Tuesday, March 27, 2012

Maggid - Menu imeficha perege!


Kama kuna vitu ambavyo Maggid huvipenda ni chakula kilichoandaliwa vizuri na hasa vile vya kulumagia (Tabia ya Wazaramo hiyo). Anapotoka Iringa kwenda Dar hakosi kupitia kwa Bi.Mkora wa Msamvu na kupata msosi mvuri aupendao. Hivi majuzi aliandaliwa msosi huu ambao umekosa samaki aina ya perege!(Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog)

Mjengwa na kwao Nyeregete

Mara nyingi huwa nasoma Blog ya Mjengwa. Pia namfahamu Mjengwa tangu wakati akiwa anaandikia gazeti la RAI, alipokuwa SWEDEN na kuna wakati alinitembelea nilipokuwa naishi Temeke Veterinary.Aliwahi pia kusaidia jezi Klabu yetu ya Mpira ya BERLIN (MILA)ya Temeke Veterinary.

Kwa jinsi ninavyomfahamu, Mjengwa ni Mzalendo na anauchungu wa nchi hii. Hana makuu. Atakuonyesha alipokuwa anaishi-Kinondoni kwa mama yake, marafiki zake, chakula anachopenda na hujali sana muda na ahadi. Maggid akisema atakutemebelea ni kweli atafika kwa muda uliopangwa.

Tangu aliporudi nchini Maggid hakosi kwenda nyumbani kwao Nyeregete-Mbarali ambako ni asili ya baba yake huko kuna dada zake, kaka zake, baba wakubwa na wadogo shangazi zake, babu na majirani.Nafahamu pia mama yake Maggid ni Mzaramo. Kwa kufanya hivyo, Maggid anawafahamu watu wake, ndugu zake,mazingira wanamoishi,uzalishaji wao. Anajitahidi kwa kila hali kuwatoa mahali walipo na kuwafikisha mahali fulani hata kama kwa uelewa tu. Angalia daraja analovuka ili kufika kijijini kwao Nyeregete! Hayo yote Mjengwa haandiki kufurahisha watu anataka watu wafahamu hali halisi ya vijiji vyetu. Mjengwa si Mbunge! Lakini amethubutu (Picha zote kwa hisani ya Mjengwa BLOG
Mjengwa na dada yake nyumbani kwao Nyeregete
Mjengwa akiwa na walimu na wanafunzi kijijini kwao Nyeregete

Sunday, March 25, 2012

Support ya viongozi je?


Unapokuwa na sapoti ya viongozi kama hawa kwani nini usishinde? Kushoto mwenye suti nyeupe Mh.Samwel Sitta Waziri wa Afrika ya Mashariki,katikati mwenye suti ya rangi ya udongo Mh.Frederick Sumaye Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu,said El Maamry mwenye cap,Mbunge kijana Zitto Kabwe mwenye jezi nyekundu alieinua vidole wakitoa company ya nguvu kwa Mwenyekiti wa Simba Mh.Aden Rage aliyevaa shati jekundu huku akitabasamu. Waliokaa niliyeweza kumtambua mara moja ni Kassim Dewji mmoja wa kikundi cha Friends of Simba. Yuko wapi Mh. Tibaijuka? Simba hatujifichi.Hapa masuala ya siasa pembeni Simba imewaunganisha. Ningekuwepo ningekuwa karibu ya Dewji!

Mashabilki chachu ya ushindi


Unapokuwa na washabiki kama hawa ujue unachinjwa tu. Hebu angalia 'damu' iliyopo uwanjani'.Eh kidedea.

Sunzu akaongeza la pili

Felix Sunzu aliihakikishia Simba ushindi kwa kufunga bao la pili.

Emmanueal Okwi mfungaji wa goli la kwanza

Kama kawaida yake Emmanuel Okwi mfungaji wa goli la kwanza aliichachafya sana ngome ya El Satif hasa kipindi cha pili na kufanikiwa kupata goli la kwanza(Picha kwa hisani ya Michuzi blog)

Kombe la Shirikisho la Afrika-Simba yaitungua EL Satif ya Algeria 2-0

Picha kwa hisani ya Michuzi blog
Nikiwa hapa Mananga, Swaziland kwa kumpitia mtandao nimepata kufuatilia pambano la mchezo wa Kombe la Shirikisho la Afrika kati ya Simba Sports Club ya Dar Es Salaam, Tanzania na El Satif ya Algeria. Matokeo Simba 2 El Satif 0. Kwa mujibu wa Coulds FM radio magoli hayo yamefungwa na Emmanuel Okwi na Felix Sunzu.Clouds mko juu sana wanangu hongereni!

Ubungo ya Mbabane

Kituo cha magari jijini Mbabane.

Kituo cha magari cha jijini Mbabane Swaziland ni kidogo kwa ukubwa,idadi ya magari na pia hakina uzio.Ukilinganisha na chetu cha Ubungo, jijini Dar.Ubungo watu ni wengi, magari ni mengi na pilika ni nyingi. Hapa Swaziland daladala zipo za kutosha vingi ni vipanya vinaingia hadi katikati ya jiji. Mabus ya kwenda mikoani ni yale marefu ya kizamani!Lakini barabara zao ni nzuri. Kuhusu usafi wa jiji naona ni vizuri tukajifunza kutoka Mbabane.

Nimesali Kanisa la Mt.Dolorosa-Mbabane,Swaziland

Leo Jumapili nimebahatika kusali katika Kanisa Katoliki la Mt. Dolorosa lililoko jijini Mbabane-Swaziland.Ni bahati iliyoje kusali kwenye Kanisa ambalo jina lake ni jina la mama mdogo Dolorasa wa Makuburi, Dar.

Kanisa hili ni kubwa kiasi na limejengwa kwa muundo wa msalaba.Ibada niliyohudhuria iliendeshwa kwa lugha ya Kiingereza. Ibada katika kanisa hili huendesha kwa lugha kuu tatu-Kiswati,Kiingereza na Kireno. Kwa kawaida misa ya pili saa 2.00 ni ya Kiingereza na saa 4.30 ni Kiswati kila Jumapili. Lakini Jumapili ya kwanza na ya tatu ya mwezi misa ya pili huwa ni ya Kireno.
Nilichoona.
Taratibu zote za ibada ni sawa kabisa kama tunavyoendesha ibada zetu(katoliki)Tanzania. Tatizo ni lile lile vijana wanaohudhuria ibada ni wachache. Utoaji wa sadaka bado ni mdogo na sarafu hotelwa pia!Ingawa hawatangazi kilichopatikana. (huenda wanaweka kwenye mbao za matangazo). Sikuona vipaji hapa (nafikiri sisi tunafanya vizuri).Wachelewaji wapo, na hata baada ya mahubiri hurusihusiwa kuingia.

Hata hivyo nimefurahishwa na utaratbu wanaoutumia wa kutenga sehemu za mbele kwa ajili ya watoto wadogo.Mabechi yao ni kama ya wakubwa tu. Nao huingia kanisani baada ya kutoa sadaka, nafikiri kabla ya hapo huwa na Sunday school (sina uhakika)halafu hupewa fursa ya kuimba angalau wimbo mmoja (waliimba kwa Kiswati).Pia hakuna matangazo yasiyo ya lazima na misa inaanza kwa wakati uliopangwa. Nilipomuuliza Chris Sibandze (siyo mkatoliki) kwanini vijana hawaendi kanisani alinijibu pengine wanavutiwa zaidi na makanisa yaliyoibuka siku hizi ambayo huendesha ibada hata kwenye viwanja vya mpira na hakuna anayejali na kinachoendelea!Nakushukuru sana Bw. Chris kwa kunipeleka kanisani.Katikati ya jiji hili la Mbabane ndipo lilipo Kanisa Katoliki Mt.Dolorosa.

Saturday, March 24, 2012

Maguga Dam kivutio cha watalii

Serikali ya Swaziland inaendelea kuendeleza Mradi wa Bwawa la Maguga kuwa kivutio cha watalii. Tayari mwekezaji amefungua mgahawa wa kisasa kando ya bwawa hilo. Banzi wa Moro alipotembelea Maguga alikuta pia maandalizi ya kujenga sehemu ya kucheza ngoma za asili.Bwawa la Maguga
Kutoka kushoto Elias Shosi, Banzi wa Moro na Collins Kamalizeni mhadhiri wa Mananga Centre
Mgahawa
Ndani ya mgahawa

Ng'ombe wa Swaziland

Ng'ombe ni alama ya utajiri kwa Waswati.Hutunzwa vizuri na nyama yake kwa kweli ni tamu. Utaratibu uliowekwa na serikali ya Swaziland inapojengwa barabara kuu ni kuwekwa uzio wa sengénge ili ngómbe na wanyama wengine wasivuke barabara na kugongwa.

Vijana wa Kiswati wakionyesha machejo

Kucheza ngoma ya Kiswati inahitaji mazoezi ya nguvu.Miguu hurushwa juu sana na kushuka chini kwa kishindo kwa kufuata mdundo wa ngoma huku akina dada wakiimba. Inapofika zamu ya kina dada kucheza nao hurusha miguu juu ndiyo aina ya uchezaji ngoma kusini mwa Afrika.Huyo dogo katikati ni mwisho wa reli. Anapiga ngoma na kucheza kwa msisimko wa Kiswati!


Mhadhiri Collins Kamlizeni kutoka Mananga (shati jeupe) haamini macho yake.

Nyama choma Mantenga Cultural Village

Banzi wa Moro anageuza nyama iive haraka.Kulia ni Msajili wa Mananga Centre of Management Development Aunt Joyce.
Shosi naye ilibidi ageuze nyama na kuchagua kipande anachopenda! Katikati aliyevaa fulana ya punda milia ni Chris Sibandze.
Tulijiandaa na nyama zetu,ugali,juice na hata mvinyo kwa aliyependa!Kushoto mwenye shirt ya polo kijani ni Mhadhili wa IT chuoniMananga Bw.Simbarashe akisubiri mambo yawe sawa.

Chris Sibandze

Kwa waliosoma Mananga Centre of Management Development jina la Chris Sibandze si geni. Kwani kwa kawaida huyu ndiye anayekupkea kutoka airport ya Matsapha na kukufikisha chuoni. Ni mwelewa na anafanya shughuli nyingi. Unajua kazi yake, nchi yake na utamaduni wao.Utakueleza mambo mengi yanayohusu Swaziland ukitaka. Sijawahi kumuona akikunja uso.Pichani Chris akiwa kwenye banda kijiji cha utamaduni Mantenga akifurahi ngoma.

Sijasahau kilimo

Hapa nipo kwenye mradi unaojilikana kama Swaziland Water and Agricultural Development Enterprise (SWADE)Aina hii ya papai ilinivutia sana. Majani yake ni mapana na matunda yana ukubwa wa wastani lakini kila mti huzaa matunda mengi.Bei ya mche mmoja wa mpapai ni Emalangeni30 sawa na shilingi za kitanzania 6,000/=

Na hapa mimi na Mtanzania mwenzangu Bw. Elias Shosi tukiangalia vitalu vya mboga (vitunguu,nyanya,mipapai,kabichi,pilipili).Ukinunua mche unapewa risti hapohapo bustanini. Good management.Is n't it!

Manzini nayo

Hizi ni sehemu tu ya jiji la Manzini. Maisha hapa ni moto ukizubaa unaibiwa mwanangu siyo kama Mbabane jiji la utulivu.Hata hivyo nyumba za kupanga hapa bei ni poa kuliko Mbabane. Mbabane ni mji wa wazito!


Jiji la Mbabane-Swaziland


Jiji la Mbabane nchini Swaziland na Makao Makuu ya Serikali na Manzini ni jiji la biashara.Mbabane imejengwa mlimani. Hapa hakuna viwanda ni nyumba za ofisi za kazi, nyumba za kuishi na nyumba za biashara.

Msichana wa Kiswati akionyehsa umahiri wake wa kucheza ngoma


Jumamosi ya tarehe 17/3/2012 Chuo cha Mananga kilituandalia safari ya kutembelea kijiji cha Utamaduni cha Mantenga ambacho hakipo mbali sana na Chuo. Baada ya kuelezwa maisha ya asili ya familia ya Kiswati tulipata burudani ya ngoma ya asili. Pichani mwanadada akionyesha umahiri wake katika kucheza ngoma ya Kiswati.

Lazima uwasilishe Mpango Kazi

Chuo cha Menejimenti cha Mananga Swaziland kina utarartibu mzuri kwa wote wanaopata mafunzo ya muda mfupi chuoni hapo. Kabla ya kuhitimu ni lazima uwasilishe Mpango Kazi (Action Plan) utakaoutekeleza mara urudipo kazini kutokana na majukumu yako na tatizo lilopo na madhumuni ya kutatua tatizo hilo kwa lengo lililowekwa. Jana wahitimu waliwasilisha Action plan zao.Pichani Elias Shosi kutoka Wizara ya Fedha, Tanzania akiwasilisha Mpango Kazi wake.
Mcebo Dlamini kutoka Swaziland
Bi.Bonisiwe Mabuza kutoka Swaziland
Chuo cha Menejimenti cha Mananga Swaziland kina utarartibu mzuri kwa wote wanaopata mafunzo ya muda mfupi chuoni hapo. Kabla ya kuhitimu ni lazima uwasilishe Mpango Kazi (Action Plan) utakaoutekeleza mara urudi kazini kutokana na majukumu yako na tatizo lilopo na madhumuni ya kutatua tatizo hilo kwa lengo lililowekwa. Jana wahitimu waliwasilisha Action plan zao.

Mfalme wa Kariakoo-Matombo?


Hapana. Hili ni vazi la Taifa la Kiswazi.Mfalme huvaa hivi, watemi(chiefs) huvaa hivi ni vazi lenye hadhi. Waswazi hulipenda vazi lao hawaoni aibu ndiyo utamaduni wao. Halikuja kwa kuundiwa kamati!