo hilo hasa vijana tukawapa mtaji nyumba za aina hii zikajengwa halafu wamapangishwe watu. Kama eneo la ekari zipatazo 20 hata 10 tu zikajengwa nyumba za aina hizi  kila wilaya kila mwaka tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika kuwapatia wananchi wetu makazi bora.

Friday, April 10, 2015

Igizo la Ijumaa Kuu liliwaliza wengi Vikindu


Kwa mara ya kwanza katika historia ya Parokia ya Vikindu. Vijana wa Seminari ya Vinsentian iliyopo Vikindu walifanya igizo la mateso ya Bw. wetu Yesu Kristo siku ya Ijumaa kuu. Igizo hili lililiza waumini wengi walifika kwenye ibada hiyo.

Semina kuhusu ndoa-Parokia ya Vikindu


Ili kuimarisha ndoa zilizopo na kuvutia wasiofunga ndoa wafunge ndoa, mwezi Machi tarehe 14, 2015 , Parokia ya Vikindu iliendesha semina ya wanandoa na wasio na ndoa kwenye ukumbi wake wa mikutano. Washiriki wa semina hiyo walikuwa ni 20 ni watoa mada walitoka Kamati ya Utume wa Familia-Jimbo Kuu la Dar Es Salaam (Bw.Didas Kapinda na Bw. Adrian Mpande). Kikubwa kilichozungumzwa kwenye semina hiyo ni kuzingatia mambo matatu katika ndoa nayo ni:- Uaminifu, Udumifu na Upokeaji.

Chai ya Ijumaa ya watafiti wa makao makuu-DSM (DRD)

Hii nayo ni motisha kwa wafanyakazi. Idara ya Utafiti na Maendeleo Makao Makuu-DSM imejiwekea utaratibu wa kuwa na chai ya saa nne kila siku ya Ijumaa. Wafanyakazi wenyewe hugharamia chai hiyo. Kikubwa wafanyakazi hutumia muda huo kupeana taarifa rasmi na zisizo rasmi!

Lyamungo Guest House-Morogoro



Kwa mara nyingine tena naweka post ya Lyamungo Guest House. Ninasababu zangu. Naipenda Lyamungo kwa sababu kuu mbili. Moja usafi na pili menejimenti ya nyumba hiyo ya wagenu ni superb! ikiongozwa na meneja Malamsha. Niwapo Lyamungo najisikia nyumbani kabisa. Angalia jinsi meneja Malamsha anavyofanya usafi kwa kujituma bila kujali nafasi yake (cheo).

Catherine na Maria - Binti zangu

Nimebahatika kupata watoto wawili. Kati ya hao wawili na mabinti. Catherine Banzi (kulia) anasoma Victory Secondary School kidato cha Nne na Maria Banzi  yuko darasa la Nne shule ya msingi ya Carmel iliyoko Vikindu, Mkuranga, Mkoa wa  Pwani. Namshukuru Mungu

Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine Morogoro

SUA- Kitovu cha wataalamu wa kilimo wa elimu ya juu Tanzania. Wataalamu wengi wa kilimo hapa nchini wamepikwa SUA. Hii ndiyo SUA (Administration Block). Chuo hiki kipo mkoani Morogoro.