Mara nyingi huwa nasoma Blog ya Mjengwa. Pia namfahamu Mjengwa tangu wakati akiwa anaandikia gazeti la RAI, alipokuwa SWEDEN na kuna wakati alinitembelea nilipokuwa naishi Temeke Veterinary.Aliwahi pia kusaidia jezi Klabu yetu ya Mpira ya BERLIN (MILA)ya Temeke Veterinary.
Kwa jinsi ninavyomfahamu, Mjengwa ni Mzalendo na anauchungu wa nchi hii. Hana makuu. Atakuonyesha alipokuwa anaishi-Kinondoni kwa mama yake, marafiki zake, chakula anachopenda na hujali sana muda na ahadi. Maggid akisema atakutemebelea ni kweli atafika kwa muda uliopangwa.
Tangu aliporudi nchini Maggid hakosi kwenda nyumbani kwao Nyeregete-Mbarali ambako ni asili ya baba yake huko kuna dada zake, kaka zake, baba wakubwa na wadogo shangazi zake, babu na majirani.Nafahamu pia mama yake Maggid ni Mzaramo. Kwa kufanya hivyo, Maggid anawafahamu watu wake, ndugu zake,mazingira wanamoishi,uzalishaji wao. Anajitahidi kwa kila hali kuwatoa mahali walipo na kuwafikisha mahali fulani hata kama kwa uelewa tu. Angalia daraja analovuka ili kufika kijijini kwao Nyeregete! Hayo yote Mjengwa haandiki kufurahisha watu anataka watu wafahamu hali halisi ya vijiji vyetu. Mjengwa si Mbunge! Lakini amethubutu (Picha zote kwa hisani ya Mjengwa BLOG
Mjengwa na dada yake nyumbani kwao Nyeregete
Mjengwa akiwa na walimu na wanafunzi kijijini kwao Nyeregete
No comments:
Post a Comment