Ninapopata fursa ya kurudi nyumbani Matombo Morogoro huwa natenga muda wa kufika makaburini walikozikwa ndugu zangu na kusali pamoja na kuwaombea. Hapa wamezikwa ndugu zangu,majirani na marafiki wengi. Hili ni kaburi la mjomba Dr. Gregory Constance Paul Mluge. Inakaribia miaka mitatu sasa tangu mjomba Dr. Mluge afariki na kuzikwa nyumbani kwetu Matombo, Morogoro. Leo kwa namna ya pekee kabisa nimemkumbuka na kwabahati mwaka wa jana mwishoni (wakati wa Christmass) nilikuwa Matombo na kubahatika kupiga picha ya kaburi la marehemu Dr.Mluge. Huyo ni mjomba wangu kwani mama yangu na mama yake ni mtu na mdogo wake tumbo na baba mmoja. Dr. Mluge ni mmoja waliochangia katika masomo yangu hadi kufikia hatua hii. Dr. Mluge licha ya kuwa daktari wa binadamu aliyetoa huduma ndani na nje ya nchi lakini alikuwa anapenda kilimo sana. Aliporudi nyumbani alijishughulisha sana na kilimo. Siku zote tulipkuwa tunazungumzia kilimo alikuwa akisema 'uncle' sioni kama mnafanya vizuri sana kwenye sekta hiyo si unao wenzetu Ulaya wanavyofanya? Nimeambiwa pia uncle Mluge alikuwa mpigaji mzuri wa kinanda kanisani. Ni kweli,Dr. Mluge alikuwa anapenda muziki sana. Nyumbani kwake Mbezi alikuwa na chumba kilichosheheni vifaa vya muziki kikiwemo kinanda kikubwa. Pumzika mjomba Dr. Gregory Mluge umetuletea heshima kwenye familia na kutoa huduma ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment